Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Alama za Musiba

    Unabii uliyotolewa na Kristo kwa ajili ya uharibifu wa Yerusalema yalitimia wazi wazi. Dalili na maajabu yalitokea. Kwa muda wa miaka saba mtu aliendelea kupanda na kutelemuka katika njia za Yerusalema, kutangaza misiba itakayokuja. Kiumbe hiki cha ajabu kilifungwa gerezani na kuazibiwa, lakini kwa matusi mabaya hayo akajibu tu, “Ole, ole kwa Yerusalema”! Aliuawa katika mitego ya maadui aliyotabiri.TSHM 5.2

    “Hakuna Mkristo hata mmoja aliyeangamia katika uharibifu wa Yerusalema. Baada ya Waroma chini ya uongozi wa Cestius walipozunguka mji, kwa gafula wakaacha mazingiwa wakati kila kitu kilionekana kuwa cha kufaa kwa shambulio. Mkuu wa Roma akaondoa majeshi yake bila sababu ndogo wazi. Alama iliyoahidiwa ilitolewa kwa Wakristo waliokuwa wakingojea. Luka 21:20,21.TSHM 5.3

    Mambo yakafanyika kwa namna ambayo hata Wayahudi ama Waroma hawakupinga kukimbia kwa Wakristo. Katika kushindwa kwa Cestius, Wayahudi wakafuata, na wakati majeshi hayo mawili yalipokutana, Wakristo popote katika inchi waliweza kufanya kimbilio lao bila kusumbuliwa mahali pa salama, kwa mji wa Pella.TSHM 5.4

    Majeshi ya Wayahudi, yalipokuwa yakifuata Cestius na jeshi lake wakaangukia upande wao wa nyuma. Ni kwa shida sana Waroma walifaulu katika kukimbia kwao. Wayahudi pamoja na mateka yao wakarudia na ushindi Yerusalema. Lakini kufaulu kwa namna hii kuliwaletea ubaya tu. Jambo hilo liliwasukuma kwa ile roho ya ukaidi wa kupinga kwa Waroma ambao kwa upesi wakaleta msiba mubaya sana juu ya muji uliohukumiwa.TSHM 5.5

    Hasara zilikuwa za ajabu zile zilianguka juu ya Yerusalema wakati mji ulizungukwa tena na Titus. Mji ulizungukwa wakati wa Pasaka, wakati mamilioni ya Wayahudi walipokusanyika ndani ya kuta zake. Duka za akiba zikaharibiwa kwanza kwa ajili ya kisasi cha makundi ya mabishano. sasa matisho yote ya njaa yakawafikia. Wanaume wakatafuna ngozi ya mikaba yao na viatu na kifuniko cha ngao zao. Hesabu kubwa ya watu wakaenda kwa uficho usiku inje kwa kukusanya mimea fulani ya pori yaliyokuwa yakiota inje ya kuta za mji, ingawa wengi walikuwa wakizunguukwa na kuuawa na mateso makali, na mara kwa mara wale waliokuwa wakirudia katika usalama ndani ya mji walinyanganywa akiba walizopata kwa shida sana. Waume wakaiba wake wao, na wake waume wao. Watoto wakanyanganya chakula kinywani mwa wazazi wazee wao.TSHM 6.1

    Waongozi wa Roma kuogopesha sana Wayuda iliwakubali wameshindwa. Wafungwa waliazibiwa, kuteswa, na kusulubiwa mbele ya ukuta wa mji. Kwa bonde la Yosafati na Kalvari, misalaba ikasimamishwa kwa wingi sana. Ilikuwa vigumu kupitia katikati ya misalaba hiyo. Ndivyo lilivyo timilika agizo la kutisha lililotajwa na Wayahudi mbele ya kiti cha hukumu cha Pilato: “Damu yake iwe juu yetu na juu ya watoto wetu”. Matayo 27:25.TSHM 6.2

    Tito alijazwa na hofu kuu alipoona miili ya wafu kulala kwa malundo katika mabonde. Kama mtu aliye katika maonyo, akatazama hekalu nzuri na akatoa agizo kwamba kusiwe hata jiwe moja lake linalopaswa kuguswa.. Akatoa mwito wa nguvu kwa waongozi wa Wayahudi wasimulazimishe kuchafua mahali patakatifu kwa damu. Kama wakiweza kupigania mahali po pote pengine, hapana Muroma atapashwa kutendea jeuri utakatifu wa hekalu! Yosefu mwenyewe, aliwasihi, akawaomba kujitoa, kwa kujiokoa wenyewe, mji wao na mahali pao pa ibada. Lakini maneno yake yakajibiwa kwa laana chungu. Mishale ya makelele ikatupwa kwake, mwombezi wao wa mwisho wa kibinadamu. Juhudi za Tito ili kuokoa hekalu zilikuwa bure. Mmoja aliyekuwa mkuu kuliko yeye alitangaza kwamba halitabaki jiwe juu ya jiwe pasipo kubomolewa.TSHM 6.3

    Mwishowe Tito akaamua kukamata hekalu kwa gafula, akakusudia kwamba ikiwezekana ilipaswa kuokolewa kwa maangamizi. Lakini maagizo yake hayakujaliwa. Kinga cha moto kikatupwa upesi na askari mmoja kwa tundu ndani ya ukumbi, na mara moja vyumba vilivyokuwa na miti ya mierezi kuzunguuka hekalu takatifu vikawaka moto. Tito akaenda kwa haraka mahali pale, na akaagiza waaskari kuzima ndimi za moto. Maneno yake hayakufuatwa. Katika hasira yao waaskari wakatupa vinga vya moto ndani ya vyumba vya karibu na hekalu, na tena pamoja na panga zao wakaua hesabu kubwa ya wale waliokimbilia ndani ya Pahali patakatifu. Damu ikatiririka kama maji juu ya vipandio vya hekalu.TSHM 6.4

    Baada ya kuangamizwa kwa hekalu, mara mji wote ukawa mikononi mwa Waroma. Waongozi wa Wayahudi wakaacha minara yao isiyoshindika. Alipokwisha kuitazama na mshangao, akasema kwamba ni Mungu mwenyewe aliyeitoa mikononi mwake; kwani hakuna mashini za vita, hata zenye nguvu, zingeweza kushinda minara kubwa sana. Mji pamoja na hekalu vilibomolewa tangu msingi, na mahali ambapo nyumba takatifu ilikuwa imesimama “palilimwa kama shamba linavyolimwa” Yeremia 26:18. Zaidi ya milioni wakaangamia; waliookoka wakapelekwa kama mateka, wakauzishwa kama watumwa, wakakokotwa chini hata Roma, wakatupwa kwa wanyama wa pori ndani ya viwanda vya michezo, ao kutawanywa mahali pote kama watembezi wasio na makao.TSHM 7.1

    Wayahudi walijaza wao wenyewe kikombe cha kisasi. Kuangamizwa kwa taifa lao na mabaya yote yaliyofuata kutawanyika kwao, ilikuwa ndiyo kuvuna mavuno ambayo mikono yao yenyewe ilipanda “O, Israel, umejiharibu wewe mwenyewe “kwa maana umeanguka sababu ya uovu wako”. Hosea 13:9; 14:1. Mateso yao yanaonyeshwa mara kwa mara kama azabu iliwafikia ya hukumu ya Mungu. Ni kwa sababu hiyo mdanganyi mkuu hujitahidi kuficha kazi yake mwenyewe. Kwa kukataa sababu ya hukumu kwa upendo wa Mungu na rehema, Wayahudi walilazimisha ulinzi wa Mungu kuondolewa kwao.TSHM 7.2

    Hatuwezi kujua namna gani tunapashwa kushukuru Kristo kwa ajili ya amani na ulinzi tunaofurahia. Ni nguvu ya Mungu inayozuia wanadamu kuanguka kabisa katika mikono ya Shetani. Waasi na wasio na shukrani wanakuwa na sababu kubwa ya kushukuru Mungu kwa ajili ya rehema yake. Lakini wakati watu wanapo pitisha mipaka ya uvumilivu wa Mungu, ulinzi huondolewa. Mungu hasimame kama mwuaji wa mhukumu juu ya kosa. Huacha wanaokataa rehema zake kuvuna walichopanda. Kila mushale wa nuru uliokataliwa ni mbegu iliyopandwa inayozaa lazima mavuno yake. Roho ya Mungu, ikipingwa kwa bidii, mwishowe itaondolewa. Kwa hiyo, hakuna tena nguvu ya kuzuia tamaa mbaya za roho, hakuna ulinzi kwa uovu na uadui wa Shetani.TSHM 7.3

    Uharibifu wa Yerusalema ni onyo la kutisha kwa wote wanaopinga maombezi ya rehema za Mungu. Unabii wa Mwokozi juu ya hukumu ya Yerusalema inakuwa na utimilizo mwengine. Katika hukumu ya mji muchaguliwa tunaona maangamizo ya ulimwengu ambao ulikataa rehema za Mungu na kukanyaga sheria yake. Habari ya shida ya mwanadamu ambayo dunia imeshuhudia ni ya giza. Matokeo ya kukataa mamlaka ya Mungu ni ya kuogopesha. Lakini mambo ya giza zaidi yanaonyeshwa katika ufunuo ya wakati ujao. Wakati ulinzi wa Roho ya Mungu utaondolewa kabisa, haitawezekana tena kuzuia kuripuka kwa tamaa ya kibinadamu na hasira ya uovu, ulimwengu utashika, kwa namna isivyofanyika mbele, matokeo ya mamlaka ya Shetani.TSHM 8.1

    Katika siku ile, kama katika uharibifu wa Yerusalema, watu wa Mungu watakombolewa. Tazama lsaya 4:3; Matayo 24:30,31. Kristo atakuja mara ya pili kukusanya waaminifu wake kwake mwenyewe. “Halafu kabila zote; na mataifa yote ya dunia yataomboleza, nao watamuona Mwana wa watu akija katika mawingu ya mbingu pamoja na uwezo na utukufu mkubwa. Naye atatuma malaika zake na sauti kubwa ya baragumu, nao watakusanya wachaguliwa wake toka pepo ine, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho ule”. Matayo 24:30,31.TSHM 8.2

    Watu wajihazari ili wasizarau maneno ya Kristo. Kama alivyoonya wanafunzi wake juu ya uharibifu wa Yerusalema ili wapate kukimbia, vile vile ameonya watu juu ya siku ya uharibifu wa mwisho. Wote watakao wapate kukimbia hasira ijao. “Na kutakuwa alama katika jua na mwezi, na nyota; na katika dunia taabu ya mataifa”. Luka 21:25. Tazama vile vile Matayo 24:29; Marko 13:24-26; Ufunuo 6:12-17. “Basi angalieni”, ndiyo maneno ya Kristo ya onyo la upole. Marko 13:35. Wale wanaokubali onyo hili hawataachwa gizani.TSHM 8.3

    Ulimwengu hauko tayari zaidi kusadiki (amini) ujumbe kwa wakati huu kuliko walivyokuwa Wayahudi kwa kupokea onyo la Mwokozi juu ya Yerusalema. Njoo ingalipo wakati, siku ya Mungu itakuja gafula kwa waovu. Wakati maisha inapoendelea katika mviringo wake wa siku zote; wakati watu wanaposhugulika katika anasa, katika kazi, katika kukusanya pesa; wakati waongozi wa dini wanapotukuza maendeleo ya dunia, na watu wanapotulizwa katika salama ya uwongo-ndipo, kama mwizi wa usiku wa manane huiba kwa gafula, ndivyo uharibifu utakuja kwa gafula juu ya wazarau na waovu, “wala hawatakimbia”. Tazama 1 Watesalonika 5:2-5.TSHM 8.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents