Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Barua ya maagano wa Uhuru

  Tangazo la Amerika la Uhuru likatangazwa: “Tunashika kweli hizi kuwa zamiri binafsi, kwamba watu wote waliumbwa kuwa sawasawa; na kwamba Muumba aliwapa haki fulani zisizoondolewa; ambazo katika hizo kuna uzima, uhuru, na kutafuta furaha.” Serkali (ya Amerika) iliahidi heshima ya zamiri: “Baraza kuu halitaweza kufanya sheria hata moja inayosimamia kwa dini, ao inayokataza uhuru wa dini.”TSHM 139.1

  “Watengenezaji wa Serkali wakatambua kanuni ya milele kwamba uhusiano wa mtu na Mungu wake unakuwa juu ya sheria ya binadamu, na haki zake za zamiri ya daima... Ni kanuni yakuliwa ambayo hakuna kitu kitakacho weza kuiondoa.”TSHM 139.2

  Habari ikaenezwa katika Ulaya kwamba kuna inchi ambapo kila mtu anaweza kufurahiwa matunda ya kazi yake na kutii zamiri yake. Maelfu wakasongana kwa pande za pwani za Dunia Mpya. Katika miaka makumi mbili kutoka siku ya kufika mara ya kwanza huko Plymouth (1620), jinsi maelfu mengi ya Wasafiri walikaa katika Uingereza Mpya.TSHM 139.3

  “Hawakuomba kitu kwa inchi bali zawadi za kweli za kazi yao... Waliishi kwa uvumilivu wa taabu ya jangwani, wakanyunyizia maji ya mti wa uhuru kwa machozi yao, na jasho ya vipaji vya nyuso zao, hata ukatia mizizi yake chini sana katika inchi.”TSHM 139.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents