Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mwito Wa Shetani Kwa Wenye Akili

  Kwa watu wenye elimu naustaarabu mfalme wa giza anaonyesha imani ya kuwa na roho za watu waliokufa na kujionyesha na kuongea na watu (spiritisme) katika mifano yake safi zaidi na ya akili. Anapendezwa sana na wazo la tendoo la kushangaza kwa furaha na maelezo yenye uwezo wa kushawishi ya mapendo na wema. Anaongoza watu kutumia kiburi sana katika hekima yao wenyewe ili ndani ya mioyo yao waaibishe Bwana wa Milele.TSHM 270.3

  Shetani anadanganya watu sasa kama alivyodanganya Hawa katika Edeni kwa njia ya kuamsha tamaa ya nguvu kwa ajili ya kujiinua.TSHM 270.4

  “Mutakuwa kama miungu,” anatangaza, “mukijua uzuri na ubaya”. Mwanzo 3:5. Imani ya kuwako kwa roho za watu waliokufa inafundisha” kwamba mtu ni kiumbe cha maendeleo... karibu ya kichwa cha uungu”. Tena; “Hukumu itakuwa ya haki, kwa sababu ni hukumu ya kila mtu binafsi.... Kiti cha enzi ni ndani yako”. Na mwingine anasema: “Kila kiumbe cha haki na kikamilifu ni Kristo”.TSHM 270.5

  Kwa hivyo Shetani aligeuza tabia ya zambi ya mtu mwenyewe kuwa amri ya pekee ya hukumu. Hii ni maendeleo, si kwenda juu, bali kwenda chini. Mtu hawezi kuinuka juu kuliko cheo chake cha usafi wala wema. Kama nafsi ndiyo kipeo chake kikamilifu cha juu kuliko, hatafikia kamwe kwa kitu cho chote kinachoinuka zaidi. Neema ya Mungu tu inakuwa na uwezo kwa kuinua mtu. Kuachwa upekee, maendeleo yake inapaswa kwenda chini.TSHM 270.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents