Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    78 — Yesu Afa Juu Ya Kalwari

    “Na walipofika mahali paitwapo Golgotha, yaani Fuvu la kichwa ndipo walipomsulubisha yeye.”TVV 420.1

    Habari za kuhukumiwa Kristo zilienea, na watu wa hali zote walifurika kwenda mahali pa kusulibiwa. Makuhani na wakuu walikuwa wamefungwa kwa ahadi kwamba hawatawasumbua wafuasi wa Kristo ikiwa Yeye atatolewa kwao, na hivyo wanafunzi na waumini walijumuika kwenye msongamano huo.TVV 420.2

    Msalaba uliokuwa umetayarishwa kwa ajili ya Baraba, ulitwishwa katika mabega ya Yesu yaliyokuwa yakichuruzika damu. Wenzi wawili wa Baraba waliopaswa kusulubiwa pamoja naye nao walibebeshwa misalaba yao. Tangu alipokula Pasaka pamoja na wanafunzi wake, Yesu alikuwa hajala wala kunywa cho chote. Alikuwa amevumilia uchungu wa kusalitiwa, na alishuhudia wanafunzi wake wakimwacha na kutawanyika. Alikuwa amepelekwa kwa Anasi, kwa Kayafa, kwa Pilato, kwa Herode na kurudishwa kwa Pilato tena. Usiku ule wote palikuwapo tukio baada ya tukio kiasi cha kuweza kudhoofisha roho ya mtu hadi kuzimia. Lakini Kristo hakushindwa. Alikabili fadhaa zote kishujaa. Lakini baada ya kupigwa mara ya pili na kutwishwa msalaba hali ya kibinadamu haikuweza kustahimili zaidi. Alianguka, na kuzimia chini ya mzigo huo.TVV 420.3

    Makutano hawakuonyesha huruma yo yote. Bali walimdhihaki kwa kushindwa kubeba msalaba. Mara nyingine tena walimtwika msalaba mara ya pili, na akaanguka tena. Watesi wake wakaona kuwa hataweza kubeba mzigo wake zaidi. Ni nani ataubeba huu mzigo wa kudhalilishwa? Wayahudi wasingeliweza, kwa sababu ya kuhofia kutiwa najisi na hivyo kuzuiwa kushiriki Pasaka.TVV 420.4

    Katika wakati huo mgeni, Simoni, Mkirene akitokea vijijini alikutana na umati huu. Alisimama kwa mshangao wa lililokuwa linatendeka na alipoonyesha moyo wa huruma, walimkamata, na kumtwisha msalaba mabegani.TVV 421.1

    Wana wa Simoni walikuwa wafuasi wa Mwokozi, lakini yeye mwenyewe hakuwa mfuasi. Kuubeba msalaba mpaka Kalwari ulikuwa mbaraka kwa Simoni. Mbaraka huo ulimuongoza achukue msalaba wa Kristo na kwa hiyari na tangu hapo alisimama chini ya mzigo wake kwa furaha.TVV 421.2

    Sio wanawake wachache waliokuwemo katika umati ulimfuata asiye na hatia mpaka kufikia kifo chake cha ukatili. Baadhi yao walikuwa wamemletea wagonjwa wao na wenye kuteseka. Wengine walikuwa wameponywa wao wenyewe. Hivyo walishangazwa na chuki aliyoonyeshwa na makutano. Na bila ya kujali maneno makali ya makuhani na wakuu, pale Yesu alipoanguka na msalaba, wanawake hawa waliangusha kilio. Kristo aliguswa na kilio hiki. Alijua kuwa hawakumlilia kwa vile ni Mwana wa Mungu, lakini hata hivyo hakudharau kule kumhurumia kwao. Kilio chao kiliamsha huruma moyoni mwake kwa ajili yao, akasema; “Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu.” Kristo aliutazama wakati Yerusalemu utakapoangamizwa ambapo wengi katika hao waliokuwa sasa wanalia wataangamia pamoja na watoto wao.TVV 421.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents