Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kushika Siku ya Kwanza (Jumapili)

  Kushika siku ya kwanza (jumapili) ni desturi ilioanzishwa na Roma, ambayo anadai kuwa alama ya mamlaka yake. Roho ya Kanisa la Roma (Papa)--ya mapatano kwa desturi za kidunia, heshima kwa desturi za kibinadamu juu ya amri za Mungu--inaenea sehemu zote za makanisa ya Waprotestanti na kuwaongoza kwa kazi ya namna moja ya kutukuza Siku ya kwanza (Jumapili) ambayo kanisa la Roma limeigeuza mbele yao.TSHM 279.4

  Sheria za kifalme, baraza za kawaida na maagizo ya kanisa zilizokubaliwa na mamlaka ya kidunia zilikuwa ni hatua ambazo siku kuu za kishenzi zilifikia cheo cha heshima katika dunia la Wakristo. Mpango wa kwanza wa kulazimisha watu wote kushika Siku ya kwanza ya juma ilikuwa sheria iliyotolewa na Constantine. Ingawa ilikuwa kweli sheria ya kipagani, ilikazwa na mfalme akiisha kukubali dini ya Kikristo.TSHM 280.1

  Eusebius, kama askofu aliyetafuta upendeleo wa watawala, na aliyekuwa rafiki wa kipekee wa Constantine, akaendesha matangazo ya kwamba Kristo alihamisha Sabato na kuiweka kwa siku ya kwanza (dimanche). Hakuna ushuhuda wa Maandiko uliotolewa kuwa uhakikisho. Eusebius yeye mwenyewe, bila kuwa na hakikisho akatangaza uwongo wake. “Vitu vyote,” anasema, “Kila kitu kilichokuwa kazi ya kufanya kwa Sabato, hivi tumevihamisha kwa siku ya Bwana”. 2TSHM 280.2

  Kwa namna Kanisa la Roma lilipoimarishwa, kutukuzwa kwa Siku ya Kwanza kukaendelea. Kwa wakati mfupi siku ya saba iliendelea kushikwa kama Sabato, lakini baadaye badiliko likafanyika. Baadaye Papa akatoa maagizo ya kwamba padri wa wilaya alipaswa kukaripia wanaoharibu siku ya kwanza (dimanche) wasilete msiba mkubwa juu yao wenyewe na kwa jirani.TSHM 280.3

  Amri za baraza zilizo hakikisha upungufu, wakubwa wa serkali wakaombwa sana kutoa amri ambayo ingeogopesha mioyo ya watu na kuwalazimisha kuacha kazi kwa siku ya kwanza (dimanche). Kwa mkutano wa wakubwa wa kanisa uliofanywa Roma, mipango yote ya mbele ikahakikishwa tena na kuingizwa katika sheria ya kanisa na kukazwa na wakubwa wa serikali.3TSHM 280.4

  Lakini ukosefu wa mamlaka ya maandiko kwa ajili ya kushika siku ya kwanza (dimanche) ukaleta mashaka. Watu wakauliza haki ya waalimu wao kwa ajili ya kutia pembeni tangazo hili, “Siku ya saba ni Sabato kwa Bwana Mungu wako,” ili kuheshimu siku ya jua. Kwa kusaidia ukosefu wa ushuhuda wa Biblia, mashauri mengine yalikuwa ya lazima.TSHM 280.5

  Musimamizi wa nguvu wa siku ya kwanza (dimanche), ambaye karibu mwisho wa karne ya kumi na mbili alizuru makanisa ya Uingereza, akapingwa na washuhuda waaminifu kwa ajili ya kweli; na kwa hivi nguvu yake ilikuwa ya bure hata akatoka kwa inchi wakati moja. Wakati aliporudi, akaleta mkunjo waonyesho ambayo alidai kutoka kwa Mungu mwenyewe, iliyokuwa na agizo la kulazimisha watu kushika siku ya kwanza (dimanche), pamoja na matisho ya ajabu kuogopesha wasiotii. Maandiko haya ya damani yalisemwa wala kutajwa kuwa ya kuanguka kutoka mbinguni na kupatikana pale Yerusalema juu ya mazabahu ya Simeona Mtakatifu, katika Golgotha. Lakini, kwa kweli yaliandikwa katika jumba kubwa la askofu kule Roma. Madanganyo na maandiko ya uwongo yalikuwa katika miaka yote yakihesabiwa ya kweli kwa watawala wa kanisa la Roma. (Tazama kwa Mwisho wa Kitabu (Nyongezo), hati kwa ukarasa 37.)TSHM 280.6

  Lakini ijapo walifanya nguvu kwa kuanzisha utakatifu wa Siku ya kwanza (dimanche) wakuu wa kanisa la Roma wao wenyewe kwa wazi wakatubu kwamba sabato inatoka kwa mamlaka ya Mungu. Katika karne ya kumi na sita baraza la Papa ikatangaza: “Acha Wakristo wote wakumbuke ya kwamba siku ya saba ilitakaswa na Mungu, na ilikubaliwa na kushikwa, si kwa Wayuda tu, lakini na kwa wengine wote wanaodai kuabudu Mungu; ingawa sisi Wakristo tumebadilisha Sabato yao kwa Siku ya Bwana.”4 Wale waliokuwa wakiharibu sheria ya Mungu walikuwa wanajua tabia ya kazi yao.TSHM 281.1

  Mufano wa kushangaza wa mipango ya Roma ulitolewa katika mateso marefu ya mauaji juu ya Waldenses (Vaudois), wengine wao walikuwa washika Sabato. (Tazama Nyongezo.) Historia ya makanisa ya Ethiopia na Abyssinia ni ya maana ya kipekee. Katikati ya huzuni ya Miaka ya Giza, Wakristo wa Afrika ya Kati walifichama kwa uso wa dunia na wakasahauliwa na ulimwengu na kwa karne nyingi wakafurahia uhuru katika imani yao. Mwishoni Roma ikajifunza juu ya maisha yao, na mfalme wa Abyssinia akadanganywa hata akakubali Papa kama mjumbe mkubwa wa Kristo. Amri ikatolewa kukataza kushikwa kwa Sabato chini ya malipizi makaii.5 Lakini uonevu wa Papa (kanisa la Roma) kwa upesi ukawa nira ya kutia uchungu sana ambayo watu wa Abyssinia wakakusudia kuivunja. Wakuu wa Roma wakafukuziwa mbali kwa mamlaka yao na imani ya zamani ikarudishwa.TSHM 281.2

  Wakati makanisa ya Afrika yalipokuwa yakishika Sabato katika utii kwa amri za Mungu, wakaepuka na kufanya kazi siku ya kwanza (dimanche) kwa kufuatana na desturi ya kanisa. Roma ikavunja Sabato ya Mungu kwa kujiinua mwenyewe, lakini makanisa ya Afrika, yakajificha karibu miaka elfu moja, hayakushirikiana kwa uasi huu. Walipoletwa chini ya Roma, wakalazimishwa kuweka pembeni kweli na kutukuza sabato ya uwongo. Lakini kwa upesi walipopata tena uhuru wao wakarudia kutii amri ya ine. (Tazama Nyongezo).TSHM 281.3

  Mambo haya yanaonyesha wazi uadui wa Roma kwa ajili ya Sabato ya kweli na wasimamizi wake. Neno la Mungu linafundisha ya kwamba mambo haya yanapashwa kutendeka tena kwa namna kukaririwa kama vile Wakatoliki na Waprotestanti wanajiunga kwa kutukuza siku ya kwanza (dimanche).TSHM 281.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents