Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mwisho wa Wote Umekatwa

    Rehema imeisha kwa wakati mfupi kabla ya kuonekana kwa Bwana katika mawingu ya mbinguni. Kristo akitazama wakati ule, anasema: “Yeye aliye mzalimu azidi kuwa mzalimu; na mwenye uchafu azidi kuwa mchafu; na mwenye haki azidi kufanya haki; na mtakatifu azidi kutakaswa. Tazama, ninakuja upesi na mshahara wangu ni pamoja nami, kulipa kila mtu kama ilivyo kazi yake.” Ufunuo 22:11,12.TSHM 238.2

    Watu watakuwa wakipanda na kujenga, kula na kunywa, wote pasipokufahamu ya kuwa hukumu ya mwisho imetangazwa katika Pahali patakatifu mbinguni. Mbele ya Garika, baada ya Noa kuingia katika safina, Mungu akamfungia ndani na kufungia waovu inje; lakini kwa siku saba watu wakaendelea na maisha yao ya kupenda anasa na wakachekelea maonyo ya hukumu. “Ndivyo” asema Mwokozi, “kutakavyokuwa kuja kwa Mwana wa watu.” Kwa kimya, bila kuonwa kama mwizi usiku wa manane, saa itakuja ambayo inaonyesha kukata shauri la mwisho wa kila mtu. “Basi angalieni: ... asije na kuwasitusha ninyi gafula, akawakuta mumelala.” Matayo 24:39; Marko 13:35,36.TSHM 238.3

    Hali ni yenye hatari ya wale ambao, huendelea kuchoka kwa kukesha kwao, wanageuka kwa mivuto ya dunia. Wakati mtu wa biashara anaposhughulika katika kufuata faida, wakati mwenye kupenda anasa anapotafuta anasa, wakati binti wa desturi ya kuvaa nguo anapotengeneza mapambo yake--inaweza kuwa katika saa ile Mwamzi wa dunia yote atatangaza hukumu, “Umepimwa katika mizani, nawe umeonekana kuwa umepunguka.” Danieli 5:27.TSHM 238.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents