Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Tyndale Anatafsiri Agano Jipya kwa Kiingereza

  Alipofukuzwa nyumbani kwa ajili ya mateso, akaenda Londoni na huko kwa mda akatumika bila kizuizi. Lakini tena Wakatoliki wakamlazimisha kukimbia. Uingereza wote ukaonekana wenye kufungwa kwake. Katika Ujeremani akaanza uchapaji wa Agano Jipya kwa lugha ya kingereza. Alipokatazwa kuchapa katika mji moja, akaenda kwa mji mwengine. Mwishowe akasafiri kwenda Worms, ambako, miaka michache mbele, Luther alipotetea injili mbele ya baraza. Katika mji ule kulikuwa rafiki wengi wa Matengenezo. Vitabu elfu tatu vya Agano Jipya vikachapwa, na mchapo mwengine ukafuata.TSHM 115.1

  Neno la Mungu likapenya kwa siri kule Londoni na kuenezwa po pote katika inchi. Wakatoliki wakajaribu kukomesha ukweli, lakini haikuwezekana. Askofu wa Durham akanunua kwa muuzavitabu akiba yote ya Mabiblia kwa kusudi la kuviharibu, kufikiri kwamba jambo hili lingesimamisha kazi. Lakini mali ikatoa vyombo vilivyonunuliwa kwa ajili ya mchapo mpya na bora kuliko. Wakati Tyndale alipofungwa baadaye, uhuru ukatolewa kwake isipokuwa ataje majina ya wale waliomsaidia kwa zawadi zao kwa mchapo wa Mabiblia. Akajibu kwamba askofu wa Durham alifanya zaidi kuliko kila mtu ye yote kwa kulipa bei kubwa kwa ajili ya vitabu vilivyobaki mkononi.TSHM 115.2

  Mwishowe Tyndale akashuhudia imani yake kwa mauti ya mfia dini; lakini silaha alizozitayarisha ziliwezesha waaskari wengine kupigana katika karne nyingi, hata kwa wakati wetu.TSHM 115.3

  Latimer akasema juu ya mimbara kwamba inafaa kusoma Biblia katika lugha ya watu. “Tusichague njia zinazopingana, bali Neno la Mungu lituongoze: tusifuate ... mababu zetu, wala kufuata yale waliyotenda, bali yale waliyopaswa kufanya.”TSHM 115.4

  Barnes na Frith, Ridley na Cranmer, waongozi katika Matengenezo ya Uingereza walikuwa wataalamu, wakaheshimiwa sana kwa bidii ao kwa utawa katika ushirika wa Kiroma. Upinzani wao kwa kanisa la Roma ulikuwa ni matokeo ya maarifa yao ya kuvumbua makosa ya “kiti kitakatifu”.TSHM 115.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents