Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Makundi Mawili ndani ya Kanisa

  Kulikuwa makundi mawili miongoni mwa wale waliojidai kuwa wafuasi wa Kristo. Wakati kundi moja lilijifunza maisha ya Mwokozi na kwa uangalifu wakatafuta kuhakikisha makosa yao na kufuata Mfano, kundi lingine likaepuka mambo ya kweli wazi wazi yaliyofunua makosa yao. Hata katika hali yake bora, washiriki wa kanisa wote hawakuwa wa kweli, safi, na amini. Yuda aliunganishwa na wanafunzi, ili kwa njia ya mafundisho na mifano ya Yesu angeweza kugeuka kwa kuona makosa yake. Lakini kwa upendeleo katika zambi akaalika majaribu ya Shetani. Akakasirika wakati makosa yake yalihakikishwa na ndipo akaongozwa kusaliti Bwana wake. Tazama Marko 14:10,11.TSHM 11.1

  Anania na Safira wakajidai kutoa kafara kamili kwa Mungu wakati walizuia kwa tamaa sehemu kwa ajili yao wenyewe. Roho wa ukweli akafunua kwa mitume tabia ya kweli ya wajanja hawa, na hukumu za Mungu zikaokoa kanisa kwa laumu mbaya kwa usafi wake. Tazama Matendo 5:1-11. Mateso yalipokuja juu ya wafuasi wa Kristo, wale tu waliotaka kuacha vyote kwa ajili ya ukweli walitamani kuwa wanafunzi wake. Lakini kwa vile mateso yalipokoma, waongofu waliongezeka wasiokuwa wa kweli, na njia ikafunguliwa kwa ajili ya Shetani kupata pa kuwekea mguu.TSHM 11.2

  Wakati Wakristo walipokubali kujiunga pamoja na wale waliogeuka kwa nusu tu kutoka katika ushenzi, Shetani akashangilia. Ndipo akawatia moyo kutesa wale waliodumu kuwa waaminifu kwa Mungu. Wakristo hawa wakufuru (waasi), walipoungana na wenzao nusu wapagani wakaelekeza vita yao juu ya mambo ya kanuni (zaidi) ya mafundisho ya Kristo. Ilitakiwa shindano kali sana kusimama imara juu ya madanganyo na machukizo yaliyoingizwa kanisani. Biblia haikukubaliwa kuwa msingi wa imani. Mafundisho ya uhuru wa dini yakaitwa uwongo, na watetezi wake wakaondolewa.TSHM 11.3

  Baada ya mapigano marefu, waaminifu waliona kwamba mutengano ulikuwa wa lazima kabisa. Hawakusubutu kuvumilia wakati mrefu zaidi makosa yaliyokuwa hatari kwa roho zao, na kufanya mfano mbaya ungaliweza kuhatarisha imani ya watoto wao na watoto wa watoto wao. Waliona kwamba amani ingepatikana kwa bei kali sana kwa kafara ya kanuni. Kama umoja ungalifanyiwa tu kwa kuvunja ukweli, heri tofauti iwepo, na hata vita.TSHM 11.4

  Wakristo wa kwanza walikuwa kweli watu wa kipekee. Wachache katika hesabu, bila utajiri, cheo, wala majina ya heshima, walikuwa wakichukiwa na waovu, hata kama vile Abeli alivyochukiwa na Kaini. Tazama Mwanzo 4:1-10. Tangu siku za Kristo hata sasa, wanafunzi wake waaminifu wameamsha chuki na upinzani wa wale wanaopenda zambi.TSHM 11.5

  Namna gani, basi, injili inaweza kuitwa habari ya amani? Malaika waliimba kwa uwanja wa Betelehemu: “Utukufu kwa Mungu aliye juu, na salama duniani, katika watu wanaomupendeza”. Luka 2:14. Kwa inje hapo kuna kinyume kati ya maneno ya unabii huu na maneno ya Kristo: “Sikuja kuleta salama lakini upanga”. Matayo 10:34. Lakini yanafahamika vizuri, maneno haya mawili yanapatana vizuri kabisa. Injili ni ujumbe wa amani. Dini ya Kristo, ikikubaliwa na kutii, ingeeneza amani na furaha duniani pote. Ilikuwa kazi ya Yesu kupatanisha watu kwa Mungu, na kwa mtu kwa mwenzake. Lakini ulimwengu wote unakuwa katika utawala wa Shetani, adui mkali wa Kristo. Injili huonyesha kanuni za maisha kuwa zinazokuwa kinyume cha tabia na mapenzi yao, nazo zinapinga injili yake. Huchukia usafi unaofunua na kuhukumu zambi zao, na hutesa na kuangamiza wale wanaotangaza haki na utakatifu. Ni kwa maana hii kwamba injili huitwa upanga. Tazama Matayo 10:34.TSHM 12.1

  Wengi wanaokuwa wazaifu katika imani wanakuwa tayari kuacha tumaini lao katika Mungu kwa sababu anakubali watu waovu kusitawi, wakati watu wema na safi wanapoteseka na uwezo wa ukali wao. Swali, namna gani, Mungu mwenye haki na rehema, ambaye uwezo wake hauna mwisho, anaweza kukubali uzalimu na mateso ya namna hiyo? Mungu ametupa ushuhuda wa kutosha wa upendo wake. Hatuwezi kuwa na mashaka juu ya wema wake kwani hatuwezi kufahamu maongozi yake. Mwokozi alisema, “Kumbukeni neno nililowaambia ninyi: Mtumwa si mkubwa kuliko Bwana yake. Kama walinitesa mimi, watawatesa ninyi vile vile”. Yoane 15:20. Wale wanaoitwa kwa kuvumilia mateso na mauti ya wafia dini wanapaswa kutembea kwa nyayo za Mwana mpendwa wa Mungu.TSHM 12.2

  Wenye haki huwekwa katika tanuru ya taabu ili wao wenyewe wapate kutakaswa, ili mfano wao upate kuvuta wengine kwa haki ya imani na wema, na kwamba mwenendo wa uaminifu wao upate kuhukumu waovu na wasioamini. Mungu huruhusu waovu kusitawi na kufunua uadui wao juu yake ili wote wapate kuona haki yake na rehema zake katika uharibifu wao kabisa. Kiia tendo la ukali juu ya waaminifu wa Mungu litaazibiwa kama kwamba lilitendewa Kristo mwenyewe.TSHM 12.3

  Paulo anasema kwamba “wote wanaotaka kuishi maisha ya utawa katika Kristo watapata mateso”. 2 Timoteo 3:12. Sababu gani, basi, kwamba mateso huonekana yamesinzia? Sababu moja tu kwamba kanisa lilijiweka kwa kawaida ya kidunia na kwa hivyo haliamushi tena upinzani. Dini katika siku zetu si safi kama imani takatifu ya Kristo na mitume wake. Kwa sababu mambo ya kweli ya Neno la Mungu yanazaniwa kwa ubaridi, kwa sababu kunakuwa utawa kidogo sana katika kanisa, Ukristo unapendwa na watu wote. Acha imani ya kanisa la kwanza ifufuke, na mioto ya mateso itawashwa tena.TSHM 12.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents