Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jinsi Mungu anavyotenda

    Simon hakung’amua kuwa Mwana wa Mungu sharti atende sawa sawa na Mungu, kwa huruma, wema, na msamaha. Fikira za Simoni zilikuwa za kutozingatia huduma ya toba ya Mariamu. Kitendo cha Mariamu kuibusu miguu ya Kristo na kuipaka mafuta kilichochea ugumu wa moyo wa Simoni. Alifikiri kuwa Kristo anapaswa kuwatambua wenye dhambi na kuwakemea.TVV 316.4

    Kwa mawazo hayo ya Simoni, Mwokozi alijibu “Simon, nina neno nitakalo kukuambia. Akasema, Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili, mmoja amwia dinari mia tano, na wa pili hamsini. Na walipokuwa hawana cha kumlipa, aliwasamehe wote wawili. Katika hao wawili ni yupi atakayempenda zaidi? Simon akajibu, akasema, “Nadhani ni yule aliyesamehewa nyingi.” Akamwambia “Umeamua haki.”TVV 316.5

    Kama alivyofanya Nathani kwa Daudi (2 Samweli 12:1-7), Kristo alimtupia mkaribishaji wake mzigo wa kujihukumu yeye mwenyewe. Simon ndiye aliyemuongoza kutenda dhambi mwanamke huyu anayemdharau sasa. Simon ndiye alimkosesha hasa. Mfano uliosemwa juu ya wadeni wawili, ulihusu Simon na Mariamu. Yesu hakutaka kufundisha kwamba tofauti za matakwa zingeonekana baina ya watu wawili, maana kila mtu alipaswa kushukuru kwa yale aliyosamehewa. Lakini Yesu alitaka kuonyesha kuwa Simon alikuwa na dhambi kubwa kuliko ya Mariamu, kama vile deni la dinari mia tano linavyozidi deni la hamsini. Simon sasa alinza kujiona katika nuru mpya. Aliona jinsi Mariamu alivyofikiriwa na yule aliyekuwa zaidi ya nabii. Akaaibika sana, akatambua kuwa alikuwa mbele ya Mtu mkuu kuliko yeye mwenyewe.TVV 316.6

    Kristo aliendelea kusema, “Niliingia nyumbani mwako, wala hukunipatia maji ya kuosha miguu yangu, lakini Mariamu kwa moyo wa kutubu ameniosha miguu yangu kwa machozi, na kuifuta kwa nywele za kichwa chake. “Hukunibusu, lakini mwanamke huyu, ambaye unamdharau, tangu nilipofika hakuacha kubusu miguu yangu.” Kristo alihesabu muda ambao Simon alioupata wa kuonyesha kuwa Bwana amemtendea mema kiasi gani. Mchunguza mioyo aliona kilichomfanya Mariamu atende kitendo hicho. Aliona pia kilichomfanya Simon aseme maneno ya jinsi hiyo. Yesu alisema, “Wamwona mwanamke huyu?” Nakuambia, “Dhambi zake ambazo ni nyingi zimesamehewa, kwa kuwa amependa sana. Lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo.”TVV 317.1

    Simon alidhani kuwa amemheshimu Yesu kwa vile alimkaribisha nyumbani kwake. Lakini sasa ameona ukweli wa mambo ulivyo. Aliona kuwa dini yake ilikuwa ni vazi la Kifarisayo tu. Alikuwa amedharau wema wa Yesu. Hakumtambua kama mjumbe wa Mungu. Mariamu alikuwa mwenye dhambi aliyesamehewa, lakini yeye alikuwa mwenye dhambi ambaye hakusamehewa.TVV 317.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents