Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Picha mbili Inamvuta Huss

  Kwa wakati huu, wageni wawili kutoka Uingereza, watu wa elimu, walipokea nuru na wakaja kuieneza katika Prague. Kwa upesi wakanyamazishwa, lakini kwa sababu hawakutaka kuacha kusudi lao, wakatafuta mashauri mengine. Walipokuwa wafundi pia wahubiri, katika mahali wazi mbele ya watu wakachora picha mbili. Moja ikaonyesha kuingia kwa Kristo katika Yerusalema, “Mpole, naye amepanda mwana punda” (Matayo 21:5) na akafuatwa na wanafunzi wake katika mavazi ya kuzeeka juu ya safari na miguu wazi. Picha ingine ilieleza mwandamano wa askofu-papa katika kanzu zake za utajiri na taji tatu, mwenye akapanda farasi ambaye amepambwa vizuri sana, ametanguliwa na wapiga tarumbeta na kufuatwa na wakuu wa baraza ya papa (cardinals) na maaskofu katika mavazi ya kifalme.TSHM 40.2

  Makutano yakaja kutazama mapicha. Hapana mtu aliweza kushindwa kusoma maana. Kukawa makelele mengi katika Prague, na wageni wakaona kwamba inafaa kuondoka. Lakini picha ikaleta wazo kubwa kwa Huss na ikamwongoza karibu sana na uchunguzi wa Biblia na wa maandiko ya Wycliffe.TSHM 40.3

  Ingawa alikuwa hakujitayarisha bado kukubali matengenezo yote yaliyotetewa na Wycliffe, aliona tabia ya kweli ya kanisa la Roma, na akalaumu kiburi, tamaa ya nguvu, na makosa ya mamlaka ya dini.TSHM 40.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents