Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Umoja wa Upagani na Ukristo

  Kanisa la Katoliki la Roma, kwa kuunganisha upagani na Ukristo, na, kama upagani, kusingizia tabia ya Mungu, lilitumia basi matendo makali. Vyombo vya mateso vilishurutisha watu kukubali mafundisho yake. Wakuu wa kanisa wakajifunza kuvumbua njia za kufanyiza mateso makubwa iwezekanavyo bila kuondoa maisha ya wale wasingekubali madai yake. Kwa mara nyingi yule aliyeteswa alipokea mauti kuwa kufunguliwa kuzuri.TSHM 278.1

  Kwa wafuasi wa Roma kanisa lilikuwa na malezi ya shida, njaa, ya mateso ya mwili. Kwa kupata kibali cha Mungu, wenye kutubu walifundishwa kupasua vifungo ambavyo Mungu alivifanya kwa kubariki na kufurahisha maisha ya mwanadamu duniani. Uwanja wa kanisa unakuwa na mamilioni ya watu waliotoa maisha yao kwa masumbuko ya bure, kwa kukomesha, kama machukizo kwa Mungu, kila wazo na nia ya huruma kwa viumbe wenzao.TSHM 278.2

  Mungu hakuweka kamwe mojawapo ya mizigo hii mzito juu watu wo wote. Kristo hakutoa mfano kwa wanaume na wanawake kujifungia wenyewe katika nyumba ya watawa (monasteres) ili kuweza kustahili kuingia mbinguni. Hakufundisha kamwe ya kwamba mapendo yanapashwa kukomeshwa.TSHM 278.3

  Papa anadai kuwa mjumbe mkubwa wa Kristo. Lakini je, Kristo alijulikana daima kutupa watu kwa gereza kwa sababu hawakumtolea heshima kubwa kama Mfalme wa mbingu? Je, sauti yake ilisikiwa kuhukumu kwa mauti wale wasiomkubali?TSHM 278.4

  Kanisa la Roma sasa linaonyesha uso mzuri kwa ulimwengu, kufunika kwa maneno ya kujitetea ukumbusho wake wa maovu ya kuchukiza. Limejivika lenyewe mavazi ya mfano wa Kikristo, lakini linakuwa lisilobadilika. Kanuni yo yote ya dini ya Roma katika vizazi vya wakati uliopita inakuwako leo. Mafundisho yaliyoshauriwa kwa miaka ya giza yangali yanashikwa. Dini ya Roma ambayo Waprotestanti wanaheshimu sasa ni ileile iliyotawala katika siku za Matengenezo (Reformation), wakati watu wa Mungu waliposimama kwa hatari ya maisha yao kufunua zambi lake.TSHM 278.5

  Kanisa la Roma ni kama vile unabii ulivyotangaza kwamba lingekuwa, ni kukufuru kwa nyakati za mwisho. Tazama 2 Watesalonika 2 :3,4. Chini ya mfano wa kigeugeu linaficha sumu isiyobadilika ya nyoka. Je, uwezo huu, ambao ukumbusho wake kwa miaka elfu umeandikwa katika damu ya watakatifu, utakubaliwa kama sehemu ya kanisa la Kristo?TSHM 278.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents