Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    19 — Yesu na Mwanawke Mwenye Waume Watano

    Yesu alipokuwa njiani kwenda Galilaya, alipitia Samaria. Alipofika katika kisima cha Yakobo, ilikuwa adhuhuri. Akiwa amechoka kwa safari hiyo, aliketi chini kando ya kisima, wakati wanafunzi wake walikwenda kutafuta chakula.TVV 97.1

    Wayahudi na Wasamaria walikuwa maadui. Wakati wa shida waliweza kuuziana vitu, hasa marabi. Lakini Myahudi hakuweza kukopa au kukopesha Msamaria. Hawakuhusiana kwa vyovyote. Wanafunzi katika kununua chakula, walifuata kanuni inavyotumiwa na taifa lao. Lakini kwa aina nyingine haikuwezekana hata kwa wanafunzi wa Yesu.TVV 97.2

    Yesu alipokuwa akiketi pale kisimani, alikuwa na njaa na kiu. Safari ilikuwa ndefu sana, na jua la saa sita za mchana lilimchoma sana. Kiu yake iliongezeka kwa vile alivyokuwa karibu na maji baridi yenye kuzima kiu, na hali yeye hana njia ya kuchotea maji katika kisima, kirefu jinsi hiyo.TVV 97.3

    Mara mwanamke wa Kisamaria alitokea, akiwa hana habari kuwa Yesu yuko. Akajaza chombo chake na maji. Alipokuwa akiondoka kurudi, Yesu alimwomba maji. Katika nchi za mashariki ombi la namna hiyo lisingefanyika. Kumpa maji msafiri ilikuwa huduma takatifu kwa Waarabu, ambao wangekuwa tayari kuifanya.TVV 97.4

    Mwokozi alikuwa akitafuta njia ya kuongea na mwanamke huyu ili amwambie Neno la Mungu. Kwa njia ya werevu wa upendo wa Mungu, alimwomba maji akitumaini kumvuta aamini. Mfalme wa mbinguni alikuja katika ulimwengu huu, akiomba huduma ya wanadamu. Yeye aliyeumba bahari, na kutawala vilindi vya maji, yeye anayefungua chemchemi za nchi, aliyetegemea fadhili za mgeni huyu ili ampatie maji.TVV 97.5

    Mwanamke alimwona Yesu kuwa ni Myahudi. Kwe mshangao wake, alisahau kumpatia alichoomba, ila alitaka kujua maana yake. Akasema, “Imekuwaje, wewe Myahudi kuniomba maji mimi Msamaria, ambavyo haiwi hivi?” Yesu akajibu: “Kama ungejua karama ya Mungu, na ni nani akuombaye maji, ungalimwomba yeye, naye angekupa maji ya uzima.” Kama ungeniomba mimi ningelikupa maji ya uzima wa milele.TVV 98.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents