Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    40 — Usiku Ziwani

    Watu walikuwa wameketi katika majani ya uwanda, walipokuwa wakila chakula kile yesu alichowaandalia wakati wa machweo ya jua. Mwujiza wa kuzidisha mikate kuwa chakula kingi, uliwaingia wote mioyoni mwao. Mungu alikuwa amewalisha Waisraeli jangwani, na sasa ni nani huyu aliyewalisha hawa, isipokuwa ni yule aliyenenwa na Musa? Hivyo ndivyo walivyosemezana wao kwa wao. “Kwa kweli huyu ndiye nabii ambaye atakuja ulimwenguni.”TVV 206.1

    Tendo hilo mashuhuri lilikuwa ushuhuda wa Mkombozi aliyekuwa amengojewa kwa muda mrefu alikuwa kati yao. Huyu ndiye aliyefanya Uyahudi kuwa Paradiso ya duniani, nchi iliyojaa asali na maziwa. Anaweza kuvunja nguvu za Kirumi, ambao huchukiwa sana. Anaweza kuonya majeraha ya askari vitani. Anaweza kuwapatia jeshi zima la askari chakula. Anaweza kuwapatia Waisraeli dola inayotamaniwa kwa muda mrefu.TVV 206.2

    Watu walikuwa tayari kumtawaza awe mfalme. Walimwona kuwa hana bidii ya kujikweza, nao waliona mashaka kwamba hawezi kujishughulisha na mambo ya kutaka ufalme. Wakizungumza pamoja waliazimu kumtawaza kwa nguvu, ili awe mfalme wa israeli. Wanafunzi wake nao waliunga mkono kuwa mtu anayestahili kurithi kiti cha enzi cha Daudi ni mwalimu wao. iwe hivyo ili makuhani na wakuu ambao ni wenye majivuno makubwa, walazimike kumtii aliyekuja akiwa na uwezo wa Mungu.TVV 206.3

    Lakini Yesu aliona jinsi mambo yanavyokwenda. Kitakachofuata ni maasi na utumiaji wa nguvu, ambavyo vingeharibu mpango wa ufalme wa Mungu. Akaona kuwa hali hii ni lazima izuilike mara moja. Akawaita wanafunzi wake akawaagiza wapande mashua na kurudi Kapernaumu, na yeye abaki akiwaaga makutano.TVV 206.4

    Wakati wowote agizo la Yesu halijawa gumu la kutiwa kama hili. Hii ilionekana kuwa ndiyo nafasi hasa ya kumtawaza mpendwa wao, awe mfalme wa Israeli. Ilikuwa vigumu kwa wanafunzi kwenda peke yao na kumwacha mwalimu wao mahali hapo. Walipinga kwenda wenyewe, lakini sasa Yesu alitumia madaraka, ambayo haikuwa kawaida yake kufanya hivyo. Basi wakaondoka kimya.TVV 207.1

    Sasa Yesu akawaamuru watu waondoke, waende zao. Hali yake ilibadilika sana, wala hakuna mtu aliyesema neno lolote, wala kubisha. Wakati ule walipotaka kumshika ili wamtawaze, hatua zao zilishindwa kuondoka. Hali tukufu ya kuonekana kwa yesu, na maneno machache aliyosema kama mwenye mamlaka, yalibatilisha maazimio yao. Waliona kuwa alikuwa na mamlaka kupita watu wote, kwa hiyo hawakuwa na neno la kusema.TVV 207.2

    Walipoondoka na kumwacha yesu peke yake, alipanda mlimani akaomba. Aliomba muda mrefu, akiomba apate nguvu za kuwadhihirihia watu tabia ya Kimungu inayofanana na kazi yake, na kwamba Shetani asiwapofushe watu na kuwapotosha. Alijua kuwa siku zake duniani ziko karibu kumalizika, na watu wanaomwamini ni wachache tu. Wanafunzi wake watajaribiwa vikali sana, na matumaini yao yatatoweka. Badala ya kumwona akitawazwa kuwa mfalme, watamwona akisulubishwa msalabani Huku ndiko kulawazwa kwake; lakini hawakufahamu hayo, na pasipo msaada wa Roho Mtakatifu, imani yao itufifia. Kwa ajili ya wanafunzi wake aliwaombea kwa uchungu mkali na kulia.TVV 207.3

    Wanafunzi wake walikuwa hawajaenda mbali sana kutoka pwani, kwa kutumaini kuwa yesu atakuja. Lakini kadiri giza la usiku lilivyozidi kuongezeka, walisonga mbele, wakavuka bahari wakaenda kapernaumu. Walilalamika kwa sababu hawakupata nafasi ya kumtawaza kuwa mfalme. Walijilaumu kwa kutoka walipoambiwa. Kama wangesisitiza kukataa maazimio yao yangetimia.TVV 207.4

    Mashaka ya kutoamini yaliwajaa. Kutaka ukuu na heshima viliwapofusha. Walitamani kumwona Yesu akitawazwa kama walivyokusudia. Je, watadumu kuhesabika tu kuwa wafuasi wa nabii wa uongo? Kwa nini mwenye uwezo mkuu namna hii asijidhihirishe kwa wazi? na kwa nini hakumwokoa Yohana na mauti? Wanafunzi walitafakari mambo hayo mpaka wakajiletea giza mioyoni mwao. Wakajiuliza, inawezekana Yesu awe mtu laghai kama Mafarisayo wanavyodai?TVV 207.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents