Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    40 / WATU WA MUNGU WANAKOMBOLEWA

    Wakati ulinzi wa sheria za kibinadamu zitakapoondolewa kutoka kwa wale wanaoheshimu sheria ya Mungu, katika inchi mbalimbali kutakuwa mwendo wa namna moja kwa ajili ya maangamizi yao. Kwa namna wakati ulioamriwa katika agizo unapokaribia, watu watafanya shauri pamoja usiku mmoja shauri la kuangamiza kwa pigo litakalonyamazisha washupavu na wasiotii.TSHM 309.1

    Watu wa Mungu wengine wapo katika vyumba vya gereza, wengine mwituni na katika milima--wanaomba ulinzi wa Mungu. Watu wenye silaha, wakilazimishwa na malaika waovu, wanajitayarisha kwa kazi ya mauti. Sasa, kwa saa ya mwisho kabisa, Mungu atajitia kati kati: “Mutakuwa na wimbo kama vile wakati wa usiku, wakati karamu takatifu inapotakaswa; na furaha ya moyo kama vile mtu anavyokwenda... katika mlima wa Bwana, aliye Mwamba wa Israeli. Na Bwana atafanya sauti yake ya utukufu kusikiwa, naye ataonyesha kushuka kwa mkono wake, wa nuru, kwa gazabu ya kasirani yake, na ulimi wa moto unaokula, pamoja na zoruba na garika na mvua ya mawe”: Isaya 30:29,30.TSHM 309.2

    Makutano makubwa ya watu waovu yanakuwa karibu kushambulia juu ya mawindo yake, wakati giza kubwa, nzito kuliko usiku, inaanguka duniani. Ndipo upindi wa mvua unazunguka mbingu kuonekana kuzunguka kila kundi la maombi. Makutano yenye kasirani yamefungwa. Makusudi ya hasira yao yamesahauliwa. Wanatazama kwa mfano wa agano la Mungu na kutamani kulindwa kwa utukufu wake.TSHM 309.3

    Kwa watu wa Mungu sauti imesikiwa, kusema, “Tazama”. Kama Stefano wanatazama na wanaona utukufu wa Mungu na wa Mwana wa watu katika kiti chake cha enzi. Tazama Matendo 7:55, 56. Wanatambua alama za unyenyekevu wake, na wanasikia ombi, “nataka sana hawa ulionipa wakae pamoja nami pahali nilipo”. Yoane 17:24. Sauti imesikiwa ikisema, “Wanakuja, watakatifu, wapole, na safi! Wameshika neno la uvumilivu wangu”.TSHM 309.4

    Kwa usiku wa manane Mungu anaonyesha uwezo wake kwa ajili ya ukombozi wa watu wake. Jua linatokea likingaa kwa nguvu zake. Alama na maajabu yanafuata. Waovu wanatazama kwa hofu kuu kwa tokeo lile, huku wenye haki wakitazama alama za ukombozi wao. Katikati ya mbingu zenye hasira kukaonekana nafasi moja wazi ya utukufu usioelezeka na pale sauti ya Mungu ikatokea kama sauti ya maji mengi, ikisema, “imefanyika! ” Ufunuo 16:17.TSHM 309.5

    Sauti inatetemesha mbingu na dunia. Hapo ni tetemeko kubwa la inchi, “hata tangu watu walipokuwa juu ya dunia halikuwa namna ile, namna lilivyokuwa kubwa tetemeko hili. ” Ufunuo 16:18. Miamba iliyopasuka ikatawanyika pande zote. Bahari ikatikisatikisa kwa hasira kali. Hapo kunasikiwa mlio wa nguvu wa tufani kama sauti ya mashetani. Upande wa juu wa inchi ukapasuka. Misingi yake yenyewe yaonekana kutoweka. Miji yenye bandari iliyokuwa kama Sodomo kwa ajili ya uovu imemezwa kwa maji yenye hasira. “Babeli ule mkubwa” ukakumbukwa mbele ya Mungu, “kupewa kikombe cha mvinyo ya gazabu ya kasirani yake. ” Ufunuo 16:19. Mvua ya mawe makubwa sana ikafanya kazi yake ya uharibifu. Miji yenye kiburi inaangushwa chini. Majumba ya fahari ambayo watu walitolea mali nyingi yao ikafunikwa na ikageuka mavumbi mbele ya macho yao. Kuta za gereza zimevunjika kwa vipande vipande, na watu wa Mungu wamewekwa huru.TSHM 310.1

    Makaburi yamefunguka, na “wengi wao wanaolala mavumbini mwa inchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, na wengine kwa haya na kuzarauliwa kwa milele”. “Na wale waliomuchoma”, wale ambao walichekelea maumivu makali ya kifo cha Kristo, na wapinzani (adui) wakali zaidi wa kweli yake, watafufuka kuona heshima inayowekwa kwa waaminifu na watiifu. Danieli 12:2; Ufunuo 1:7.TSHM 310.2

    Umeme kali utafunika dunia kwa shuka la ndimi ya moto. Juu ya ngurumo (radi), sauti za ajabu na hofu kubwa, zinatangaza mwisho wa waovu. Wale waliokuwa wenye kujisifu na wenye kutaka vita, wakali kwa wenye kushika amri za Mungu, sasa wanatetemeka kwa woga. Mashetani wanatetemeka wakati watu wanapoomba rehema.TSHM 310.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents