Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wasiwasi wa watu ulitulizwa

    Asubuhi ya siku iliyofuata sikukuu, ilikuta watu wakiwa na uchovu wa sikukuu. Ghafla Yesu alipaza sauti yake na kusema: “Mtu akiwa na kiu na aje kwangu, kama maandiko yasemavyo, mito ya maji itabubujika tumboni mwake.” Watu walikuwa katika kuhangaika na mambo mengi tu, na kusikiliza nyimbo tu, lakini mioyoni mwao walikuwa hawana kitu cha kuwaridhisha na kuwatuliza.TVV 256.3

    Asubuhi hiyo makuhani walikuwa wamefanya ukumbusho wa mwamba uliotoa maji jangwani. Mwamba huo ulikuwa mfano wa yule atakayekufa, na kifo chake kiwezeshe mito ya maji ibubujike matumboni mwao, ambao ni wokovu. Mbele ya mkutano huo Yesu alijidhihirisha kuwa ndiye mwamba utakaopigwa na kuuletea ulimwengu wokovu. Yesu alipokuwa akisema haya watu walipata kicho cha namna ya ajabu. Wengi walikuwa tayari kusema kama mwanamke wa Kisamaria alivyosema: “Nipe na mimi maji haya, ili nisione kiu tena.” Yohana 4:15.TVV 256.4

    Wengi waliomsikiliza Yesu walikuwa wakilia kwa kutokuwa na matumaini, wakihangaika tu na mambo ya ovyo, huku wakitamani mambo ya dunia, lakini kati ya masikitiko yao ilisimama furaha ya kuridhisha mahitaji yao. Lakini sauti ile iliyosema: “Kama mtu akiona kiu, na aje kwangu”, na kusikiliza maneno yaliyofuata yalileta tumaini jipya. Waliona mfano uliokuwa mbele yao kuna toleo la mmoja asiye na kasoro la kupata wokovu. TVV 256.5

    Sauti ya Kristo kwa mtu aliye na kiu ingali inaendelea hata sasa. Sauti hiyo inatuita sisi kwa nguvu zaidi kuliko zamani, kwa watu waliosikia hekaluni ikinenwa na Yesu. “Mtu aliye na kiu na aje kwangu. Na yeyote atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.” Ufunuo 22:17.TVV 257.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents