Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wanadamu Wawili Wanakutana

  Wakati waliookolewa wanapokaribishwa kwa mji wa Mungu, hapo kunakuwa kilio cha shangwe nyingi. Wanadamu wawili ni karibu kukutana. Mwana wa Mungu anapashwa kupokea baba wa taifa letu--aliyeumbwa, aliyefanya zambi, na kwa ajili ya zambi yake alama za msalaba zinakuwa kwa sura ya Mwokozi. Wakati Adamu alipotambua alama za misumari, kwa unyenyekevu anaanguka yeye mwenyewe kwa miguu ya Kristo. Mwokozi anamwinua na kumwalika kutazama tena kwa makao ya Edeni ambapo amehamishwa kwa wakati mrefu.TSHM 314.3

  Maisha ya Adamu yalijazwa na huzuni. Kila jani lililokufa, kila nyama wa kafara, kila doa juu ya utakatifu wa mtu, ilikuwa ukumbusho wa zambi yake. Maumivu ya majuto yalikuwa ya kutisha sana wakati alipokutana na laumu zilizotupwa juu yake mwenyewe kama sababu ya zambi. Kwa uaminifu akatubu zambi yake, na alikufa katika tumaini la ufufuko. Sasa, kwa njia ya upatanisho, Adamu amerudishiwa hali ya kwanza.TSHM 315.1

  Alipojazwa na furaha, anatazama miti ambayo ilikuwa mara ya kwanza furaha yake, matunda yake yeye mwenyewe alikuwa akikusanya mbele ya kuwa na hatia. Ameona mizabibu ambayo mikono yake mwenyewe ilikomalisha, maua aliyoyapenda zamani kulinda. Hii ni Edeni iliyorudishwa kweli!TSHM 315.2

  Mwokozi akamwongoza kwa mti wa uzima na akamwalika kula. Akatazama mkutano wa jamaa yake waliokombolewa. Ndipo akatupa taji lake kwa miguu ya Yesu na kumkumbatia Mkombozi. Akagusa kinubi, na sehemu ya juu pa mbingu ikarudisha mwitiko wa sauti za wimbo wa ushindi: “Anastahili Mwana kondoo” aliyechinjwa”. Ufunuo 5:12. Jamaa ya Adamu inatupa taji zao kwa miguu ya Mwokozi wanapoinama wakiabudu. Malaika walilia kwa kuanguka kwa Adamu na wakafurahi wakati Yesu alipofungua kaburi kwa wote walioamini kwa jina lake. Sasa wanatazama kazi ya ukombozi kutimizwa na kuunga sauti zao kwa kusifu.TSHM 315.3

  Kwa “bahari ya kioo iliyochanganyika na moto” wamekutanika kundi la watu ambao “waliomshinda yule mnyama na sanamu na alama yake, na hesabu ya jina lake”. Wale elfu mia moja na makumi ine na ine waliokombolewa katika watu, na wanaimba “wimbo mpya” wimbo wa Musa na wimbo wa Mwana-Kondoo. Ufunuo 15:2,3. Hakuna mtu bali wale elfu mia moja na makumi ine na ine watakaoweza kujifunza wimbo ule, kwa maana ni wimbo wa mambo ya maisha ambayo hakuna jamii ingine walikuwa nayo”. Hawa ndio wanaofuata Mwana-Kondoo kila pahali anapokwenda. “Hawa waliochukuliwa kutoka katikati ya wahai, ni “malimbuko ya kwanza kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo”. Ufunuo 14:4,5. Walipitia katika wakati wa mateso makubwa ambayo hayajakuwako tangu taifa lilikuwako; walivumilia maumivu makuu ya wakati wa taabu ya Yakobo; walisimama pasipo mwombezi katika kumiminwa kwa mwisho kwa hukumu za Mungu. “Wamefua mavazi yao na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo”. “Na katika vinywa vyao haukuonekana uwongo; maana wao ni pasipo kilema” mbele ya Mungu. “Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala joto lo lote. Kwani Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi atawachunga, naye atawaongoza hata chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atapangusa machozi yote katika macho yao”. Ufunuo 7:14; 14:5; 7:16,17.TSHM 315.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents