Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mwujiza haukanushiki

  Hoja za Mafarisayo na chuki yao, pamoja na hali yao ya kutoamini viliwazibua watu, wakaona hali halisi ilivyo. Walijiuliza wenyewe kwa wenyewe wakisema, Yawezekana kwamba Mungu afanye jambo kubwa kama hili kwa njia ya mtu asiyemwamini, jinsi Mafa:risayo wanavyosema kuwa Yesu si mtu wa Mungu?TVV 268.4

  Mafarisayo hawakuweza kukanusha mwujiza huo. Mtu aliyekuwa kipofu alisimulia kisa chake kwa furaha sana na shukrani kubwa. Mafarisayo walijaribu tena kumkatisha tamaa ili anyamaze. Walisema: “Msifu Mungu, kwani tunajua ya kuwa mtu huyu Yesu ni mwenye dhambi.” Usiseme kuwa mtu huyu amekuponya, Mungu ndiye aliyekuponya. Kipofu akajibu: “Kwamba yu mwenye dhambi, au la, mimi sijui. Najua jambo moja tu, ‘nilikuwa kipofu. na naona.”TVV 268.5

  Wanafiki hawa walipojaribu kumkosesha mtu huyu asiamini, Mungu alimsaidia, akasimama imara, wala hakuyumbishwa yumbishwa. Aliwajibu akisema: “Niliwaambia tayari, hamkusikia?” Je, mnataka kuwa wanafunzi wake? Kisha walimtukana wakisema: “Wewe u mwanafunzi wake sisi tu wanafunzi wa Musa. Tunajua kuwa Mungu alizungumza na Musa, lakini mtu huyu hatujui atokako.”TVV 269.1

  Bwana alimpa neema na usemi wa kukata na kukemea unafiki wa Mafarisayo hawa, naye akawa mashahidi wa Kristo. Hapa Yesu alifanya mwujiza, na Mafarisayo walikiri bila kujua uwezo wake wa kufanya hivyo. Yule mtu akasema: . “Hii ni ajabu! Hamjui atokako, naye amenifumbua macho! Twajua kuwa Mungu hawasikii waovu, lakini mtu akiwa mcha Mungu na kutenda yampendezayo humsikia. Tangu mwanzo wa ulimwengu hatujasikia kuwa mtu amemfungua kipofu macho. Kama mtu huyu Yesu angekuwa mwenye dhambi, asingeliweza, kutenda lolote.”TVV 269.2

  Hoja ya mtu yule haikupata jawabu. Mafarisayo hawakupata la kujibu. Walinyamaa kwa muda. Kisha Makuhani na Marabi walimkemea kwa ghadhabu, wakisema: “Ulizaliwa katika dhambi, nawe sasa watufundisha sisi?” Wakamwondoa hapo.TVV 269.3

  Yesu aliposikia mambo waliyomfanyia, alipomwona, akamwambia: “Unamwamini mwana wa Mungu?” Kwa mara ya kwanza yule alimtazama Mwokozi uso kwa uso. Alikuwa amewaona wazazi wake, wakihangaika na kuwa na wisiwasi, alikuwa ameona nyuso za Marabi zenye shari, sasa macho yake yaliona uso mtulivu, uliojaa upendo, ambao ni uso wa Yesu. Yeye aliyekuwa akimwuungamia kwa shida na wasiwasi mkuu, sasa amemwona uso kwa uso.TVV 269.4

  Kwa swali la Mwokozi, yule mtu “Ni nani Bwana nipate kumwamini?” Yesu akasema: “Umemwona na ndiye unayesema naye.” Ndipo yule mtu akajitupa miguuni pake akamsujudia. Kristo alijidhihirisha kwa mtu huyu, na kumpokea kama aliyetumwa na Mungu.TVV 269.5

  Kundi la Mafarisayo lilikuwa limekusanyika hapo karibu, na Yesu akaona tofauti ya maneno yake na kazi yake ilivyo dhahiri. Yesu akasema: “Nimekuja ulimwenguni kwa hukumu, ili wanaoona wawe vipofu, na vipofu wapate kuona.” Watu wa siku za Mwokozi walikuwa na bahati ya kumwona Mungu kwa ukamilifu. Lakini katika bahati hii ilipita bure tu. Tabia zao zilipimwa, na maelekeo yao yalionekana wazi.TVV 269.6

  Baadhi ya wasikilizaji wake waliona kuwa maneno yanawahusu, kwa hiyo waliuliza: Sisi nasi vipofu? Yesu akajibu, “Kama mngalikuwa vipofu msingelikuwa na dhambi.” Kama Mungu amewawezesha kuona ukweli, kutojua kwenu kusingekuwa hatia. Lakini mwasema: “Tunaona.” Mwadhani kuwa mnaona, na kuikataa kweli ” Mafarisayo walikataa kuja kwa Kristo, wakaachwa gizani. Yesu alisema “Dhambi zenu zinakaa.”TVV 270.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents