Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  12 / MAPAMBAZUKO KATIKA UFRANSA

  Ushuhuda wa Spires na Ungamo la Augsburg yalifuatwa na miaka ya vita na giza. Yakazoofishwa na migawanyiko, Kiprotestanti kikaonekana katika hali ya kuangamizwa.TSHM 97.1

  Lakini wakati wa ushindi huu wa wazi mfalme akapigana sana na kushindwa. Mwishowe akalazimishwa kukubali kuachia uhuru mafundisho ambayo ilikuwa tamaa ya nguvu katika maisha yake ya kuyaharibu. Aliona majeshi yake kuangamizwa na vita, hazina zake kutiririka, watu wengi wa ufalme wake kutiishwa na uasi, na po pote ambapo imani aliyojitahidi kukomesha ikaenea. Charles V alikuwa akigombeza uwezo wa Mwenye mamlaka yote. Mungu alisema, “Nuru iwe,” lakini mfalme akataka kudumisha giza. Aliposhindwa kutimiza makusudi yake, akazeeka upesi, akajitosha kitini cha ufalme na akaenda kujizika mwenyewe katika nyumba ya watawa.TSHM 97.2

  Katika Uswisi, hivi makambi mengi yalikubali imani ya Matengenezo, wengine wakajifungia kwa imani ya Roma. Mateso juu ya wafuasi ikaamka kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Zwingli na wengi waliojiunga katika Matengenezo wakaanguka kwa shamba la damu la Cappel. Roma ikawa na ushindi na katika mahali pengi ikaonekana kupata yote aliyopoteza. Lakini Mungu hakusahau kazi yake wala watu wake. Kwa upande mwengine akainua watumishi kuendesha kazi ya Matengenezo.TSHM 97.3

  Katika Ufransa mmojawapo wa kwanza kupata nuru alikuwa ndiye Lefévre; mwalimu katika chuo kikuu cha Paris. Katika uchunguzi wake wa vitabu vya maandiko ya zamani, uangalifu wake ukaongozwa kwa Biblia, na akaingiza mafundisho yake miongoni mwa wanafunzi wake. Akaanza kutayarisha historia ya watakatifu wa wafia dini kama ilivyotolewa katika mapokeo ya kanisa, na alikuwa amekwisha kufanya maendeleo ya namna sana kwa hayo, alipofikiri kwamba angeweza kupata usaada kutoka kwa Biblia, akaanza mafundisho yake. Na hapa kweli akapata watakatifu, lakini si kama vile ilionekana katika kalenda ya Roma (Kanisa la Katoliki). Katika machukio akaenda zake kwa kazi aliyojiagizia mwenyewe na akajitoa wakfu kwa Neno la Mungu.TSHM 97.4

  Katika mwaka 1512 kabla ya Luther ao Zwingli walikuwa hawajaanza kazi ya Matengenezo, Lefévre akaandika, “Ni Mungu anayetupatia, kwa imani, haki ile ambayo kwa neema pekee hutuhesabia haki kwa uzima wa milele.” Na wakati alipofundisha kwamba utukufu wa wokovu ni wa Mungu tu, na akatangaza pia kwamba kazi ya kutii ni ya binadamu.TSHM 97.5

  Wengine miongoni mwa wanafunzi wa Lefévre wakasikiliza kwa bidii maneno yake na wakati mrefu baada ya sauti ya mwalimu kunyamaza, wakaendelea kutangaza ukweli. Mmoja wao alikuwa William Farel. Alikelewa kwa wazazi watawa na mkatoliki mwenye juhudi, alitamani sana kuharibu kila kitu kilichojaribu pinga kanisa. “Ningesaga meno yangu kama mbwa mwitu mkali,” akasema baadaye. “Ninaposikia mtu ye yote kusema kinyume cha Papa.” Lakini ibada ya watakatifu, kuabudu mbele ya mazabahu, na kupambwa na zawadi za mahali patakatifu hakukuweza kuleta amani ya roho. Kusadikishwa kwa zambi kukaimarishwa juu yake, ambako matendo yote ya toba yalishindwa kumupa uhuru. Akasikiliza maneno ya Lefévre: “Wokovu ni kwa neema.” “Ni msalaba wa Kristo tu unaofungua milango ya mbinguni, na kufunga milango ya kuzimu.”TSHM 98.1

  Kwa kutubu kama kule kwa Paulo, Farel akageuka kutoka kwa utumwa wa asili hata kwa uhuru wa wana wa Mungu. “Baada ya moyo wa uuaji wa mbwa mwitu mkali,” akarudi akasema, “kwa kimya kama mwana kondoo mwema na mpole, moyo wake wote umeondolewa kwa Papa, na ukatolewa kwa Yesu Kristo.”TSHM 98.2

  Wakati Lefévre alipokuwa akitawanya nuru miongoni mwa wanafunzi, Farel akaendelea kutangaza kweli wazi wazi. Mkuu mmoja wa kanisa, askofu wa Meaux, akajiunga mara kwao. Waalimu wengine wakaungana katika kutangaza injili, na ikavuta wafuasi kutoka kwa makao ya wafundi na wakulima hata kwa jumba la mfalme. Dada wa Francis I akakubali imani ya Matengenezo. Kwa matumaini bora ya Watengenezaji walitazamia wakati ambapo Ufransa ulipaswa kuvutwa kwa injili.TSHM 98.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents