Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Jinsi Roho Mtakatifu Anavyofanikisha Kazi va Kristo Kwa Ajili Yetu

  Kabla Kristo hajajitoa kuwa kafara ya wenye dhambi, alitafuta zawadi muhimu . . . atakayowapa wafuasi wake Alisema: “Nami nitamwomba Baba, naye alawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu (Yohana 14:16-18). Wakati Kristo alipokuwa hapa duniani, wanafunzi hawakuwa na haja na mfariji mwingine. Hata atapokwisha kupaa, ndipo watajisikia wanahitaji Roho, na ndipo Atikapokuja.TVV 379.1

  Roho Mtakatifu ni mwakilishi wa Kristo, lakini asiyekuwa na hali ya kibinadamu na hivyo huru. Kristo alipokuwa na mwili wa mwanadamu hakuweza kuwa mahali popote kwa wakati uleule. Kwa hiyo ilikuwa kwa manufaa yao kwa Yesu kuondoka na kutumwa Roho badala ya Yesu Hivyo, hakuna ambaye angenu-faika kutokana na mahali alipo. Kwa njia ya Roho Mtakatifu Kristo angepatikana kwa wote.TVV 379.2

  Yesu alisoma mambo ya mbele ya wanafunzi wake. Aliona kuwa mmoja atanyongwa, mwingine atasulibishwa msalabani, mmoja atafungwa kisiwani katikati ya bahari wengine watateswa na kuangamizwa. Lakini katika matatizo yote hayo Yeye atakuwa pamoja nao. Ikiwa mfuasi wake atapata matatizo kwa ajili ya kweli na kusimamishwa mbele ya mahakama dhalimu Kristo atasimama pamoja naye. Mashutumu watakayo shutumiwa yataanguka kwake. Ikiwa fulani atatupwa gerezani, Kristo atamfariji, kwa pendo lake.TVV 379.3

  Po pote tutakapokuwa na kwa wakati wo wote, tutakapojisikia wanyonge na hali ya upweke, Mfariji atatumwa katika kujibu ombi la imani. Katika hali fulani tunaweza kutengana na rafiki zetu wa dunia lakini hakuna kitu cha kututenga na Mfariji wetu wa mbinguni. Yuko pamoja nasi siku zote kututia nguvu na kutufariji. Bado Wanafunzi wakashindwa kuelewa maneno ya Kristo, na tena akaeleza: Kwa njia ya Roho atajidhihirisha mwenyewe kwao “Msaidizi huyo Roho Mtakatifu, ambaye na Baba, atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote.” Hamtaweza tena kusema kuwa sikuelewa.TVV 379.4

  Kristo alikuwa azungumze na watu wote duniani kwa njia ya wanafunzi wake. Lakini katika kifo cha Kristo wanafunzi walikuwa wakatishwe tamaa mno. Kusudi baada ya hali hiyo neno lao lipate kuwa hakika, Yesu aliahidi, kuwa Msaidizi atakapokuja “atawaku-mbusha yote, niliyowaambia.” “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote mtakayoyasikia atakayoyanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi; kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari” Wanafunzi wa Yesu walizoezwa kuyaamini maneno ya marabi kana kwamba ni maneno ya Mungu, na mambo hayo bado yalikuwa na mvuto akilini mwao. Hawakuelewa aina ya ufalme wa kiroho wa Kristo. Mafundisho yake mengi yalionekana kupita. Yesu aliahidi kuwa mambo haya yote watakumbushwa na Roho Mtakatifu. Msaidizi huitwa “Roho wa Kweli.” Kazi yake ni kufafanua na,kudumisha kweli. Kwanza hukaa moyoni kama Roho wa kweli na hivyo kuwa Msaidizi. Kuna faraja katika kweli lakini hakuna faraja katika uwongo.TVV 379.5

  Kwa mapokeo ya uongo Shetani hutawala akili za watu Kanuni hupotosha tabia. Roho mtakatifu hudhihirisha makosa, na kuyao-ndoa kutoka moyoni. Kwa njia ya Roho wa kweli, akitenda kazi kwa Neno la Mungu, Kristo huwatiisha kwake mwenyewe watu wake Aliowachagua.TVV 380.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents