Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  27 / UFUFUO WA KISASA UNAKUWA NA MAFANIKIO NAMNA GANI?

  Popote Neno la Mungu lilipohubiriwa kwa uaminifu, matokeo yaliyofuata ni ya kushuhudia asili yake ya kimungu. Wenye zambi walijisikia zamiri zao kuamka. Hakikisho la kosa likashikilia nia zao na mioyo yao. Walikuwa na utambuzi wa haki ya Mungu, na wakapaza sauti: “Nani atakayeniokoa na mwili huu wa kufa?” Waroma 7:24. Kama vile msalaba ulivyofunuliwa, waliona kwamba hakuna kitu kingine bali tabia nzuri tu za Kristo ziliweza kupatanisha kwa ajili ya makosa yao. Kwa damu ya Yesu walikuwa na “ondoleo la zambi zile zilizopita.” Waruma 3:25.TSHM 223.1

  Roho hizi zikaamini na zikabatizwa na wakasimama kwa kutembea katika upya wa uzima, kwa imani ya Mwana wa Mungu kwa kufuata hatua zake, kuonyesha tabia yake, na kujitakasa wao wenyewe kama yeye ni mutakatifu. Vitu walivyokuwa wakichukia sasa wakavipenda, na vile walivyokuwa wakipenda wakavichukia. Mwenye kiburi akawa mpole, mtu asiyefaa na wa kujivuna akawa wa maana na mnyenyekevu. Mlevi akawa mwenye busara, mpotovu akawa mtakatifu. Wakristo hawakutafuta “kujipamba kwa kusuka nywele, na kuvaa vitu vya zahabu, ao kuvaa mavazi; lakini ... katika mapambo yasiyoharibika, ndiyo roho ya upole na utulivu iliyo ya damani kubwa mbele ya Mungu.” 1 Petro 3:3,4.TSHM 223.2

  Maamsho yaliamshwa na miito ya upole kwa mwenye zambi. Matunda yalionekana katika roho zilizojitenga si kwa kujikana mwenyewe bali wakafurahi kwamba walihesabiwa kustahili kuteswa kwa ajili ya Kristo. Watu wakaona badiliko katika wale waliotangaza jina la Yesu. Ni vile mambo yalivyokuwa katika miaka ya kwanza iliofuata nyakati za uamsho wa dini.TSHM 223.3

  Lakini maamsho mengi ya nyakati za kisasa yanaonyesha tofauti kubwa. Ni kweli kwamba wengi wanatangaza toba, na wengi wanaingia ndani ya makanisa. Hata hivyo matokeo si ya namna kama ya kushuhudia imani kwamba hapo kumekuwa na maendeleo ya kulingana ya maisha ya kiroho ya kweli. Nuru ambayo inawaka kwa muda ikafa kwa upesi.TSHM 223.4

  Maamsho ya watu wengi mara nyingi yanaamsha sikitiko, hupendeza watu kwa kitu kinachokuwa kipya na cha kwanza. Kwa hivyo wale waliogeuka wanakuwa na haja kidogo kusikiliza kweli ya Biblia. Isipokuwa hudumu ya kanisa inakuwa na kitu cha tabia ya ajabu, kama si vile, haina mvuto kwao.TSHM 223.5

  Kwa kila roho iliyogeuka kweli uhusiano kwa Mungu na kwa vitu vya milele utakuwa ni kitu kikubwa chakuzungumuziwa katika maisha. Ni pahali gani katika makanisa ya watu wengi ya leo kunapatikana roho ya kujitoa kwa Mungu? Waliogeuka hawaache kiburi na mapendo ya dunia. Hawakubali tena kuikana nafsi na kufuata Yesu mpole na mnyenyekevu kuliko mbele ya toba yao. Utawa karibu kutoka kwa wengi wa makanisa.TSHM 224.1

  Ijapo imani ilipunguka mahali pengi sana, kunakuwa wafuasi wa kweli wa Kristo katika makanisa haya. Kabla ya kufika kwa hukumu za Mungu za mwisho, kutakuwa katikati ya watu wa Bwana uamsho wa utawa wa zamani za mababu ambao haujashuhudiwa tangu nyakati za mitume. Roho ya Mungu itamwangiwa. Wengi watajitenga kwa makanisa hayo ambayo mapendo ya dunia hii yaliondoa upendo kwa Mungu na Neno lake. Wahubiri wengi na watu watakubali kwa furaha zile kweli kubwa ambazo zinatayarisha watu kwa kuja kwa Bwana mara ya pili.TSHM 224.2

  Adui wa roho anataka kuzuia kazi hii, na kabla ya kufika kwa mwenendo wa namna hiyo, atafanya nguvu kuuzuia kwa njia ya kuingiza mwigo. Katika makanisa yale ambayo anaweza kuleta chini ya mamlaka yake ataifanya kuonekana kwamba baraka ya kipekee ya Mungu imemwangwa juu yao. Makutano yatashangilia, “Mungu anatumika kwa ajabu,” wakati ile kazi ni ya roho ingine. Chini yamtindo wa dini, Shetani atatafuta kueneza mvuto wake kwa ulimwengu wa Wakristo. Hapo kunakuwa mwamsho wa maono, mchanganyiko wa kweli na uwongo, uliotengenezwa vizuri sana kwa kudanganya.TSHM 224.3

  Lakini katika nuru ya Neno la Mungu si vigumu kutambua tabia ya kazi hizi. Pahali pote watu wanapozarau ushuhuda wa Biblia, kugeukia mbali na hizi zilizo zaili zinazo jaribu roho ambazo zinaomba kujikana mwenyewe na kukana dunia, hapo tunaweza kuwa na hakika kwamba baraka ya Mungu haikutolewa. Na kwa amri, “Mutawatambua kwa njia ya matunda yao,” (Matayo 7:16), ni ushuhuda kwamba kazi hizi si kazi ya Roho ya Mungu.TSHM 224.4

  Ukweli ya Neno la Mungu inakuwa ngao juu ya madanganyo ya Shetani. Kuzarau kweli hizi kulifungua mlango kwa maovu yanayoenea sasa katika ulimwengu. Umuhimu wa sheria ya Mungu umesahauliwa kwa eneo kubwa sana. Wazo mbaya juu ya sheria ya Mungu limeongoza kwa makosa katika toba na utakaso, kwa kushusha kipimo cha utawa. Hapa ndipo panapopatikana siri ya ukosefu wa Roho ya Mungu katika maamsho ya wakati wetu.TSHM 224.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents