Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ujumbe wa Waadventisti katika Uingereza

    Mwanzoni wa mwaka 1826 ujumbe wa kuja kwa kristo ukaanza kuhubiriwa katika Uingereza. Kwa kawaida, tarehe kamili ya kurudi kwa Yesu haikufundishwa, lakini ukweli wa kuja kwa Kristo mwenye uwezo na utukufu ukatangazwa kwa watu wengi. Mwandishi mmoja wa Kingereza akasema kwamba karibu wahuduma 700 wa kanisa la Uingereza walijitoa katika kuhubiri “habari njema hii ya ufalme.”TSHM 173.5

    Ujumbe ulioonyesha mwaka 1844 kuwa wakati wa kuja kwa Bwana ukatolewa vilevile katika Uingereza. Maandiko juu ya habari ya kurudi yakatangazwa sana kutoka America. Katika mwaka 1842 Robert Winter, Mwingereza aliyeamini kurudi kwa Yesu alipokuwa America, akarudi katika inchi yake na kutangaza habari ya kuja kwa Bwana. Watu wengi wakajiunga naye katika kazi ndani ya sehemu mbalimbali za Ungereza.TSHM 174.1

    Katika upande wa America ya kusini, Lacunza, “Jesuite” wa Espania, akakubali ukweli wa kristo kurudi upesi. Kutaka kuepuka karipio la Roma, akatangaza habari yake chini ya jina la kujitwalia la Rabbi-Ben-Ezra, akajionyesha mwenyewe kama Muyahudi aliyegeuka. Karibu ya mwaka 1825 kitabu chake kitatafsiriwa katika Kiingereza. Kilitumiwa kwa kuongeza usikizi uliokwisha kuamshwa katika Uingereza.TSHM 174.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents