Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mheshimiwa Simeoni Alimtambua Yesu

  Simeoni alipoingia hekaluni, alijisikia kikamilifu kwamba, mtoto aliyetolewa na kuwekwa wakfu kwa Bwana, ndiye aliyeahidiwa na kungojewa kwa muda mrefu. Kuhani ambaye alipigwa na bumbuazi walishituka na kuingiwa na kiwewe cha furaha. Alimchukua mtoto mkononi mwake, hali akijaa furaha kubwa sana, ambavyo hajapata kuwa nayo. Alipomwinua mtoto, ambaye ni Mwokozi kuelekea mbinguni, alisema, Bwana, sasa mtumshi wako, na alale kwa furaha na amani, kama neno lako lilivyo: maana macho yangu yameona wokovu wako, uliowaandalia watu wote, ambayo ni nuru ya kuwaangazia watu ambao ni wa mataifa, na utukufu wako kwa watu wako Israel.TVV 25.2

  Wakati Yusufu na Mariamu walipokuwa wamesimama hali wakiyastaajabia maneno hayo, alimwambia Mariamu, “Angalia, mtoto huyu amewekwa ili kuwaangusha na kuwainua watu wengi katika Israeli na ishara inenwayo (Wewe upanga utakupasua moyo wako pia) ili mawazo ya wengi yapate kufunuliwa.TVV 25.3

  Vile vile Anna, nabii mke aliingia, akayaunga mkono maneno ya Simeoni. Uso wake uling’aa kwa utukufu, akatoa shukrani kwamba, ameruhusiwa kumwona Kristo Bwana.TVV 25.4

  Watu hawa wanyenyekevu, wamejifunza unabii. Lakini makuhani walidhani kuwa walikuwa na unabii wa thamani, kumbe hawakutembea katika njia ya Bwana. Macho yao hayakufunguliwa ili waone nuru ya maisha.TVV 25.5

  Hivyo ndivyo ilivyo hata leo. Wakaaji wa mbinguni wameleta mambo yote, ambayo wenye dini wangaliongozwa na waongozi wao kuyafuata. Watu wanamkiri Kristo katika historia. Lakini Kristo kuhusu ufukara na mateso, hawamkubali. Inakuwa hali ile ile iliyokuwako katika muda ule wa miaka elfu mbili iliyopita.TVV 25.6

  Mariamu alipokuwa akimwangalia mtoto mchanga mikononi mwake, na kuyakumbuka maneno ya wachungaji, alikuwa na tumaini la hakika. Maneno ya Simeoni yalimkumbusha maneno ya nabii Isaya: Watu waliokaa gizani, wameona nuru kuu nao wanaokaa katika uvuli wa mauti, nuru imewazukia. “Tumezaliwa mtoto, nasi tumepewa mtoto wa kiume, na ukuu utakuwa begani mwake, jina lake ataitwa Wa ajabu, mshauri wa ajabu, Mungu hodari, Baba wa milele, Mkuu wa amani.” Isaya 9:2-6.TVV 26.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents