Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jambo lolote likoseshalo litupwe mbali

    Dhambi moja ikipendelewa na kuhifadhiwa na mtu inatosha kupotosha tabia ya mtu na kuwakosesha wengine. Kama mguu au mkono ungekatwa au jicho kung’olewa ili kuuokoa mwili usiangamie, tungekuwa na juhudi kadiri gani kuacha dhambi zinazotuangamiza!TVV 250.2

    Katika huduma ya kafara, chumvi ilitiwa katika kila sadaka iliyotolewa. Kama iliyokuwa sadaka ya manukato hii ilionyesba kuwa haki ya Kristo peke yake ndiyo iliyofanya huduma yoyote ikubalike mbele za Mungu. Kuhusu jambo hili Yesu alisema: “Mwe na chumvi ndani yenu, na mwe na amani ninyi kwa ninyi.’ Wote lazima wawe na chumvi yenye kuokoa, yaani haki ya Mwokozi wetu. Hapo ndipo watakuwa chumvi ya ulimwengu”, wakizuia maovu yasitendwe na watu, sawa kama chumvi inavyozuia kuharibika.” Mathayo 5:13. Lakini kama chumvi imeharibika, maisha ya mtu hayawezi kuwavuta watu kuelekea katika uzima. Yesu alisema: ‘Inawapasa ninyi kuwa washiriki wa neema yangu, ili mpate kuwa wenye mvuto uelekeao kwenye uzima. Ndipo hapatakuwapo naushindani, au ubinafsi, wala kutamani ukuu.’ Tunapomwona Yesu kama Mtu wa Huzuni, ajuaye sikitiko, akifanya kazi kuokoa ulimwengu uliopotea, akidharauliwa na kudhihakiwa, akifukuzwa toka mji hata mji mpaka kazi yake imalizike, tunapomwangalia katika Gethsemane akitoka jasho la damu, na katika msalaba akifa kifo cha uchungu mzito, tuyaonapo haya, ubinafsi hautatusogelea, tutabeba msalaba kwa furaha kumfuata Yesu, na kustahimili yote, majaribu, aibu, mateso kwa ajili yake.TVV 250.3

    Hakuna mtu anayemwamini Kristo atakayehesabiwa kuwa hana thamani. Wote tuliopewa elimu, uwezo, uzuri wa tabia, utawa, tunalo deni kwa wale wasiopewa nafasi kama yetu. Lazima tuinue mikono ya watu kama hao. Malaika huwajia watu wale wanaopigana na hali ya ubinafsi, wenye makasoro ya tabia, ambao hupigana sana ili kurekebisha tabia hiyo ambao mazingara yao ni mazito sana. Hata hivyo watu hawa hujitia hivyo katika huduma ya Kristo.TVV 250.4

    Yesu alisema: “Mwaonaje, mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akipotea, hawaachi wale tisini na lisa, akaenda milimani na kumtafuta yule aliyepotea, hata amwone? Na akimwona, nawaambieni, hufurahi sana kuliko wale tisini na tisa ambao hawakupotea. Vivyo hivyo na Baba yangu aliye mbinguni hufurahi kwa ajili ya mmoja wapo wa watoto hao, asipotee.”TVV 251.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents