Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  38 — Kristo na Wanafunzi Wapumzika

  Waliporudi kutoka katika safari yao ya mahubiri, wanafunzi walikuja kwa Yesu kumsimulia mambo ya safari yao, jinsi walivyofanya, na mafundisho waliyofundisha. Yesu aliwaambia: “Njooni peke yenu mahali pasipokuwa na watu mpumzike kidogo.”TVV 198.1

  Uhusiano wa wanafunzi na Yesu ulikuwa mkubwa sana. Walimweleza mambo yote ya kazi yao ya kuhubiri, mafanikio yao na matatizo yao pia. Kwa jinsi walivyomweleza mambo kwa wazi, aliona kuwa wanahitaji mafundisho zaidi.TVV 198.2

  Lakini mahali walipokuwapo hapakufaa, maana watu wengi walikuwa wakiingia na kutoka mfululizo, wala hakuna nafasi ya kula. Watu walikuwa wakimfuata Kristo, ili awaponye maradhi yao, na kutaka kumsikiliza. Kwa wengi alionekana kuwa ni asili ya mibaraka yote.TVV 198.3

  Lakini sasa Kristo alitamani mahali pa kupumzika; maana alikuwa na mambo mengi yaliyowahusu wanafunzi wake wenyewe. Katika kazi yao mara nyingi wametatanika, hawakujua jinsi ya kusema. Sasa walitaka kwenda mahali pa upweke, ambapo Yesu angawaelimisha zaidi kuhusu kazi yao ya baadaye. Walikuwa wamejitumbukiza katika kazi kamili, hivyo nguvu zao za kimwili na za kiroho zimelegea. Iliwapasa wapumzike.TVV 198.4

  Kwa kuwa wanafunzi walifanikiwa kazini, kulikuwa na hatari ya kujisifu na kujichukulia utukufu, na kuangukia katika shimo la Shetani. Iliwapasa wajifunze kuwa uwezo wa kufaulu hautokani na wao wenyewe. Iliwapasa kuongea na Kristo, kuchunguza viumbe vya asili na kujichunguza wao wenyewe.TVV 198.5

  Wakati huo ndipo Yesu alipata habari za kifo cha Yohana Mbatizaji. Jambo hili lilimthibitishia mwisho wake pia, kwa kadiri alivyokuwa akienenda na mafundisho yake. Makuhani na Marabi walikuwa nyumba yake, kwa kuweka majasusi ili wapate kumnasa na kumshitaki.TVV 198.6

  Habari za kazi ya Yesu zilimfikia Herode . Basi Herode alisema: “Huyu ni Yohana Mbatizaji, amefufuka katika wafu.” Naye alieleza kuwa na hamu ya kumwona Yesu. Herode alikuwa na hofu ya daima kwa ajili ya mapinduzi yanayoweza kutokea ya Wayahudi kuasi serikali ya Warumi. Roho ya chuki na uasi ilienea pote kwa wayahudi. Ilikuwa wazi kwamba kazi ya Kristo huko Galilaya isingedumu muda mrefu, naye alitamani kuwa mbali na makutano ya watu kwa muda kidogo.TVV 199.1

  Kwa huzuni wanafunzi wa Yohana walikuwa wameuchukua mwili wa Yohana mpaka mahali pa makaburi. Kisha walikwenda na kumwarifu Yesu. Wanafunzi hawa walikuwa na wivu na Yesu, hata walikuwa na mashaka ya Uungu wake, maana hakumwokoa Yohana. Lakini sasa walitaka faraja katika huzuni yao, na maongozi kuhusu kazi yao ya siku zajazo. Walikuja na kuunganika na Yesu.TVV 199.2

  Huko nga’mbo ya ziwa, upande wa kasikazini kulikuwa na semu ya nafasi, isiyokuwa na watu. Ilikuwa sehemu nzuri yenye maji mengi na majani. Waliingia katika mashua kuiendea. Ilikuwa sehemu ya kupendeza. Mahali hapo wangemsikiliza Yesu bila fujo. na ghasia za Waandishi na Mafarisayo.TVV 199.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents