Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  “Wende na Ulihubiri kwa Uiimwengu”

  “Wakati nilikuwa katika kazi zangu,” akasema, “nikasikia sauti kukariri katika masikio yangu, `Wende na uambie ulimwengu hatari yao.’ Maneno haya yalikuwa yakitokea daima kwangu: `Wakati ninapomwambia mwovu; kama mwovu Ee mwovu, hakika utakufa, wala husemi kuonya mwovu aache njia yake; mwovu yule atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.’ Nikaona kama mwovu angeweza kuonywa, wengi miongoni mwao wangalitubu; na kama hawakuonywa, damu yao ingeweza kutakwa mkononi mwangu.” Maneno yalikuwa yakimrudia kwa akili yake: “Wende na ulihubiri kwa ulimwenguni; damu yao nitaitaka mkononi mwako.” Akangoja mda wa miaka tisa, mzigo ulizidi kulemea kwa roho yake, hata katika mwaka 1831 yeye kwa mara ya kwanza kwa wazi akatoa sababu za imani yake.TSHM 157.4

  Alikuwa sasa na miaka makumi tano, hakuzoea kusema mbele ya watu wengi, lakini kazi zake zikabarikiwa. Mafundisho yake ya kwanza yakafuatwa na mwamusho wa dini. Jamaa kumi na tatu isipokuwa tofauti ya watu wawili,zilitubu. Alikuwa akilazimishwa kuhubiri kwa mahali pengine, na karibu pahali pote wenye zambi walikuwa wakigeuka. Wakristo waliamshwa kwa utakaso mkubwa, na watu wenye imani ya kuwako kwa Mungu lakini hawakubali mambo ya dini na makafiri (wasioamini) wakaongozwa kwa maarifa ya ukweli wa Biblia. Mahubiri yake yakaamsha akili ya watu na kuzuia mambo ya anasa ya kidunia yaliyokuwa yakikua na ya kutamanisha maisha.TSHM 157.5

  Katika mahali pengi makanisa ya Kiprotestanti karibu aina zote wakamfungulia kwake, na mialiko mara kwa mara ikaja kutoka kwa wahuduma. Ilikuwa desturi yake ya kutotumika mahali wasipomwalika, lakini kwa upesi akajiona mwenyewe hawezi kutimiza hata kwa nusu ya mialiko iliyokuwa ikimfikia. Wengi wakasadikishwa kwa hakika na ukaribu wa kuja kwa Kristo na mahitaji yao ya kujitayarisha. Katika miji mikubwa mingine, wenye duka ya vileo vikali na wakageuza duka zao kuwa vyumba vya mikutano; nyumba za michezo ya kamari zikavunjwa; makafiri na hata na wapotovu walioachwa wengi wakabadilika. Mikutano ya maombi ikaanzishwa na makanisa mbali-mbali karibu kila saa, wachuuzi wakakusanyika wakati wa jua kali kwa kuomba na kusifu. Hapo hapakuwa na wasiwasi wa kupita kiasi. Kazi yake kama ile ya Watengenezaji wa kwanza ikaamsha zamiri kuliko kuchocheza tamaa tu.TSHM 158.1

  Katika mwaka 1833 Miller akapokea ruhusa ya kuhubiri kwa Kanisa la Baptiste. Hesabu kubwa ya wahuduma wa kanisa lake wakakubali kazi yake; ilikuwa ni kwa ukubali wao wa kawaida ambao akaendelea na kazi zake. Akasafiri na kuhubiri bila kukoma, bila kupokea mali ya kutosha kwa ajili ya gharama ya kusafiri kwa mahali alipoalikwa, hivi kazi yake kwa ajili ya watu wote ilikuwa kodi nzito kwa mali yake.TSHM 158.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents