Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uchungu mkali

  Mambo hayo yote yalionekana kuwa maajabu. Manong’onezo ya Shetani yaliusumbua moyo wa Yohana na kivuli cha hofu kilimwingilia. Je, inawezekana kuwa Mwokozi aliyengojewa kwa muda mrefu bado kufika? Yohana alikata tamaa vibaya kuhusu kazi yake. Alitumaini kuwa ujumbe kutoka kwa Mungu utawasisimua watu kama ule wa siku za Yosia na Ezra. (2 Mambo ya Nyakati 34; Nehemia 8), kwamba watu watatubu. Je, maisha yake ya kujitolea yamekuwa kazi bure? Je, kazi kwa wanafunzi wake imekuwa ya bure, bila matunda? Je, hakuwa mwa-minifu kazini, ndiyo sababu amekomeshwa? Je, kama Mwokozi aliyeahidiwa angekuwa amekuja, na Yohana amekuwa mwaminifu Yesu asingaliwatoa katika utumwa wa Warumi na Yohana kufunguliwa?TVV 117.1

  Walakini Yohana Mbatizaji hakuacha imani yake kwa Kristo ianguke. Sauti aliyosikia kutoka mbinguni, kushuka kwa mfano wa hua, maisha manyofu ya Kristo, Roho Mtakatifu aliyemjilia Yohana alipomjia Mwokozi, ushuhuda wa maandiko matakatifu, yote hushuhudia kuwa Yesu ndiye Mwokozi aliyeahidiwa.TVV 117.2

  Yohana aliazimu kutuma ujumbe kwa Yesu. Alituma wanafunzi wake wawili, akiamini kuwa kukutana na Yesu kutawaimarisha. Na yeye alitamani kusikia maneno kutoka kwa Yesu. Wale wanafunzi walimjia Yesu wakisema: “Je wewe ndiye yule ajae, au tumtazame mwingine?’ Swali hilo lilikuwa la kuonyesha uchungu na kukata tamaa. Kama Yohana ambaye ndiye mtangulizi wa Yesu, alishindwa kutambua kazi ya Yesu, je, ingetazamiwa nini kwa watu wapendao mambo ya ubinafsi?TVV 117.3

  Mwokozi hakulijibu swali hilo la wanafunzi mara moja. Walipokuwa wakisimama katika hali ya ukimya, wagonjwa na wenye maradhi walikuwa wanamjia Yesu ili awaponye. Vipofu, wenye maradhi mbalimbali walikuwa wakisongamana kumjia Yesu. Sauti ya Mponyaji mkuu ilipenya mpaka ndani ya kiziwi. Neno lake, mguso wa mkono wake, ulifungua macho ya kipofu. Yesu alikemea homa na maradhi yote. Sauti yake ilifika mpaka kwa mtu anayekufa, na wote wakachangamka, wakasimama. Alipokuwa akiwaponya wenye maradhi, watu maskini na wakulima ambao walikuwa wamepigwa marufuku na marabi, kama watu wasiotakiwa, walikuwa wakisongamana kuja kwake, naye akawazungumzia maneno ya uzima wa milele.TVV 117.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents