Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Waliokombolewa katika Utukufu

  Katika vizazi vyote wateule wa Mwokozi wametembea katika njia nyembamba. Wametakaswa katika tanuru ya mateso. Kwa ajili ya Yesu wakavumilia uchuki, masingizio, kujinyima, na hasara za uchungu. Walijifunza ubaya wa zambi, uwezo wake, kosa yake, msiba wake; wanaitazama na machukio makuu. Maana ya kafara isiyokuwa na mwisho iliyofanywa kwa ajili ya dawa yake inawanyenyekeza na kujaza mioyo yao na shukrani. Wanapenda sana kwa sababu walisamehewa sana. Tazama Luka 7:47. Washiriki wa mateso ya Kristo, wanastahili kuwa washiriki wa utukufu wake.TSHM 316.1

  Wariti wa Mungu wanatoka kwa vyjumba vya orofani, vibanda vibovu, gereza, mahali wauaji wanaponyongwa kwa sheria, milimani, jangwani, mapangoni. Walikuwa “maskini, wakiteswa, kusumbuliwa”. Mamilioni walienda kwa kaburi wakilemezwa na sifa mbaya kwa sababu walikataa kujitoa kwa Shetani. Lakini sasa hawateseki tena, hawatawanyike tena, na hawaonewe. Toka sasa wanasimama wanapovaa mavazi ya utajiri kuliko nguo watu walioheshimiwa sana wa dunia waliyovaa, kuvikwa na mataji ya utukufu zaidi kuliko yale yaliyovikwa kwa paji la uso ya wafalme wa dunia. Mfalme wa utukufu amepanguza machozi kwa nyuso zote. Wanatoa wimbo wa sifa, wazi, tamu, na wakupatana. Wimbo wa furaha ukaenea katika miruko ya mbinguni: “Wokovu kwa Mungu wetu anayeketi juu ya kiti cha enzi, na kwa Mwana-Kondoo”. Na wote wakaitika, “Amina: Baraka na utukufu, na hekima, na shukrani, na heshima, na uwezo, na nguvu kwa Mungu wetu hata milele na milele”. Ufunuo 7:10,12.TSHM 316.2

  Katika maisha haya tunaweza tu kuanza kufahamu asili ya ajabu ya wokovu. Kwa ufahamu wetu wenye mpaka tungeweza kufikiri zaidi kwa kweli haya na utukufu, uzima (maisha) na mauti, haki na rehema, yanayokutana katika msalaba; lakini kwa mvuto zaidi wa nguvu za akili yetu tunashindwa kuelewa maana yake kamili. Urefu na upana, urefu wa kwenda chini na urefu wa kwenda juu, wa upendo wa ukombozi unafahamika kidogo tu. Shauri la wokovu halitafahamika kamili, hata wakati waliokombolewa wanapoona kama wanavyoonwa na kujua kama wanavyojulikana; lakini katika vizazi vya milele kweli mpya itaendelea kufunuliwa akili ya ajabu na furaha. Ijapo masikitiko na maumivu na majaribu ya dunia yanapomalizika na sababu imeondolewa, watu wa Mungu watakuwa na maarifa ya kupambanua, na akili ya kufahamu bei ya wokovu wao. Msalaba utakuwa ni wimbo wa waliookolewa milele. Katika Kristo aliyetukuzwa wanamtazama Kristo aliyesulibiwa. Haitasahauliwa kamwe ya kwamba Mwenye Enzi wa mbinguni alijinyenyekeza mwenyewe kwa kuinua mtu aliyeanguka, ili achukue kosa na haya ya zambi na kuficha uso wa Baba yake hata misiba ya ulimwengu uliopotea unapovunja moyo wake na kuangamiza maisha yake. Muumba wa dunia yote akaweka pembeni utukufu wake sababu ya upendo kwa mtu--hii itaamsha milele mshangao wa viumbe vyote. Wakati mataifa ya waliookolewa wanapomtazama Mkombozi wao na kujua ya kwamba ufalme wake ni wa kutokuwa na mwisho, wanaendelea katika wimbo: “Anastahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, na aliyetukomboa kwa Mungu kwa damu yake mwenyewe ya damani!”TSHM 316.3

  Siri ya msalaba inaeleza siri zote. Itaonekana ya kwamba yeye anayekuwa pasipo mwisho kwa hekima hangefanya shauri lingine kwa ajili ya wokovu wetu isipokuwa kafara ya Mwana wake. Malipo kwa ajili ya kafara hii ni furaha ya kujaza dunia na viumbe vilivyokombolewa, vitakatifu, vya furaha, na vya milele. Hii ni damani ya nafsi ambayo Baba anatoshelewa kwa bei iliyolipwa. Na Kristo mwenyewe, kwa kutazama matunda ya kafara yake kubwa, anatoshelewa.TSHM 317.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents