Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Thawabu ya Kujitolea

    Yesu kabla hajawauliza wanafunzi kuacha mashua zao za kuvulia, alikuwa amewaambia kuwa Mungu atawapatia mahitaji yao yote. Matumizi ya mashua ya Petro ilikuwa ikimpatia mapato mengi sana. Yeye aliye tajiri wa kila kitu alikuwa amesema: “toeni, nanyi mtapewa, kipimo cha kujaa, na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kujaa.” Warumi 10:12; Luka 6:38. Katika kipimo cha namna hii ndicho Bwana alichomzawadisha Petro katika kazi yake. Na kila aina ya kujitolea katika kazi yake, italipwa sana. Soma Waefeso 3:20; 2:7.TVV 133.2

    Usiku huo wa wasiwasi katika ziwa, wanafunzi wakiwa peke yao, walikuwa na mashaka makuu. Lakini akiwapo pamoja nao, huburudika na kufurahi: Ndivyo ilivyo na kwetu pia. Tukiwa peke yetu bila Kristo, kazi yetu huwa kazi bure, na ni rahisi kunung’unika. Lakini tunapofanya kazi chini ya uongozi wake, hufurahi kwa uwezo wake. Hutuimarisha katika imani na tumaini. Yeye anayeweza kukusanya samaki baharini, kama alivyofanya kwa Petro na wenzake, huweza pia kuwavuta watu, ili watumishi wake waweze kuwa, “wavuvi wa watu.”TVV 133.3

    Kristo alikuwa anao uwezo wa kuwawezesha watu wasio na elimu, kama wavuvi, ili wawe hodari na kuwa na madaraka kama hayo waliyokuwa nayo. Mwokozi hadharau elimu, ambayo hutawaliwa na upendo wa Mungu. Uwezo wa elimu ni baraka. Lakini wenye akili wa wakati wake walikuwa watu wenye kujitegemea wenyewe, hata hawakuweza kuafikiana na’ mtu wa Nazareti. Walidharau kufundishwa na Kristo. Kitu cha kwanza ambacho wote wanapaswa kujifunza ni kutokujitegemea, hivyo hujiandaa kuvikwa tabia ya Kristo. Hali hii haipatikani kwa elimu ya sayansi inayofundishwa katika shule.TVV 133.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents