Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Siku za Hatari kwa Kanisa

    Wachukuzi wa bendera waaminifu walikuwa wachache sana. Hapo hapo ilionekana kwamba makosa ingekuwa karibu kushinda kabisa, na dini ya kweli kuondolewa duniani. Injili ilisahauliwa na watu wakalemewa na azabu kali. Walifundishwa kutumainia kazi zao wenyewe kwa malipo ya zambi zao. Safari ndefu za kwenda kuzuru patakatifu, matendo ya kitubio, ibada ya masalio ya mambo ya watakatifu wa kale, majengo ya makanisa, na mazabahu, malipo ya mali mingi kwa kanisa-haya yalilazimishwa kwa kutuliza hasira ya Mungu ao kujipatia upendeleo wake.TSHM 17.4

    Karibu ya mwisho wa karne ya mnane, wafuasi wa Papa wa Roma wakaendelea kulazimisha kwamba katika siku za kwanza za kanisa maaskofu wa Roma walikuwa na uwezo wa kiroho sawa sawa na ule ambao wanachukuwa sasa. Maandiko ya uwongo yakaandikwa na watawa wakidanganya kwamba ni ya zamani sana. Maagizo ya baraza ambayo hayakusikiwa mbele ya kuimarisha ukubwa wa Papa tangu nyakati za kwanza, yakavumbuliwa (Tazama Nyonge 20).TSHM 17.5

    Waaminifu wachache waliojenga juu ya msingi wa kweli. (1 Wakorinto 3:10,11) wakafazaika. Kuchoka kwa ajili ya kupigana na mateso, udanagnyifu, kila kizuizi kingine ambacho Shetani angevumbua, watu fulani ambao walikuwa waaminifu wakakata tamaa. Kwa ajili ya upendo wa amani na salama kwa mali yao na maisha yao, wakaacha msingi wa kweli. Wengine hawakuongopeshwa na upinzani wa adui zao.TSHM 18.1

    Ibada ya sanamu ikawa kawaida. Mishumaa (bougies) iliwashwa mbele ya masanamu, na maombi yakatolewa kwao. Desturi zisizo za maana na kuabudu uchawi zikawa na uwezo. Hata hakili yenyewe ikaonekana kupoteza nguvu zake. Kwa sababu mapadri na maaskofu wao wenyewe walikuwa wenye kupenda anasa, na rushwa, watu waliotazamia uongozi kwao wakatazamia katika ujinga na makosa.TSHM 18.2

    Katika karne ya kumi na moja, Papa Gregoire VII akatangaza kwamba kanisa halijakosa kamwe, na halitakosa kamwe, kwa kutokana na Maandiko. Lakini hakika za Maandiko hazikufuatana na maneno yale. Askofu mwenye kiburi alidai pia uwezo wa kuondoa wafalme. Mfano moja wa tabia ya uonevu huyu anaotetea madai ya kutoweza kukosa ni jambo alilotendea mfalme wa Ujeremani, Henry IV. Kwa sababu alijaribu kuzarau mamlaka ya Papa, mfalme huyu akatengwa kwa kanisa na akatoshwa kwa kiti chake cha ufalme. Watoto wake wenyewe wa kifalme wakashawishiwa na mamlaka ya Papa katika uasi juu ya baba yake.TSHM 18.3

    Henry akaona lazima ya kufanya amani pamoja na Roma. Pamoja na mke wake na mtumishi wake mwaminifu akavuka milima mirefu (Alpes) katika siku za baridi kali, ili apate kujinyenyekea mbele ya Papa. Alipofikia ngome ya Gregoire, akapelekwa katika uwanja wa inje. Kule, katika baridi kali ya wakati wa majira ya baridi, na kichwa wazi na vikanyagio, alingoja ruhusa ya Papa kuja mbele yake. Ni baada ya siku tatu za kufunga na kuungama, ndipo askofu akamtolea rehema. Na hivyo ni katika hali ya kwamba mfalme alipaswa kungoja ruhusa ya Papa kwa kupata tena alama za cheo ao kutumia uwezo wa kifalme. Gregoire, alipofurahia ushindi wake, akatangaza ya kwamba kazi yake ilikuwa ni kuangusha kiburi cha wafalme.TSHM 18.4

    Ni ajabu ya namna gani tofauti kati ya askofu mwenye kiburi na upole na utulivu wa Kristo anayejionyesha mwenyewe kama mwenye kuomba ruhusa kwa mlango wa moyo. Alifundisha wanafunzi wake: “Naye anayetaka kuwa wa kwanza katikati yenu atakuwa mtumwa wenu” Matayo 20:27.TSHM 18.5

    Hata mbele ya kuanzishwa kwa cheo cha Papa mafundisho ya watu wapagani wenye maarifa wakapata usikizi na kutumia muvuto wao katika kanisa. Wengi waliendelea kujifungia kwa mafundisho ya maarifa zote ya kipagani na wakalazimisha wengine kujifunza elimu ile kama njia ya kueneza mvuto wao katikati ya wapagani. Ndipo makosa makubwa yakaingizwa katika imani ya Kikristo.TSHM 19.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents