Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Hukumu Inatangazwa Juu ya Waasi

  Mbele ya wakaaji waliokusanyika wa dunia na wa mbinguni kwa mkutano na kuviikwa taji kwa Mwana wa Mungu. Na sasa, kuvikwa mamlaka makubwa na uwezo, Mfalme wa wafalme anatangaza hukumu juu ya waasi waliovunja sheria yake na kutesa watu wake. “Nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, naye anayeketi juu yake, dunia na mbingu zikakimbia uso wake; na pahali pao hapakuonekana. Nikaona wafu, wakubwa na wadogo, wamesimama mbele ya Mungu, na vitabu vikafunuliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, kilicho cha uzima; na wafu wakahukumiwa katika mambo haya yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao”. Ufunuo 20:11, 12.TSHM 325.2

  Wakati jicho la Yesu linapoangalia juu ya waovu, wanakuwa na ufahamu wa kila zambi waliyoitenda. Wanaona pahali miguu yao ilipoacha njia ya utakatifu. Majaribu ya kuvuta ambayo waliimarisha kwa anasa katika zambi, wajumbe wa Mungu waliozarauliwa, maonyo yaliyokataliwa, mawimbi ya rehema yaliyorudishwa kwa ukaidi, moyo usiotubu--yote inaonekana kama yameandikwa kwa maandiko ya moto.TSHM 325.3

  Juu ya kiti cha enzi kunafunuliwa msalaba. Kwa maoni kamili kukatokea mambo ya kuanguka kwa Adamu na hatua za kufuatana katika shauri la wokovu. Kuzaliwa kwa unyenyekevu kwa Mwokozi; maisha yake ya kawaida; ubatizo wake katika Yorodani; kufunga na majaribu katika jangwa; huduma yake kufunua kwa watu mibaraka ya mbinguni; siku zilizojaa na matendo ya rehema, usiku wa kukesha katika maombi kule milimani; mashauri ya hila ya tamaa na uovu ambayo yalilipa faida zake; maumivu makali ya siri katika Getesemane chini ya uzito wa zambi za ulimwengu; usaliti wake kwa kundi la wauaji, matukio ya usiku ule wa kitisho kikuu-mfungwa asiyeshindana aliyeachwa na wanafunzi wake, aliyeshitakiwa katika jumba la kuhani mkuu, katika chumba kikubwa cha hukumu cha Pilato, mbele ya Herode mwenye hofu, aliyechekelewa, kutukanwa, kuteswa, na kuhukumiwa kufa--yote yanaelezwa kwa wazi.TSHM 325.4

  Na sasa mbele ya makutano yaliyowayawaya maoni ya mwisho yanafunuliwa; Mteswaji mvumulivu akakanyanga njia ya Kalvari; Mfalme wa mbinguni kutundikwa msalabani; makuhani na walimu wakachekelea maumivu makali ya kukata roho yake; giza kubwa sana kuonyesha wakati wakati Mkombozi wa ulimwengu alipotoa maisha yake.TSHM 325.5

  Ajabu ya kutisha inaonekana kama tu ilivyokuwa. Shetani na watu wake hawana uwezo wa kugeuza na kutoka kwa picha. Yeyote aliyehusika kwa kufanya tendo anakumbuka sehemu aliyoifanya. Herode, aliyewaua watoto wasiokuwa na kosa wa Betelehemu; chanzo Herodias, ambaye juu ya nafsi yake kunadumu damu ya Yoane Mtabizaji; mzaifu, Pilato mwenye kulinda wakati; askari wenye kuchekelea; msongano wa watu wenye wazimu waliopaaza sauti, “damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu”! --kutafuta namna yote bila kuweza kujificha kutoka kwa utukufu wa uso wake Mungu, wakati waliokombolewa wanapotupa taji zao kwa miguu ya Mwokozi, kuapaaza sauti, “Alikufa kwa ajili yangu”!TSHM 326.1

  Hapo kuna Neno, mkatili mkali na muovu, kutazama utukufu wa wale aliowatesa na kwa maumuvu yao akapata furaha ya kishetani. Mama yake anashuhudia kazi yake mwenyewe, namna gani tamaa alizoendelesha na mvuto wake na mfano zimezaa matunda katika mauaji yaliyoletea dunia kutetemeka.TSHM 326.2

  Hapo kunakuwa mapadri wa Papa na maaskofu waliojidai kuwa mabalozi wa Kristo, huku walipokuwa wakitumia mbao zenye vyango vya kutundikia watu, gereza, na kigingi kwa kutawala watu Wake. Hapo panakuwa maaskofu wenye kiburi waliojiinua wenyewe juu ya Mungu na wakasubutu kugeuza sheria ya Mungu Aliye juu. Wale waliojidai kuwa wababa wanakuwa na hesabu ya kutoa kwa Mungu. Kwa mda kitambo unapopita wamefanywa kuona ya kwamba Mwenye Kujua yote anakuwa na wivu wa sheria yake. Wanajifunza sasa ya kwamba Kristo anatambua faida zake pamoja na watu wake wanaoteseka.TSHM 326.3

  Ulimwengu mzima wenye uovu unasimama kwakushitaki kwa ajili ya maasi makubwa juu ya kupinga serkali ya mbinguni. Hawana yeyote kwa kutetea maneno yao; hawana sababu yo yote; na hukumu ya mauti ya milele inatangazwa juu yao.TSHM 326.4

  Waovu wanaona kile walichopotewa kwa sababu ya uasi wao. “Yote hii”, nafsi iliyopotea inalia, “ningaliweza kuwa nayo, Ee, upumbafu wa namna gani! nimebadili amani, furaha, na heshima kwa ajili ya ubaya, sifa mbaya, na kukata tamaa”. Wote wanaona ya kwamba kufukuzwa kwao mbinguni ni kwa haki. Katika maisha yao wametangaza: “Hatuwezi kuwa na mtu huyu (Yesu) kutawala juu yetu”.TSHM 326.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents