Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Yesu alimsaidia mama yake

  Walipotoka Yerusalemu, Yesu alitumaini kuwaelekeza wazazi wake juu ya unabii unaohusu mateso ya Mwokozi katika msalaba wa Kalwari. Alitumaini kupunguza huzuni ya mamaye. Alikuwa akimfikiria sana. Maana Mariamu atakuwako kuyaona mateso yatakayompata. Na Yesu alitaka afahamu kazi yake hasa, ili wakati huo asije akazimia kwa huzuni. Kama angefahamu kazi yake, angemsaidia jinsi gani kustahimili mateso ya Yesu! Kule kutojali wajibu wao kwa siku moja Yusufu na Mariamu, walimpoteza Mwokozi. Lakini iliwachukua siku tatu kumwona. Ndivyo ilivyo hata kwetu pia. Kwa njia ya maongezi hafifu, au kutojali maombi, tunaweza kumpoteza Mwokozi na inaweza kutuchukua siku nyingi kumpata tena.TVV 40.3

  Lazima tujihadhari tusije tukamsahau Yesu, tukapata hali ya kuwa wazembe, bila kuwa na mwungano wa mbingu kwa njia ya malaika. Viumbe hawa watakatifu hawawezi kutukumbusha mahali tulipomwacha Mwokozi, wala kututia hamu ya kuwa naye tena.TVV 40.4

  Wengi huhudhuria ibada za dini, na kujiburudisha kwa neno la Mungu, lakini kwa kutojali maombi ya kujitoa, hupoteza mibaraka. Kwa njia ya kujitenga na Yesu, huzuia nuru yake kutuangazia.TVV 40.5

  Inatufaa sana kuwa na saa moja kila siku kutafakari maisha ya Kristo. Tuyatafakari hatua kwa hatua, hasa maisha yake ya mwisho. Ndivyo matumaini yetu kwake, na upendo wetu kwake vitavuviwa Roho Mtakatifu. Kwa kuitazama tabia yake, tutabadilishwa; kufanana hivyo na kutoka utukufu hata utukufu. 2 Wakorintho 3:18.TVV 40.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents