Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Makosa ya Hatari

  Miongoni mwa vyombo vya ushindi zaidi vya mdanganyi mkubwa ni maajabu ya uwongo ya imani ya roho za watu waliokufa (spiritisme). Kwa namna watu wanavyokataa kweli wanatekwa kwa udanganyifu.TSHM 256.1

  Kosa lingine ni mafundisho yanayokana Umungu wa Kristo, kudai kwamba hakuwako mbele ya kuja kwake kwa ulimwengu huu.TSHM 256.2

  Maelezo haya yanakausha maneno ya Mwokozi wetu juu ya uhusiano wake na Baba na kuwako kwake siku zote za mbele. Yanaharibu imani katika Biblia kama ufunuo kutoka kwa Mungu. Kama watu wanakana ushuhuda wa Maandiko juu ya Umungu wa Kristo, ni bure kubishana nao; hakuna mabishano, hakuna neno hata wazi la kuweza, kuwasadikisha; Hakuna anayeshikilia kosa hili anayeweza kuwa na wazo la kweli la Kristo wala la mpango wa Mungu kwa ajili ya ukombozi wa mtu.TSHM 256.3

  Tena kosa lingine ni imani kwamba Shetani haishi kama kiumbe chenye nafsi, kwamba jina linalotumiwa katika Maandiko ni kufananisha tu mawazo mabaya ya watu na tamaa.TSHM 256.4

  Mafundisho kwamba kuja kwa mara ya pili kwa Kristo ni kuja kwake kwa kila mtu wakati wa mauti ni uongo kwa kupotosha akili kusahau kwa kuja kwake mwenyewe katika mawingu ya mbingu. Shetani basi amekuwa akisema, ‘’Tazama, yeye ni katika vyumba vya ndani” (Tazama Matayo 24:23-26), na wengi wamepotea katika kukubali udanganyifu huu.TSHM 256.5

  Tena watu wa maarifa wanadai kwamba hakuna jibu la kweli linaweza kuwako kwa kuomba; hii ingekuwa uvunjaji wa sheria-mwujiza, na miujiza haiwezi kuwako. Ulimwengu, wanasema, unatawaliwa katika sheria zisizobabilika, na Mungu Mwenyewe hafanye kitu kinyume kwa sheria hizi. Kwa hivi wanafananinisha Mungu kama amelazimishwa katika sheria zake mwenyewe--kana kwamba sheria za Mungu zingekataza uhuru wa Mungu. Fundisho la namna hii linapinga ushuhuda wa maandiko.TSHM 256.6

  Je, miujiza haikufanywa na Kristo na mitume wake? Mwokozi yule yule anapendezwa basi kusikiliza maombi ya imani kama vile alivyotembea kwa wazi miongoni mwa watu. Hali ya viumbe vinashirikiana na hali ya Mungu. Ni sehemu ya mpango wa Mungu kutusaidia, katika jibu kwa ombi la imani, lile ambalo hangali- toa tusilouliza.TSHM 256.7

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents