Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Luther Alikimbilia Tu kwa Biblia

  Wakati adui walikimbilia kwa desturi na desturi ya asili, Luther alikutana nao anapokuwa na Biblia tu, bishano ambayo hawakuweza kujibu. kutoka mahubiri ya Luther na maandiko kulitoka nyali za nuru ambazo ziliamsha na kuangazia maelfu. Neno la Mungu lilikuwa kama upanga unaokata ngambo mbili, unaokata njiayake kwa mioyo ya watu. Macho ya watu, kwa mda mrefu yaliongozwa kwa kawaida za kibinadamu na waombezi wa kidunia, sasa walimugeukia Kristo katika imani na Yeye aliyesulubishwa.TSHM 58.3

  Usikizi huu ukaamsha woga kwa mamlaka ya Papa. Luther akapokea mwito kuonekana huko Roma. Rafiki zake walijua vizuri hatari ile iliyomngoja katika mji mwovu huo, uliokwisha kunywa damu ya wafia dini wa Yesu. Wakauliza kwamba apokee mashindano yake katika Ujeremani.TSHM 58.4

  Jambo hili likatendeka, na mjumbe wa Papa akachaguliwa kusikiliza mambo yenyewe. Katika maagizo kwa mkubwa huyu, alijulishwa kwamba Luther alikwisha kutangazwa kama mpingaji wa imani ya dini. Mjumbe alikuwa basi ni “kutenda na kulazimisha bila kukawia.” Mjumbe akapewa uwezo wa “kumufukuza katika kila upande wa Ujeremani; kumfukuzia mbali, kumlaani, na kutenga wale wote walioambatana naye”, Kuwatenga na cheo cho chote kikiwa cha kanisa ao cha serkali, ila tu mfalme, hatajali kumkamata Luther na wafuasi wake na kuwatoa kwa kisasi cha Roma.TSHM 58.5

  Hakuna alama ya kanuni ya kikristo ao hata haki ya kawaida inapaswa kuonekana katika maandiko haya. Luther hakuwa na nafasi ya kueleza wala kutetea musimamo wake; lakini alikuwa amekwisha kutangazwa kuwa mpingaji wa imani ya dini na kwa siku ile ile alishauriwa, kushitakiwa, kuhukumiwa, na kulaumiwa.TSHM 59.1

  Wakati Luther alihitaji sana shauri la rafiki wa kweli, Mungu akamtuma Melanchthon kule Wittenberg. Shida ya hukumu ya Melanchthon, ikachanganyika na usafi (utakatifu) na unyofu wa tabia, ikashinda sifa ya watu wote. Kwa upesi akawa rafiki mwaminifu sana wa Luther--upole wake, uangalifu, na usahihi ikawazidisho la bidii na nguvu za Luther.TSHM 59.2

  Augsburg palitajwa kuwa mahali pa hukumu, na Mtengenezaji (Reformateur) akaenda huko kwa miguu. Vitisho vilifanywa kwamba angeuawa njiani, na rafiki zake wakamuomba asijihatarishe. Lakini maneno yake yalikuwa, “Ninakuwa kama Yeremia, mtu wa ushindano, na ugomvi; lakini kwa namna matisho yao yalizidi, ndipo furaha yangu iliongezeka... Wamekwisha kuharibu heshima (sifa) yangu na mwenendo wangu. ... Kuhusu roho yangu, hawawezi kuikamata. Yeye anayetaka kutangaza neno la Kristo ulimwenguni, inampasa kutazamia kifo wakati wowote.”TSHM 59.3

  Akari ya kufika kwa Luther huko Augsburg kukaleta kushelewa kukubwa kwa mjumbe wa Papa. Mpinga mafundisho ya dini anayeamsha ulimwengu akaonekana sasa kuwa chini ya uwezo wa Roma; hakupaswa kuponyoka. Mjumbe alikusudia kulazimisha Luther kukana, ao isipowezekana alazimishe kwenda Roma kufuata nyayo ya Huss na Jerome. Mjumbe wa Papa akatuma watu wake kumwambia Lutter afike bila ahadi ya ulinzi salama wa mfalme na matumaini yake mwenyewe wema wake. Kwa hiyo mtengenezaji akakataa. Hata wakati alipopata ahadi ya ulinzi wa mfalme mkuu ndipo akakubali kuonekana mbele ya mjumbe wa Papa. Kama mpango wa busara, watu wa Roma wakakusudia kumpata Luther kwa njia ya kujioyesha kama wapole. Mjumbe akajionyesha kawa rafiki mkubwaa, lakini akaomba kwamba Luther ajitoe kabisa kwa kanisa na kukubali kila kitu bila mabishano wala swali. Luther, kwa kujibu, akaonyesha heshima yake kwa ajili ya kanisa, mapenzi yake kwa ajili ya ukweli, kuwa tayari kwa kujibu makatazo yote kuhusu yale aliyoyafundishwa, na kuweka mafundisho yake chini ya uamuzi wa vyuo vikubwa (universites). Lakini alikataa juu ya mwendo wa askofu katika kummulazimisha kukana bila kuonyesha na kuhakikisha kosa lake.TSHM 59.4

  Jibu moja tu lilikuwa, “uKane, ukane”! Mtengenezaji akaonyesha kwamba msiimamo wake unakubaliwa na Maandiko. Hakuweza kukana ukweli. Mjumbe, aliposhindwa kujibu kwa mabishano ya Luther, akamulemeza na zoruba ya laumu, zarau, sifa ya uongo maneno kutoka kwa kiasili (traditions), na mezali (maneno) ya Wababa, akikatalia Mtengenezaji nafasi ya kusema. Luther mwishowe, bila kupenda, akamupa ruhusa ya kutoa jibu lake kwa maandiko.TSHM 60.1

  Akasema,akiandika kwa rafiki, “Mambo yaliyoandikwa ingeweza kutolewa kwa mawazo ya wengine; na jambo la pili, mtu anakuwa na bahati nzuri sana ya kutumika kwa hofu nyingi, kama si kwa zamiri, ya bwana wa kiburi na wa kusema ovyo ovyo ambaye njia ingine angeshinda kwa kutumia maneno yake makali.”TSHM 60.2

  Kwa mkutano uliofuata, Luther akaonyesha maelezo mafupi na ya nguvu ya mawazo yake, yanayoshuhudiwa na Maandiko. Kartasi hii, baada ya kusoma kwa sauti nguvu, akaitoa kwa askofu, naye akaitupa kando kwa zarau, kuitangaza kuwa mchanganyiko wa maneno ya bure na mateuzi yasiyofaa. Sasa Luther akakutana na askofu wa kiburi kwa uwanja wake mwenyewe--mambo ya asili na mafundisho ya kanisa--na kuangusha kabisa majivuno yake.TSHM 60.3

  Askofu akapoteza kujitawala kote na katika hasira akapandisha sauti, “ukane! ao nitakutuma Roma”. Na mwishowe akatangaza, katika sauti ya kiburi na hasira, “uKane, ao usirudi tena.”TSHM 60.4

  Mtengenezaji kwa upesi akaondoka pamoja na rafiki zake, hivyo kutangaza wazi kwamba asingoje kwake kwamba atakana. Hili si jambo ambalo askofu alilokusudia. Kutoka kwa Luther Sasa, akaachwa peke yake pamoja na wasaidizi wake, wakatazamana wao kwa wao na huzuni kwa kushindwa kusikotazamiwa katika mipango yake.TSHM 60.5

  Makutano makubwa yaliyokuwa pale wakawa na nafasi ya kulinganisha watu wawili hawa na kuhukumu wao wenyewe roho iliyoonyeshwa nao, vivyo hivyo na nguvu na ukweli wa nia zao. Mtengenezaji, munyenyekevu, mpole, imara, kwa kuwa na ukweli kwa upande wake; mjumbe wa Papa, mwenye kujisifu, mwenye kiburi, mpumbavu, bila hata neno moja kutoka kwa Maandiko, lakini wa juhudi ya kupandisha sauti, “uKana, ao utumwe Roma.”TSHM 60.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents