Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Roma Inakutana na Dini ya Biblia

    Lakini Roma ilikusudia kuweka Uingereza chini ya mamlaka yake. Katika karne ya sita wajumbe (missionnaires) wake wakajaribu kutubisha Wasaxons wapagani. Jinsi kazi ilivyoendelea, waongozi wa kiPapa wakakutana na Wakristo wa zamani za kale -wapole, wanyenyekevu, wenye kupatana na maneno ya Maandiko katika tabia, mafundisho, na wa mwenendo mwema. Wale wakiroma walionyesha imani ya mambo ya uchawi, ukuu, na kiburi cha kipapa. Roma alilazimisha kwamba makanisa haya ya Kikristo yapate kukubali mamlaka ya askofu mkuu. Waingereza wakajibu kwamba Papa hakutajwa kuwa mkuu katika kanisa na wangeweza kumtolea tu utii ule unaofaa kwa kila mfuasi wa Kristo. Hawakujua bwana mwingine isipokuwa Kristo.TSHM 21.5

    Sasa roho ya kweli ya kanisa la Roma ikafunuliwa. Akasema mwongozi wa Roma: “Kama hamutapokea wandugu wanaowaletea amani, mutapokea maadui watakaowaletea vita”. Vita na udanganyifu vikatumiwa juu ya washahidi hawa kwa ajili ya imani ya Biblia, hata wakati makanisa ya Waingereza ya kaharibiwa au kulazimishwa kutii Papa.TSHM 22.1

    Katika inchi iliyokuwa mbali na mamlaka ya Roma, kwa karne nyingi miili ya Wakristo iliishi na usalama kidogo bila uovu wa kipapa. Waliendelea kutumia Biblia kuwa kiongozi pekee cha imani. Wakristo hawa waliamini umilele wa sheria ya Mungu na walishika Sabato ya amri ya ine. Makanisa walioshika imani hii na kuitumia waliishi katika Afrika ya Kati na miongoni mwa Waarmenia wa Asia.TSHM 22.2

    Kwa wale waliosimama imara mamlaka ya Papa, Wavaudois (Waldenses) walisimama wa kwanza. Katika inchi kanisa za Kiroma ziliimarisha kiti chake, makanisa ya Piedmont yakadumisha uhuru wao. Lakini wakati ukakuja ambapo Roma ilishurutisha juu ya utii wao. Lakini wengine, walikataa kujitoa kwa Papa ao maaskofu, wakakusudia kulinda usafi na unyenyekevu wa imani yao. Utengano ukatokea. Wale walioambatana na imani ya zamani sasa wakajitenga. Wengine, kwa kuacha inchi yao ya Alpes za milima mirefu (Alps), wakainua mwenge ya ukweli katika inchi za kigeni. Wengine wakakimbilia katika ngome za miamba ya milima na huko wakalinda uhuru wao wa kuabudu Mungu.TSHM 22.3

    Imani yao ya dini iliimarishwa juu ya Neno la Mungu lenye kuandikwa. Wakulima hao wanyenyekevu, waliofungiwa inje ya ulimwengu, hawakufikia wao wenyewe kwa ukweli katika upinzani wa mafundisho ya kanisa la uasi. Imani ya dini yao ilikuwa uriti wao kutoka kwa mababa zao. Walitoshelewa kwa ajili ya imani ya kanisa la mitume. “Kanisa jangwani”, sio serekali ya kanisa la kiburi iliyotawazwa katika mji mkubwa wa ulimwengu, lililokuwa kanisa la kweli la Kristo, mlinzi wa hazina za ukweli ambazo Mungu alizoweka kwa watu wake kwa kutolewa kwa ulimwengu.TSHM 22.4

    Miongoni mwa sababu muhimu zilizoongoza kwa utengano wa kanisa la kweli kutoka kwa kanisa la KiRoma ilikuwa ni uchuki wa kanisa hili juu ya Sabato ya Biblia. Kama ilivyotabiriwa na unabii, mamlaka ya kanisa la KiRoma likagandamiza sheria ya Mungu katika mavumbi. Makanisa chini ya kanisa la Roma yakalazimishwa kuheshimu siku ya kwanza (Dimanche). Kwa kosa la kupita kawaida wengi miongoni mwa watu wa kweli wa Mungu wakafazaika sana hata ingawa walishika Sabato, wakaacha kutumika pia siku ya kwanza ya juma (Dimanche). Lakini jambo hilo halikuwafurahisha waongozi wa Papa. Walilazimishwa kwamba Sabato ichafuliwe, na wakashitaki wale waliosubutu kuonyesha heshima yake.TSHM 23.1

    Mamia ya miaka kabla ya Matengenezo (Reformation) Wavaudois (Waldenses) walikuwa na Biblia katika lugha yao yenyewe. Jambo hili likawatelea kuteswa kulikowengine. Wakatangaza Roma kuwa Babeli mkufuru wa Ufunuo. Katika hatari ya maisha yao wakasimama imara kushindana na maovu yake. Katika miaka ya uasi kulikuwa Wavaudois (Waldenses) waliokana mamlaka ya Roma, wakakataa ibada ya sanamu kama kuabudu miungu, na wakashika Sabato ya kweli. (Tazama Nyongezo).TSHM 23.2

    Nyuma ya ngome za juu sana za milima Wavaudois wakapata mahali pa kujificha. Hawa wakimbizi waaminifu wakaonyesha watoto wao urefu wa munara juu yao katika ukuu na wakasema juu ya yule ambaye Neno lake linakuwa la kudumu kama milima ya milele. Mungu aliimarisha milima; si mkono lakini ule unaokuwa na uwezo usio na mwisho ungaliweza kuihamisha. Kwa namna ile ile akaimarisha sheria yake. Mkono wa mtu haungeweza kuongoa milima na kuitupa kwa nguvu baharini, kama vile hauwezi kubadili sheria moja ya Mungu. Wasafiri hawa hawakunungunika kwa sababu ya taabu ya mateso yao; hawakuwa peke yao katika ukiwa wa milima. Walijifurahisha katika uhuru wao kwa ibada. Kutoka ngome ya juu waliimba sifa za Mungu, na majeshi ya Roma hawakuweza kunyamazisha nyimbo zao za shukrani.TSHM 23.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents