Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  18 / NURU MPYA KATIKA DUNIA MPYA

  Mkulima mwaminifu, wa haki, ambaye alitamani kujua ukweli, alikuwa mtu aliyechaguliwa na Mungu kuongoza katika kutangaza kuja kwa Kristo mara ya pili. Kama watengenezaji wengi wengine, William Miller alipigana na umaskini na akajifunza fundisho la kujikana.TSHM 150.1

  Hata katika utoto alitoa ushuhuda wa uwezo wa akili zaidi kuliko ule wa kawaida. Kwa kukomaa kuwa mtu mzima, akili yake ilikuwa ya utendaji na ikaendelea sana, na alikuwa na kiu cha bidii kwa maarifa. Upendo wake wa kujifunza na tabia ya mafikara ya uangalifu kuambatana na ujuzi vikamfanya kuwa mtu wa hukumu na maono ya uchunguzi. Alikuwa na tabia ya matendo mema isiyolaumiwa na sifa nzuri. Alifanya kazi za serkali na za kiaskari pamoja na sifa njema. Utajiri na heshima vilionekana kufunguliwa sana kwake.TSHM 150.2

  Katika utoto alikuwa mtu wa mawazo ya dini. Mawazo ya mtu mkubwa, kwa hivi akajiingiza katika jamii ya watu wanaokuwa na imani katika Mungu (deistes), mvuto wake ulikuwa wa nguvu kwa jambo kwamba walikuwa karibu raia wema,wapole na wakarimu. Kuishi kati ya vyama vya Kikristo, tabia zao zilikuwa za kadiri zilizofanywa na wale waliowazunguuka. Kwa ajili ya wema ambao uliwapatia heshima, wakawapashwa kushukuru Biblia, na zawadi hizi nzuri zikawaongoza kwa kutumia mvuto juu ya Neno la Mungu. Miller akaongozwa kuitika nia zao.TSHM 150.3

  Mafasiri ya kisasa ya Maandiko yalionyesha magumu ambayo ilionekana kwake kwamba kubwa sana; lakini imani mpya yake, kwa kuweka Biblia kando, haikumsaidia kitu, na akawa mbali ya kutoshelewa. Lakini wakati Miller alipokuwa na miaka makumi tatu na ine, Roho Mtakatifu akamfahamisha moyo wake kwa hali aliyokuwamo kama mwenye zambi. Hakuona tumaini la furaha ngambo ya pili ya kaburi. Wakati ujao ulikuwa giza na huzuni. Kwa kutazama mawazo yake ya moyo kwa wakati huu, akasema: 1Deism : ni imani kwamba Mungu anakuwako na aliumba ulimwengu, lakini baadaye hakutumia uongozi juu yake ao kujali maisha ya watu; imani kwamba akili inatosha kwa maarifa ya kweli, kwa hiyo wakakataa ufunuo. Webster’s New World Dictionary.TSHM 150.4

  “Mbingu zilikuwa kama shaba juu ya kichwa changu, na dunia kama chuma chini ya miguu yangu... Nilipofikiri zaidi hukumu zangu zikatawanyika. Nikajaribu kukataza mawazo yangu, lakini mawazo yangu haikuweza kutawalika. Nikawa maskini kwa kweli, lakini bila kufahamu sababu. Nikanungunika na kulalamika, lakini sikujua juu ya nani. Nikajua kwamba kosa lilikuwako, lakini sikujua namna gani ao mahali gani kupata haki.”TSHM 150.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents