Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Uwezo wa Neno

    Makelele haikukawia kuenea katika Wittenberg kwamba Luther alirudi na alitaka kuhubiri. Kanisa likajaa. Kwa hekima kubwa na upole akafundisha na kuonya: “Misa ni kitu kibaya; Mungu huchukia kitu hiki; kinapaswa kuharibiwa. ... Lakini mtu asiachishwe kwacho kwa nguvu. ... Neno ... la Mungu linapasa kutenda, na si sisi. ...Tunakuwa na haki kusema: hatuna na haki kutenda. Hebu tuhubiri; yanayobaki ni ya Mungu. Nikitumia nguvu nitapata nini? Mungu hushika moyo na moyo ukikamatwa, umekamatika kabisa. ...TSHM 87.1

    “Nitahubiri, kuzungumza, na kuandika; lakini sitamshurutisha mtu, kwani imani ni tendo la mapenzi. ... Nilisimama kumpinga Papa, vyeti vya kuachiwa zambi, na wakatoliki, lakini bila mapigano wala fujo. Ninaweka Neno la Mungu mbele; nilihubiri na kuandika--ni jambo hili tu nililolifanya. Na kwani wakati nilipokuwa nikilala, ... neno ambalo nililohubiri likaangusha mafundisho ya kanisa la Roma, ambaye hata mtawala ao mfalme hawakulifanyia mambo mengi mabaya. Na huku sikufanya lolote; neno pekee lilitenda vyote.” Neno la Mungu likavunja mvuto wa mwamusho wa ushupavu. Injili ilirudisha katika njia ya Kweli watu waliodanganywa.TSHM 87.2

    Miaka nyingi baadaye ushupavu wa dini ukainuka pamoja na matokeo ya ajabu. Akasema Luther: “Kwao Maandiko matakatifu yalikuwa lakini barua yenye kufa, na wote wakaanza kupaaza sauti, ‘Roho! Roho! ‘ Lakini kwa uhakika sitafuata mahali ambapo roho yao inawaongoza.”TSHM 87.3

    Thomas Munzer, alikuwa na bidii zaidi miongoni mwa washupavu hawa, alikuwa mtu wa uwezo mkubwa, lakini hakujifunza dini ya kweli. “Alipokuwa na mapenzi ya kutengeneza dunia, na akasahau, kama wenye bidii wote wanavyofanya, kwamba ilikuwa kwake mwenyewe ambaye Matengenezo ilipashwa kuanzia.” Hakutaka kuwa wa pili, hata kwa Luther. Yeye mwenyewe akajidai kwamba alipokea agizo la Mungu kuingiza Matengenezo ya kweli: “Ye yote anayekuwa na roho hii, anakuwa na imani ya kweli, ijapo hakuweza kuona Maandiko katika maisha yake.”TSHM 87.4

    Waalimu hawa wa bidii wakajifanya wenye kutawaliwa na maono, kuona kuwa kila mawazo na mvuto kama sauti ya Mungu. Wengine hata wakachoma Biblia zao. Mafundisho ya Munzer yakakubaliwa na maelfu. Kwa upesi akatangaza kwamba kutii watawala, ilikuwa kutaka kumtumikia Mungu na Beliali.TSHM 88.1

    Mafundisho ya uasi ya Munzer yakaongoza watu kuvunja mamlaka yote. Sherehe za kutisha za upinzani zikafuata, na mashamba ya Ujeremani yakajaa na damu.TSHM 88.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents