Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uhodari wa Mfia Dini

  Wakati Mtengenezaji alipoendelea mbele, makundi kwa hamu kubwa kwa kusongana karibu naye na kwa sauti za upole wakamuonya juu ya Waroma. “Watakuchoma”, akasema mwengine, “na kugeuza mwili wako kuwa majivu, kama walivyomfanya Jean Huss.” Luther akajibu, “ijapo wangewasha moto njiani mote toka Worms hata Wittenberg, ... ningetembea kati kati yake kwa jina la Bwana; ningeonekana mbele yao, ... kushuhudia Bwana Yesu Kristo.”TSHM 68.4

  Kukaribia kwake huko Worms kukafanya msukosuko mkubwa. Rafiki wakatetemeka kwa ajili ya usalama wake; maadui wakaogopa kwa ajili ya maneno yao. Kwa ushawishi wa wapadri akalazimishwa kwenda kwa ngome ya mwenye cheo mwema, mahali, ilitangazwa, magumu yote yangeweza kutengenezwa kwa kirafiki. Warafiki wakaonyesha hatari zilizomngoja. Luther, bila kutikisika, akatangaza: “Hata kukiwa mashetani wengi ndani ya mji wa Worms kama vigae juu ya nyumba, lazima nitaingia.”TSHM 68.5

  Alipofika Worms, makundi ya watu wengi sana yakakusanyika kwa milango ya mji kwa kumukaribisha. Kulikuwa wasiwasi nyingi sana. “Mungu atakuwa mkingaji wangu,” akasema Luther alipokuwa akishuka kwa gari lake. Kufika kwake kulijaza wapadri hofu kuu. Mfalme akawaita washauri wake. Ni upande gani unaopashwa kufuatwa? Padri mmoja mkali akatangaza: “Tumeshauriana mda mrefu juu ya jambo hili. Mfalme mtukufu uondoshe mbio mtu huyu. Upesi, Sigismund hakuwezesha John Huss kuchomwa? Hatulazimishwe kutoa cheti cha mpinga imani ya dini wala kuliheshimu.m “Hapana,” akasema mfalme, “tunapashwa kushika ahadi yetu.” Tulipatana kwamba Mtengenezaji angepashwa kusikiwa.TSHM 68.6

  Mji wote ulitamani kuona mtu huyu wa ajabu. Luther, mwenye kuchoka sababu ya safari, alihitaji ukimya na pumziko. Lakini alifurahia pumziko ya saa chache wakati watu wa cheo kikuu, wenye cheo, wapadri, na wanainchi walimuzunguka kabisa. Kati ya watu hawa walikuwa wenye cheo walioomba na juhudi kwa mfalme matengenezo ya matumizi mabaya ya kanisa. Maadui pamoja na rafiki walifika kumtazama mwa shujaa. Kuvumulia kwake kulikuwa imara na kwa uhodari. Uso wake mdogo wakufifia, ulikuwa uso wa upole na hata wa furaha. Juhudi nyingi ya maneno yake ikatoa uwezo ambao hata maadui zake hawakuweza kusimama kabisa. Wengine walisadikishwa kwamba mvuto wa Mungu ulikuwa naye; wengine wakatangaza, kama walivyofanya wafarisayo juu ya Kristo: “Ana pepo.” Yoane 10:20.TSHM 69.1

  Kwa siku iliyofuata afisa mmoja wa mfalme akaagizwa kumpeleka Luther kwa chumba kikubwa cha wasikilizaji. Kila njia ilijaa na washahidi wenye shauku ya kutazama juu ya mtawa aliyesubutu kushindana na Papa. Jemadari mzee mmoja, aliyeshinda vita nyingi, akamwambia kwa upole: “Maskini mtawa, unataka sasa kwenda kufanya vita kubwa kuliko vita mimi ao kapiteni wengine waliofanya katika mapigano ya damu nyingi. Lakini, ikiwa kama madai yako ni ya haki, ...endelea katika jina la Mungu,na usiogope kitu chochote. Mungu hatakuacha.”TSHM 69.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents