Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Usikivu na Kutokuamini

  Usikivu ukaendelea kuongezeka. Kutoka kwa makumi mawili na mamia, makutano yakaongezeka kwa maelfu mengi. Lakini baada ya wakati, upinzani ulionekana juu ya hawa waliogeuka, makanisa yakaanza kuchukua hatua za kutiisha kwa wale waliokubali maoni ya Miller. Jambo hili likaita jibu kwa kalamu yake: “Kama tunakuwa wakosefu ninawaomba mtuonyeshe kwa namna gani kosa letu linakuwa kutoka katika neno la Mungu; tulichekwa ya kutosha; na ile haiwezi kutusadikisha kwamba tunakuwa katika kosa; Neno la Mungu pekee linaweza kugeuza maoni yetu. Hukumu yetu ilifanyika kwa kusudi pamoja na maombi, kama tulivyoona ushuhuda katika Maandiko.”TSHM 160.4

  Wakati uovu wambele ya garika ulipomsukuma Mungu kuleta garika duniani, kwanza akawajulisha kusudi lake. Kwa miaka 120 likasikiwa onyo kwa kutubu. Lakini hawakuliamini. Wakazarau mjumbe wa Mungu. Kama ujumbe wa Noa ulikuwa wa kweli, sababu gani watu wote wa dunia hawakuuona na kuuamini? Tendo la kudai haki la mtu mmoja kupinga hekima ya maelfu! Hawakuweza kuamini onyo wala kutafuta kimbilio ndani ya safina.TSHM 161.1

  Watu wa zarau wakaonyesha kwa mwandamano usiobadilika wa majira, mbingu za rangi ya samawi zisizonyesha mvua kamwe. Katika zarau wakatangaza mhubiri wa haki kama mwenye juhudi ya kishenzi. Wakaenda zao, kujikaza zaidi kwa njia zao mbovu kuliko mbele. Lakini kwa wakati uliotajwa Hukumu za Mungu zikaanguka juu ya waliokataa huruma yake.TSHM 161.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents