Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kwa nini Kondoo wake humfuata kwa furaha

    Mchungaji wa nchi za mashariki hakuwa akifukuza kondoo kwa kutumia fimbo yake. Hakuwatisha kondoo kwa kuwasukuma, ila yeye alikuwa akiwatangulia kondoo, nao humfuata nyuma yake. Ndivyo hivyo na Mchungaji ambaye ni Mwokozi. Husema: “Nimekupenda upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.” Yeremia 31:3.TVV 273.1

    Wanafunzi wa Yesu hawamfuati kwa kuogopa adhabu yake, au kwa kutamani zawadi yake. Humfuata kwa ajili ya upendo wake uliodhihirishwa kwake, tangu kuzaliwa katika Bethlehemu, ndani ya hori, mpaka kufa kwake Kalwari juu ya msalaba. Onekano lake huvutia watu na kuwaburudisha kabisa. Upendo huamshwa moyoni mwa mtu, naye husikia sauti yake na kumfuata.TVV 273.2

    Mchungaji hutangulia mbele ya kondoo zake, na kukumbana kwanza na hatari zilizoko mbele. Hivyo ndivyo Yesu anavyofanya kwa watu wake. Njia ya mbinguni hutakaswa na nyayo za Mwokozi.TVV 273.3

    Ingawa sasa anaishi katika utukufu wa mbinguni, Yesu hakupoteza hali yake ya fadhili. Leo mikono ile iliyopigiliwa na misumari, huonyeshwa ili kuwabariki watu wake waliomo ulimwenguni. Asema: “Hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakayewapokonya toka mikononi mwangu.” Mtu yeyote atakayejitolea kwa Kristo huwa wa thamani kabisa kuliko ulimwengu wote. Yesu hatamwacha mtu yeyote aliyemfia. Atawashikilia kabisa, isipokuwa watu wake wamwache wenyewe.TVV 273.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents