Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Alichukua Hali zote za kibinadamu

    Watu wengi hudai kuwa haikuwezekana kwa Yesu kushindwa na majaribu ya Shetani. Kwamba hakuwa katika hali aliyokuwamo Adamu, wala hakuweza kushinda katika hali kama hiyo. Tungejua hali ya kutisha aliyokuwamo Kristo ndipo tungefahamu kuwa anatupita. Alichukua hali zote za ubinadamu pamoja na hali ya kushindwa na majaribu. Sisi hatuna udhuru wa jambo lolote ambalo Kristo hakukutana nalo, na kufaulu.TVV 58.1

    Kama kwa Kristo sawa na kwa wazazi wetu katika Edeni, jaribu la uchu wa chakula, lilikuwa la kwanza kutajwa. “Alipokwisha kufunga siku arobaini mchana na usiku akaona njaa. Na mjaribu alipomjia, alisema, Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mkate.”TVV 58.2

    Maneno haya ya kwanza yaliisaliti tabia yake. “Kama wewe ni Mwana wa Mungu.” Hilo lilikuwa neno la kutoamini lililopenyezwa hapo. Kama Yesu angefanya maneno aliyosema Shetani angelikubali neno la mashaka lililotolewa na Ibilisi. Shetani alifikiri kuingiza neno katika mawazo ya Hawa neno la shaka kuhusu tunda zuri, liwe kinyume cha vile Mungu alivyosema juu yake. Hivyo ndivyo mjaribu alivyofanya kuleta hila yake: akasema, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu.” Katika sauti yake kulikuwa na mashaka kabisa. Je, Mungu angemwacha Mwanawe akae katika jangwa kati ya wanyama, bila chakula, wala maji? Alipenyeza neno la mashaka kwamba Mungu asingalifanya namna hiyo, kwa hiyo alisema, “kama wewe ni Mwana wa Mungu”, onyesha uwezo wako, kwa kuyaamuru mawe haya yawe mkate.TVV 58.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents