Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Shida ya Kutisha

  Hiyo ilikuwa shida ya kutisha sana kwa Matengenezo. Luther hakuwa kipofu kwa zoruba karibu kupasuka, lakini alitumaini Kristo kuwa egemeo lake na ngabo yake. “Kitu kinacho karibia kutokea sikijui, na sijali kujua. ... Hakuna hata sivile jani linawezakuanguka, bila mapenzi ya Baba yetu. Kiasi gani zaidi atatuchunga! Ni vyepesi kufa kwa ajili ya Neno, kwani Neno ambalo lilifanyika mwili lilikufa lenyewe.” Wakati barua ya Papa ilimufikia Luther, akasema: Ninaizarau, tena naishambulia, kwamba niya uovu, ya uongo.... Ni Kristo yeye mwenyewe anayelaumiwa ndani yake. Tayari ninasikia uhuru kubwa moyoni mwangu; kwani mwishowe ninajua ya kwamba Papa ni mpinga kristo na kiti chake cha ufalme ni kile cha Shetani mwenyewe.”TSHM 62.5

  Lakini mjumbe wa Roma halikukosa kuwa na matokeo. Wazaifu na waabuduo ibada ya sanamu wakatetemeka mbele ya amri ya Papa, na wengi wakaona kwamba maisha yalikuwa ya damani sana kuhatarisha. Je, kazi ya Mtengenezaji ilikuwa karibu kwisha?TSHM 62.6

  Luther angali bila woga. Kwa uwezo wa kutisha akarudisha juu ya Roma yenyewe maneno ya hukumu. Mbele ya makutano ya wanainchi wa vyeo vyote Luther akachoma barua ya Papa. Akasema, “Mapigano makali yameanza sasa. Hata sasa nilikuwa nikicheza tu na Papa. Nilianza kazi hii kwa jina la Mungu; si mimi atakaye imaliza, na kwa uwezo wangu.... Nani anayejua kama Mungu hakunichagua na kuniita na kama hawapashwe kuogopa hiyo, kwa kunizarau, wanazarau Mungu Mwenyewe? ...TSHM 63.1

  “Mungu hakuchagua kamwe kuhani aokuhani mkuu wala mtu mkubwa yeyote; bali kwa kawaida huchagua watu wa chini na wenye kuzarauliwa, hata mchungaji kama Amosi. Kwa kila kizazi, watakatifu walipaswa kukemea wakuu, wafalme, wana wa wafalme, wakuhani, na wenye hekima, kwa hatari ya maisha yao. ... Sisemi kwamba niko nabii; lakini nasema kwamba wanapashwa kuogopa kabisa kwa sababu niko peke yangu na wao ni wengi. Ninakuwa hakika ya jambo hili, kwamba neno la Mungu linakuwa pamoja nami, na kwamba haliko pamoja nao.”TSHM 63.2

  Kwani haikuwa bila vita ya kutisha kwamba yeye mwenyewe ambaye Luther aliamua juu ya kutengana kwa mwisho na kanisa: “Ee, uchungu wa namna gani iliniletea, ijapo nilikuwa na Maandiko kwa upande wangu, kuhakikisha mimi mwenyewe kwamba ningepaswa kusubutu kusimama pekee yangu kumpinga Papa, na kumutangaza kuwa kama mpinzani wa Kristo! Mara ngapi sikujiuliza mwenyewe kwa uchungu swali lile ambalo lilikuwa mara nyingi midomoni mwa watu wa Papa: ‘Ni wewe peke yako mwenye hekima? Je, watu wote wanadanganyika? Itakuwa namna gani, kama, mwishoni wewe mwenyewe ukionekana kuwa na kosa na ni wewe anayeshawishi katika makosa yako roho nyingi kama hizo. Ni nani basi atakayehukumiwa milele? Hivi ndivyo nilipigana na nafsi yangu na Shetani hata Kristo, kwa neno lake la hakika, akaimarisha moyo wangu juu ya mashaka haya.”TSHM 63.3

  Amri mpya ikaonekana, kutangaza mtengano wa mwisho wa Mtengenezaji kutoka kwa kanisa la Roma, kumshitaki kama aliyelaaniwa na Mbingu, na kuweka ndani ya hukumu ilete wale watakaopokea mafundisho yake.TSHM 63.4

  Upinzani ni sehemu ya wote wale ambao Mungu hutumia kwa kuonyesha ukweli zinazofaa hasa kwa wakati wao. Kulikuwa na ukweli wa sasa katika siku za Luther; kuna ukweli wa sasa kwa ajili ya kanisa leo. Lakini ukweli hautakiwe na watu wengi leo kuliko ilivyokuwa na watu wa Papa waliompinga Luther. Wale wanaoonyesha ukweli kwa wakati huu hawapaswi kutazamia kupokewa na upendeleo mwingi zaidi kuliko watengenezaji wa zamani. Vita kuu kati ya kweli na uwongo, kati ya Kristo na Shetani, itaongezeka kwa mwisho wa historia ya ulimwengu huu. Tazama Yoane 15:19, 20; Luka 6:26.TSHM 63.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents