Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sadaka isiyo na Kifani ya Mjane Maskini

    Kristo aliwakaripia wenye kuharibu mali, lakini alikuwa mwangalifu kwa watu wanaotmiza wajibu wao kuhusu kutumia mali. Matumizi mabaya ya matoleo ya Mungu yasingelizuia mibaraka ya Mungu kutoka kwa mtoaji.TVV 344.2

    Yesu alikuwa ukumbini, akiwatazama waliokuwa wakitoa sadaka zao. Matajiri walileta fedha nyingi kwa majivuno. Yesu aliwatazama kwa masikitiko ila hakusema neno kuhusu sadaka zao kubwa. Mara moja uso wake uling’aa alipomwona mjane mmoja maskini akija kwa kusitasita kana kwamba anawaogopa watoaji.TVV 344.3

    Aliangalia sadaka yake katika mikono yake. Ilikuwa ndogo sana kulinganisha na sadaka za wengine, walakini ilikuwa ndiyo yote aliyo nayo. Aliweka vipande viwili vya fedha kwa haraka, akaondoka. Alipofanya hivyo alikutanisha macho na Yesu aliyekuwa akimwangalia kwa makini.TVV 344.4

    Mwokozi aliwataka wanafunzi wake wamwangalie mjane huyu maskini. Kisha maneno yake ya sifa yakasikika masikioni mwa yule mjane. “Hakika nawaambia huyu mjane maskini: ametia zaidi kuliko wote.” Machozi ya furaha yakamlengalenga, alipofahamu kuwa sadaka yake imekubalika. Watu wengi wangalimshauri kuwa aache kutoa, atumie tu maana isingelitambulikana miongoni mwa sadaka nyingi za thamani kubwa zilizoletwa katika hazina. Lakini aliamini kuwa huduma ya hekaluni imeamuriwa na Mungu, naye alitaka kuisaidia huduma hiyo kwa kadiri awezavyo. Alitenda alivyoweza, na sadaka yake ilikuwa ukumbusho wakati wote, na furaha yake ya milele. “Ametia zaidi kuliko wote.” Sadaka kubwa ya matajiri haikuwa ya kujinyima, kwa hiyo haikuweza kuhesabika kwa thamani kama ile ya mjane maskini.TVV 344.5

    Nia huongoza matendo yetu, ikiyafanya yawe mazuri au yawe mabaya. Matendo madogo yatendwayo kwa furaha, na sadaka zitolewazo bila majivuno, huwa ya thamani mbele za Mungu. Mjane maskini alijinyima chakula chake ili kutoa senti mbili hizo kwa kazi aliyoipenda sana. Alifanya hivyo kwa imani, akiamini kuwa Baba wa mbinguni hawezi kumnyima riziki yake. Huduma hii isiyokuwa ya ubinafsi, na imani kama ya mtoto mdogo, ilisifiwa na Mwokozi.TVV 345.1

    Watu wengi miongoni mwa katika maskini hutamani kuonyesha shukrani zao kwa Mungu kwa ajili ya neema yake na kweli yake. Watu kama hao hebu na wakusanye senti zao chache na kuziweka katika hazina ya mbinguni. Ikiwa watazitoa kwa moyo mkunjufu, uliyojaa upendo wa Munngu, vitu vidogo hivi vikitolewa sadaka, Mungu huvifurahia na kuvibariki.TVV 345.2

    Yesu aliposema kwa mjane yule kuwa, “Ametia zaidi kuliko wote”, maneno yake yalikuwa ya kweli, siyo kwa nia tu, bali pia kwa matokeo ya sadaka yake. Zile senti mbili hizo zilizoletwa hazinani, zilizidi matoleo ya Wayahudi matajiri. Sadaka ndogo hiyo imekuwa kijito kilicho panuka na kuzidi kima kwa karne zote. Kwa njia elfu elfu mbali mbali imekuwa msaada kwa wenye dhiki, na kuitegemeza injili. Kielelezo chake cha kutoa kwa kujinyima kimeigwa katika nchi zote na watu maelfu katika kila karne. Mbaraka wa Mungu kwa sadaka ile ya mjane umeifanya kuwa na matokeo makubwa sana. Ndiyo ilivyo na kwa sadaka zote zitolewazo kwa utukufu wa Mungu. Matokeo yake hayahesabiki na mwanadamuTVV 345.3

    “Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki, kwa kuwa maana mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani adili na rehema na imani, hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.” Yesu hakuacha kuhimiza mambo ya lazima. Kulipa zaka kuliamuriwa na Mungu nako kulitekelezwa tangu mwanzoni. Ibrahimu alilipa zaka katika mali zake zote. Mpango wa kulipa zaka jinsi Mungu alivyouweka ulikuwa safi na wa haki, lakini Makuhani na Walimu walikuwa wameufanya kuwa mzigo wa kusumbua.TVV 345.4

    Mafarisayo walikuwa wakilipa zaka kamili ya mazao ya bustani zao, kama bizari, jira na mboga. Vitu hivyo viligharimu kidogo sana, na hivyo kuwapa sifa kwamba ni waaminifu kweli kweli. Lakini mambo makuu ya sheria, kama vile adili, rehema, na ukweli waliyaacha. Kristo alisema: “hayo imewapa kuyafanya wala yale mengine msiyaache.”TVV 345.5

    Mambo mengine ya sheria yalikuwa yamepotoshwa kwa jinsi hiyo na Walimu. Maagizo aliyoagizwa Musa, kama kula nyama ya nguruwe, na wanyama wengineo waliokatazwa yalitolewa ili kuepukana na maradhi na hivyo kufupisha maisha. Lakini Mafarisayo walipita kiasi. Watu waliambiwa wachuje maji yote yasije yakawa na wadudu, ambao wangehesabiwa sawa na wanyama wachafu. Yesu akilinganisha haya mambo madogo madogo na dhambi zenyewe hasa aliwaambia Mafarisayo “Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia.”TVV 346.1

    “Mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote.” Makaburi meupe yaliyopambwa yalificha maozea yaliyomo ndani yao. Ndivyo ilivyokuwa kwa makuhani na wazee waliokuwa wakionekana kwa nje kama wanyofu, walificha uovu ndani yao.TVV 346.2

    Yesu aliendelea kusema: “Mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki, na kusema: Kama sisi tungalikuwepo zamani za baba zetu, hatungalishirikiana nao katika (kumwaga) damu ya manabii”. Hivyo mwajishuhudia wenyewe kuwa ninyi ni wana wa wale waliowaua manabii”.TVV 346.3

    Ushirikina wa kuheshimu makaburi ya watakatifu ulidumishwa na fedha nyingi zilitumika katika kuyapamba. Machoni pa Mungu hii ilikuwa ni ibada ya sanamu. Ilionyesha kuwa hawakumpcnda Mungu hata kidogo, wala jirani zao kama nafsi zao. Leo watu wengi hawawajali wajane, na yatima, wagonjwa na maskini, ili kutoa gharama ya kujenga minara ya kumbukumbu kwa ajili ya watu. Wajibu kwa waliohai,wajibu ambao Kristo ameuagiza kwa dhati umeachwa bila kutendeka.TVV 346.4

    Mafarisayo walisema wao kwa wao: Kama sisi tungaliishi siku za baba zetu, tusingalishirikiana nao kumwaga damu za watumishi wa Mungu. Lakini wakati ule ule walikuwa wakipanga kumwua Mwana wa Mungu. Jambo hili linapasa kumfunua macho yetu tuone jinsi Shetani anavyowadanganya watu na kuwatoa katika njia ya kweli. Wengi hushangaa kwa upofu wa Wayahudi wa kumkataa Kristo. Husema: Kama sisi tungaliishi siku hizo za Kristo, tusingelishiriki katika hatia ya wale waliomkataa Mwokozi, lakini watu hawa wanapotakiwa kumtii Mungu na kuishi maisha yasiyokuwa ya ubinafsi, hukataa kufanya hivyo. Hudhihirisha roho ile ile ya Mafarisayo.TVV 346.5

    Wayahudi hawakutambua hata kidogo matokeo ya kutisha ya kumkataa Kristo. Katika kila kizazi manabii walipaza sauti zao kuwaonya watawala, wakuu, na watu, na hivyo wakihatarisha maisha yao katika kumtii Mungu. Kumekuwako na kurundikana kwa adhabu ya kufisha wale walioikataa nuru na kweli. Kwa kunikataa kwao Mwokozi makuhani na watawala walijihusisha na damu ya watakatifu wote kutoka Habili mpaka hadi Yesu mwenyewe. Wayahudi walikuwa karibu kukijaza kikombe chao cha uovu. Na karibu kitamwagwa vichwani mwao katika kulipiza haki. Kwa ajili ya hayo Yesu aliwaonya akisema: “hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki hata damu ya Zakaria na bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu Amini nawaambieni, Mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki.”TVV 347.1

    Waandishi na Mafarisayo walijua jinsi nabii Zakaria alivyouawa. Wakati alipokuwa akinena onyo kutoka kwa Mungu, ghadhabu ya kishetani ilimchochoea mfalme mwovu na kwa amri yake nabii akauwawa. (Tazama 2 Nyakati 24:18-22). Damu yake ilikuwa imejigandisha katika mawe ya hekalu, na kuwa ushuhuda wa uasi wa Israeli. Kadiri hekalu litakavyodumu kuwako, doa la damu hiyo itakuwa ikilia mbele za Mungu ili ilipiziwe kisasi. Yesu alipozighusia dhambi hizi, hofu kuu iliwajaza watu.TVV 347.2

    Yesu alipoona ugumu wa mioyo ya Wayahudi, alisema kuwa hali yao ya ngumu wa moyo itakuwa sawa kama ilivyokuwa wakati uliopita.TVV 347.3

    “Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii, na wenye hekima, na Waandishi: na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulubisha; na wengine wao mtawapiga masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji. “Yesu alitamka maneno haya ya adhabu hali mikono yake ikiwa imeinuliwa mbinguni, na nuru ya Uungu ikimfunika, Kristo alinena hayo kama jaji katika kukemea na hukumu. Wasikilizaji wake walitetemeka sana. Hali ya mvuto na maneno yake ilikuwa nanma isiyoweza kufutika kabisa.TVV 347.4

    Chuki ya Kristo hasa iliekezwa kwa dhambi zinazotendwa na watu wakijiharibu wenyewe, na kuwadanganya wengine na kumdharau Mungu. Lakini hakunena maneno ya kulipiza kisasi. Hakudhihirisha hasira yo yote. Huruma ya kimbingu ilionekana usoni pa Mwana wa Mungu, alipolitazama mara moja hekalu na kisha wasikilizaji wake. Kwa sauti iliyojawa na huzuni na majonzi mazito alitamka, “‘Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! ni mara ngapi nimetaka kuwa kusanya Pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabaya yake, lakini hamkutaka.” Katika maombolezo ya Kristo, moyo wa Mungu uliguswa. Hivyo ilikuwa kwaheri ya kisirisiri ya uvumilivu wa. upendo wa Mungu.TVV 347.5

    Mafarisayo na Masadukayo walinyamazishwa kimya. Yesu aliwakusanya wanafunzi wake wakatoka hekaluni, akiwa siyo kama mtu aliyeshindwa, bali kama ambaye ametimiza kazi yake. Aliondoka akiwa mshindi kutoka katika pambano.TVV 348.1

    Katika siku hiyo yaajabu, katika mioyo mingi mawazo mapya yalichipuka, na, historia mpya ikaanza. Baada ya kusulubishwa na kufufuka, watu hawa walijitokeza mbele wakiwa na hekima na bidii. Walikuwa na ujurnbe uliowavutia watu. Mbele ya ushuhuda wao dhana na falsafa za wanadamu zilikuwa hadithi za kubuni.TVV 348.2

    Lakini Israeli kama taifa lilikuwa limejitenga kutoka kwa Mungu. Akiangalia ndani ya hekalu kwa mara ya mwisho, Yesu alisema kwa huruma na kuomboleza! “Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa. Kwa maana nawambia, Hamtaniona kamwe tangu sasa, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.” Kama vile Mwana wa Mungu alivyozitoka zile kuta, Utukufu wa kuweko Mungu utaondolewa milele kutoka, katika hekalu lililojengwa kwa ajili ya utukufu wake. Tamasha zake hazitakuwa na maana, huduma zake zitakuwa dhihaka.TVV 348.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents