Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uadui Juu ya Kristo

  “Mahali pia Bwana wetu alisulibiwa.” Jambo hili vile vile lilitimilika kwa Ufransa. Hakuna inchi ambayo ukweli ulikutana na upinzani wa ukaidi kama Ufransa. Katika mateso iliyozuriwa kwa washahidi wa injili, Ufransa ulisulibisha Kristo katika mwili wa wanafunzi wake.TSHM 126.4

  Karne kwa karne damu ya watakatifu ilikuwa ikimwangika. Huku Wawaldense (Vaudois) walitoa maisha yao kwa milima ya Piedmont (kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu Kristo,” ushuhuda wa namna ile ile uliochukuliwa na Albigeois wa Ufransa. Wanafunzi wa Matengenezo waliouawa kwa mateso ya ajabu. Mfalme na wakuu, wanawake wa kizazi cha juu na wabinti wazuri walishibisha macho kwa maumivu makuu ya wafia dini wa Yesu. Wahuguenots washujaa walimwaga damu yao pahali pa mapigano makali, kuwindwa kama wanyama wa mwitu.TSHM 126.5

  Wazao wachache wa Wakristo wa zamani waliobaki kwa karne ya kumi na nane wakajificha katika milima ya Kusini, wakalinda imani ya mababa zao. Wakatembea kwa shida kwa maisha marefu ya utumwa ndani ya mashua ya vita (galères). Watu wa malezi safi sana na wenye akili wa Ufransa waliishi katika minyororo, katika mateso mabaya sana, kati ya wanyanganyi na wauaji. Wengine wakapigwa risasi na kuanguka katika damu ya baridi wanapoanguka kwa magoti yao katika sala. Inchi yao, ikateketezwa kwa upanga, shoka, na kwa moto, “ikageuka kuwa jangwa kubwa, la giza.” “Mambo haya mabaya sana yakaendelea ... katika nyakati zisizokuwa za giza bali katika wakati wa nuru wa Louis XIV. Elimu iliongezeka, vitabu ao maarifa yakaendelea vizuri, walimu wa elimu ya tabia na sifa za Mungu wa baraza ya hukumu na wa mji mkuu walikuwa wenye maarifa (savants) na wasemaji, wakavutwa na neema ya upole na upendo.”TSHM 127.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents