Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  9 / NURU ILIWASHWA KATIKA USUISI

  Juma chache baada ya kuzaliwa kwa Luther katika kibanda cha mchimba madini katika Saxe, Ulric Zwingli akazaliwa katika nyumba ndogo ya wachungaji katika milima mirefu ya Alpes. Alipokelewa pahali penye maubule makubwa, akili yake mwanzoni tu ikavutwa na utukufu wa Mungu. Kando ya babu wake mwanamke, alisikiliza hadizi chache za damani za Biblia alizokusanya kwa shida kutoka kwa hadizi na mafundisho ya kanisa yaliyotokea zamani.TSHM 79.1

  Kwa umri wa miaka kumi na mitatu akaenda Berne, mahali palipokuwa shule lililokuwa la sifa sana katika Usuisi. Hapa, lakini, kukatokea hatari. Juhudi nyingi zikafanywa na watawa kwa kumvuta katika nyumba ya watawa. Kwa bahati baba yake akapata habari ya makusudi ya watawa. Aliona kwamba mafaa ya wakati ujao ya mwanawe yalikuwa ya kufa kwa ajili ya imani ya dini na akamwongoza kurudi nyumbani.TSHM 79.2

  Agizo likasikiwa, lakini kijana hakuweza kurizika katika bonde lake la kuzaliwa, akaenda kufuata masomo yake huko Ba le. Ni hapo ambapo Zwingli alisikia mara ya kwanza injili ya neema ya Mungu isionunuliwa. Huko Wittembach, alipokuwa akijifunza (kiyunani) Kigiriki na Kiebrania, akaongozwa kwa Maandiko matakatifu, kwa hivyo nyali za nuru ya Mungu ikatolewa katika akili za wanafunzi aliokuwa akifundisha. Akatangaza kwamba kifo cha Kristo ni ukombozi wa kipekee wa mwenye zambi. Kwa Zwingli maneno haya ni nyali ya kwanza ya nuru unayotangulia mapambazuko.TSHM 79.3

  Zwingli akaitwa upesi kutoka Bale kwa kuingia kwa kazi yake ya maisha. Kazi yake ya kwanza ilikuwa katika vilaya ya milima mirefu. Akatakaswa kama padri, “akajitoa wakfu na roho yake yote kwa kutafuta kweli ya Mungu.”TSHM 79.4

  Namna alizidi kutafuta Maandiko, zaidi tofauti ikaonekana kwake kati ya ukweli na mambo ya kupinga imani ya dini ya Roma. Akajitoa mwenyewe kwa Biblia kama Neno la Mungu, amri moja tu inayofaa na ya haki. Aliona kwamba Biblia inapaswa kuwa mfariji wake mwenyewe. Akatafuta usaada wowote kwa kupata ufahamu kamili wa maana yake, na akaomba usaada wa Roho Mtakatifu. “Nikaanza kumuomba Mungu kwa ajili ya nuru yake, “baadaye akaandika, “na Maandiko yakaanza kuwa rahisi zaidi kwangu.”TSHM 79.5

  Mafundisho yaliyohubiriwa na Zwingli hayakupokewa kutoka kwa Luther. Yalikuwa mafundisho ya Kristo. “ikiwa Luther anahubiri Kristo,” akasema Mtengenezaji wa Usuisi, “anafanya ninavyofanya. ... Hakuna hata neno moja lililoandikwa nami kwa Luther wala lililoandikwa na Luther kwangu. Ni kwa sababu gani? ... Ili ipate kuonyeshwa namna gani Roho wa Mungu anakuwa katika sauti moja kwake mwenyewe, hivi sisi wawili, bila mgongano, tunafundisha mafundisho ya Kristo kwa ulinganifu kama huo.”TSHM 79.6

  Katika mwaka 1516 Zwingli akaalikwa kuhubiri katika nyumba ya watawa huko Einsiedeln. Hapa alipashwa kutumia kama Mtengenezaji mvuto ambao ungesikiwa mbali hata kuvuka milima mirefu (Alpes) alipozaliwa.TSHM 80.1

  Katika vitu vya mvuto wa Einseideln ni sanamu ya Bikira, walisema kwamba ilikuwa na uwezo wakufanya. Juu ya mlango wa nyumba ya watawa kulikuwa na maandiko, “Ni hapa kunapatikana msamaha wa zambi zote.” Makundi mengi wakaja kwa mazabahu ya Bikira kutoka pande zote za Usuisi, na hata kutoka Ufaransa na Ujeremani. Zwingli akapata nafasi ya kutangaza uhuru kwa njia ya injili kwa watumwa hawa wa mambo ya ibada ya sanamu.TSHM 80.2

  “Musizani,” akasema, “kwamba Mungu yuko katika hekalu hii zaidi kuliko kwa upande mwingine wauumbaji. ... Je, kazi zisizofaa, safari za taabu, sadaka, masanamu, sala za Bikira ao za watakatifu zingeweza kuwapatia neema ya Mungu? ... Ni manufaa gani ya kofia ya kungaa, kichwa kilichonolewa vizuri, kanzu ndefu na yenye kuvutwa, ao viato vyenye mapambo ya zahabu?” “Kristo,” akasema, “aliyetolewa mara moja juu ya msalaba, ni toko na kafara, alifanya kipatanisho kwa ajili ya zambi za waaminifu hata milele.”TSHM 80.3

  Kwa wengi lilikuwa uchungu wa kukatisha tamaa kuambiwa kwamba safari yao ya kuchokesha ilikuwa ya bure. Hawakuweza kufahamu rehema waliyotolewa bure katika Yesu Kristo. Njia ya mbinguni iliyowekwa na Roma iliwatoshelea. Ilikuwa ni rahisi sana kutumaini wokovu wao kwa wapadri na Papa kuliko kutafuta usafi wa moyo.TSHM 80.4

  Lakini kundi lingine wakapokea kwa furaha habari za ukombozi kwa njia ya Kristo, na katika imani wakakubali damu ya Muokozi kuwa kipatanisho chao. Hawa wakarudi kwao kuonyesha wengine nuru ya damani waliyoipokea. Kwa hivi ukweli ukapelekwa mji kwa mji, na hesabu ya wasafiri kwa mahali patakatifu pa Bikira ikapunguka sana. Sadaka sasa zikapunguka, na kwa sababu hiyo mshahara wa Zwingli uliyokuwa ukitoka humo. Lakini jambo hilo lilimletea tu furaha namna alivyoona kwamba uwezo wa ibada ya sanamu ulikuwa ukivunjwa. Ukweli ukapata uwezo kwa mioyo ya watu.TSHM 80.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents