Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kosa la Hatari

    Kosa la mauti ambalo lilileta msiba wa namna hiyo kwa Ufransa lilikuwa kuitokujali kwa ukweli huu mmoja mkubwa; uhuru wa kweli unaokuwa katikati ya makatazo ya sheria ya Mungu. “Laiti ungalisikiliza maagizo yangu! Ndipo salama yako ingalikuwa kama mto, na haki yako kama mawimbi ya bahari.” Isaya 48:18. Wale ambao hawatasoma fundisho kutoka kwa Kitabu cha Mungu wanaalikwa kulisoma katika historia.TSHM 134.1

    Wakati Shetani alitenda kwa njia ya kanisa la Roma kuongoza watu kuacha utii, kazi yake ikageuka.. Kwa kazi ya Roho wa Mungu makusudi yake yakazuiwa kufikia matumizi yao kamili. Watu hawakutafuta matokeo kwa mwanzo wake na kuvumbua asili ya taabu zao. Lakini katika mapinduzi sheria ya Mungu iliwekwa kando kwa wazi na Baraza la Taifa. Na katika Utawala wa Hofu Kuu uliofuata, kazi na matokeo yaliweza kuonekana kwa wote.TSHM 134.2

    Kuvunja sheria ya haki na nzuri matunda yake inapaswa kuwa maangamizi. Roho wa Mungu wa kiasi, ambaye analazimisha uaguzi juu ya uwezo mkali wa Shetani, uliotoka kwa kiasi kikubwa, na yule ambaye furaha yake ni taabu ya watu aliruhusiwa kufanya mapenzi yake. Wale waliochagua uasi waliachiwa kuvuna matunda yake. Inchi ikajaa na zambi. Kutoka mitaa iliyoteketezwa na miji iliyoangamizwa kilio, cha kutisha kilisikiwa cha maumivu makali. Ufransa ukatikisishwa kama kwa tetemeko. Dini, sheria, kanuni ya watu wote, jamaa, serkali, na kanisa--vyote vikashindwa na mkono mpotovu ambao uliinuliwa kupinga sheria ya Mungu.TSHM 134.3

    Washuhuda waaminifu wa Mungu, waliochinjwa kwa uwezo wa dini ya yule “anayotoka katika shimo pasipo mwisho,” hawakubakia kimya.” Na nyuma ya siku tatu na nusu, roho ya uhai ikatoka kwa Mungu ikaingia ndani yao, wakasimama juu ya miguu yao; woga mkubwa ukaangukia watu wote waliowatazama.” Ufunuo 11:11. Katika mwaka 1793 Baraza la Taifa la Ufransa likaweka amri za kutenga Biblia kando. Miaka mitatu na nusu baadaye, shauri la kutangua amri hizi likakubaliwa na mkutano ule ule. Watu wakatambua lazima ya imani katika Mungu na Neno lake kama msingi wa uwezo na maarifa ya wema na ubaya.TSHM 134.4

    Kwa habari ya “washuhuda wawili” (Maagano ya Kale na Jipya) nabii akatangaza zaidi: “Wakasikia sauti kubwa kutoka mbingu ikisema kwao: Pandeni hata hapa. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama.” Ufunuo 11:12. “Washahidi hawa wawili wa Mungu” wakaheshimiwa zaidi kuliko mbele. Katika mwaka 1804 Chama cha Biblia cha Uingereza na inchi za kigeni kikatengenezwa, kikafuatwa na matengenezo ya namna hii juu ya bara la Ulaya. Katika mwaka 1816 chama cha Biblia cha Waamarica kikaimarishwa. Biblia ikatafsiriwa tangu hapo katika mamia mengi ya lugha na matamko. (Tazama Nyongezo).TSHM 134.5

    Mbele ya mwaka 1792, uangalifu kidogo ukatolewa kwa watu waliopasha kwenda kufundisha na inchi za kigeni. Lakini karibu ya mwisho wa karne ya kumi na mnane mabadiliko kubwa yakafanyika. Watu wakawa hawatoshelewi na kufuata akili za binadamu na wakapatwa na lazima ya ufunuo wa mambo ya kimungu na dini ya hakika. Tokea wakati huu kazi za ujumbe wa kigeni zikapata maendeleo kuliko mbele. (Tazama Nyongezo.)TSHM 135.1

    Maendeleo katika ufundi wa uchapishaji ulisaidia sana kwa maenezi ya Biblia. Kupotea kwa upendeleo usio na haki wa zamani na ubaguzi wa taifa na mwisho wa uwezo wa ulimwengu, askofu wa Roma kukafungua njia kwa mwingilio wa Neno la Mungu. Sasa Biblia ikachukuliwa kwa kila sehemu ya dunia.TSHM 135.2

    Kafiri Voltaire akasema: “Nachoka kusikia kukariri kwamba watu kumi na mbili walianzisha dini ya kikristo.” Nitawaonyesha kwamba mtu mmoja anatosha kwa kuiangamiza” (N.B Missine,sentence). Mamilioni ya watu wakajiunga katika vita juu ya Biblia. Lakini ni mbali kwa kuiangamiza. Mahali palikuwa mia kwa wakati wa Voltaire, sasa panakuwa vitabu ama nakala mamia ya maelfu ya Kitabu cha Mungu. Katika maneno ya Mtengenezaji wa mwanzo, “Biblia ni chuma cha mfinyanzi iliyomaliza nyundo nyingi.” Chochote kitu kilichojengwa juu ya mamlaka ya mtu kitaangushwa; lakini kile ambacho kilijengwa juu ya mwamba wa Neno la Mungu, kitasimama mileleTSHM 135.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents