Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mashindano ya Kushindania Ukuu

  Mwokozi aliwaambia, “Mtu yeyote atakaye kuwa wa kwanza kwenu, na awe mdogo kuliko wote, na kuwa miumishi wa wote.” Hawakufahamu aina ya ufalme wa Kristo, bila shaka hili ndilo lililokuwa asili ya mabishano yao. Lakini sababu hasa ilikuwa kubwa zaidi kuliko hilo. Hata walipokwisha kufahamu kabisa, swali lolote la mambo yaliyotangulia lingeweza kuamsha matatizo. Hivyo msukosuko ungeweza kuletwa kanisani, baada ya Kristo kuondoka. Kushindania ukuu, ulikuwa kazi ya juu juu ya nia ile ya ushindani mkuu ulioanzia mbinguni, uliosababisha Yesu kuja na kufa. Mbele yake ilitokea njozi ya Shetani aliyesema, “Nitafanana naye aliye juu.” Isaya 14:14. Tamaa ya ukuu ilileta mashindano katika baraza la mbinguni. Lusifa alitamani kupata uwezo wa Mungu, sio tabia ya Mungu. Alitafuta kupata ukuu, na kila mtu au kila kiumbe chenye nia hiyo, hutenda mambo kama hayo. Utawala wa Shetani ni wa mabavu. Kila mtu humhesabu mwingine kuwa ni ngazi yake ya kupandia kwenda kwenye ukuu.TVV 247.6

  Wakati Lusifa alipotafuta kulingana na Mungu, “kristo alijifanya kuwa hana utukufu, akajitwalia namna ya mtumwa, akawa mfano wa mwanadamu, na alipokuwa na umbo la mwanadamu akajinyenyekeza, akawa mtii mpaka mauti, nayo mauti ya msalaba.” Wafilipi 2:7, 8. Sasa msalaba ulikuwa mbele yake, na wanafunzi wake walikuwa wakijitafutia ukuu, wala hawakushughulikia na hali ya unyenyekevu aliokuwa nayo Bwana wao, wala hawakuelewa na maneno yake kuhusu unyenyekevu kwa ajili yao.TVV 248.1

  Yesu alijaribu kusahihisha maovu haya. Aliwaonyesha ni kanuni gani inayotakiwa katika ufalme wa mbinguni, na ukuu wa kweli ni upi. Wale waliojawa na kiburi na kujiona walikuwa wakijifikiria na zawadi watakayopata. Watu kama hao hawakufaa katika ufalme wa mbinguni, maana walionekana kuwa katika jamii ya Shetani. Kabla ya kupata heshima, kwanza kunyenyekea. Kupata cheo mbele ya wanadamu, mbingu huchagua watendakazi walio katika sehemu ya chini machoni pa Mungu. Mwanafunzi wafananaye na mtoto, ndiye afaaye zaidi katika kazi ya Mungu. Anayehitaji msaada wa mbinguni, atauomba kutoka katika kuongea na Kristo, ataondoka kwenda katika kazi yake, akiwa na msaada alioomba naye hufaulu pale watu wenye elimu zaidi wanaposhindwa.TVV 248.2

  Lakini watu wanaojitukuza wenyewe, wakijiona kuwa wanatosha kufaulu kazini na kuendesha mpango wa Mungu, Bwana huwaweka kando tu, wala hana haja nao. Kazi ya Mungu haisimami, bali huendelea kwa nguvu zaidi.TVV 248.3

  Haikutosha kuwafundisha wanafunzi wa Kristo namna ufalme wa Mungu ulivyo. Jambo kubwa walilohitaji ni kuongoka, na kubadilika mioyo yao. Yesu akimwita mtoto, alimweka kati yao, akamkumbatia mikononi mwake, akasema, “Msipoongoka, mkawa kama’ mtoto mdogo, hamtaingia katika ufalme wa mbinguni.” Hali isiyokuwa ya kutaka makuu, kujisahau nafsi, na kuwa na upendo kama mtoto mdogo, ndiyo hali yenye thamani machoni pa mbingu, nayo ndiyo inayoonyesha ukuu wa kweli. Katika miguu ya Yesu, fahari ya ulimwengu na ukuu wake husahauliwa. Matajiri na maskini, wasomi na wasio wasomi, hukutana pamoja kama watu walionunuliwa kwa damu ya thamani bila ubaguzi wa aina yoyote.TVV 248.4

  Mungu huweka muhuri wake kwa watu, sio kwa ajili ya vyeo walivyo navyo, ila kwa ajili ya ungano waliloungana na Kristo. “Nawe umenipa ngao ya wokovu . . . wako.” Kama mafao ya tabia ya mwanadamu, “Umenikuza.” Zaburi 18:35.TVV 249.1

  Maneno ya Mwokozi yaliwafanya wanafunzi wake wasijitumainie. Yohana aliamshwa aulize, kama matendo yake ni ya sawa, au namna gani. Alisema: “Bwana, tulimwona mtu mmoja akifukuza pepo kwa jina lako . . . sisi tulimkataza kwa sababu hafuatani na sisi.” Yakobo na Yohana walidhani kuwa kumkataza mtu huyo walikuwa wakimtetea Bwana wao; kumbe sivyo.TVV 249.2

  Walianza kufahamu kuwa kufanya hivyo walikuwa wakiona wivu kwa ajili yao wenyewe. Walikubali kosa lao, na kukubaliana na makemeo ya Yesu. Bwana aliwaambia: “Msimkataze, maana hakuna awezaye kufanya miujiza kwa jina langu, kisha akawa kinyume changu.” Watu wengi walivutiwa na tabia pamoja na kazi ya Kristo, ambao walimwamini. Wanafunzi inawapasa kuwa waangalifu sana ili wasiwakatishe tamaa hawa watu. Lazima waonyeshe fadhili kama zile walizoona Bwana wao.TVV 249.3

  Kristo ni Mwalimu Mkuu; nasi twapaswa kukaa miguuni mwake na kujifunza kwake. Kila mtu aliyevutwa na Mungu ni mfereji wa kupitishia upendo wa Yesu na kuwafikia wengine. Ingelupasa kuwa waangalifu kadiri gani ili kusudi tusije tukawakatisha wachukuzi nuru wa Mungu na kuvuruga nuru ambayo wangeangaza ulimwenguni!TVV 249.4

  Kitendo kama cha Yohana cha kumkataza afanyaye miujiza kwa jina la Yesu, kingeweza kupoteza mtu. Yesu alisema kuhusu jambo hili. “Ni heri kama angefungiwa jiwe, shingoni mwake na kutupwa kilindini mwa bahari.”TVV 249.5

  Mbona kusema maneno haya magumu? Kwa sababu “Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilicopotea.” Luka 19:10. Je, wanafunzi wake wataonyesha roho ya ubinafsi kwa wenzao, kuliko Bwana wa mbinguni alivyoonyesha roho ya fadhili kwa watu? Dhambi ya kumkosesha mtu ni kubwa kadiri gani? Kwa mtu huyu kilio na masumbuko ya Mwokozi yalikuwa bure. Ni dhambi kubwa mno!TVV 249.6

  Ole ni wa ulimwengu kwa ajili ya mambo ya kukosesha. Mambo ya kukosesha hayana budi kuja. Ulimwengu utawapinga wafuasi wa Kristo kwa hakika. Lakini ole wa mkristo afanyaye mambo haya. Watu wengi hudanganywa na kupotoshwa na wale wanaojidai kuwa ni wafuasi wa Kristo, hali wakipotosha tabia yake.TVV 250.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents