Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  6 / KIFO KIMEWAFIKIA MACHONI WASHUJAA WAWILI

  Mwanzoni kwa karne ya tisa Biblia ilikuwa imekwisha kutafsiriwa na ibada ya watu wote ikafanyika katika lugha ya watu wa Bohemia. Lakini Gregoire VII alikusudia kuweka watu utumwani, na tangazo likatolewa kukataza ibada ya watu katika lugha ya Kibohemia. Papa akatangaza kwamba “ilikuwa ni furaha kwa Mwenye enzi yote kwamba ibada yake ifanyiwe katika lugha isiyojulikana.” Lakini Mungu anaweka tayari wajumbe kwa kulinda kanisa. Wavaudois wengi na Waalbigenses, walipofukuzwa kwa ajili ya mateso, wakaja Bohemia. Wakatumika kwa bidii katika siri. Kwa hiyo imani ya kweli ikalindwa.TSHM 39.1

  Mbele ya siku za Huss kulikuwa watu katika Bohemia waliohukumu machafu ndani ya kanisa. Vitisho vya serkali ya kanisa vikaamshwa, na mateso yakafunguliwa juu ya injili. Baada ya mda ikaamriwa kwamba wote waliotoka kwa ibada ya kanisa la Roma walipaswa kuchomwa. Lakini Wakristo, wakaendelea mbele kushinda kwa kusudi lao. Mmoja akatangaza alipokuwa akifa, “Kutainuka mmoja kutoka miongoni mwa watu, bila upanga wala mamlaka, na juu yake hawataweza kumushinda.” Tayari mmoja alikuwa akipanda, ambaye ushuhuda wake wa kupinga Roma utashitusha mataifa.TSHM 39.2

  Yohana Huss alikuwa mnyenyekewa tangu kuzaliwa na alikuwa ameachwa mapema yatima kwa ajili ya kifo cha baba yake. Mama yake mtawa, kuzania elimu na kuogopa ya Mungu kama hesabu kuwa thamani ya vile tunavyo, akatafuta kulinda urithi huu kwa ajili ya kijana wake. Huss alijifunza kwa chuo cha jimbo, baadaye akaenda kwa chuo kikubwa (universite) kule Prague, kwa sababu ya umaskini wake akapokelewa kwa bure.TSHM 39.3

  Kwa chuo kikubwa, kwa upesi Huss akajitofutisha kwa ajili ya maendeleo yake ya upesi. Upole wake, alipokwisha kupata mwenendo (tabia) ukampatia heshima ya ulimwengu. Alikuwa mshiriki mwaminifu wa Kanisa la Roma na mwenye kutafuta na juhudi mibaraka ya kiroho. Kanisa la Roma linajidai kutoa. Baada ya kutimiza majifunzo yake ya college, akaingia katika ukasisi (upadri). Kwa haraka alipofikia cheo kikuu, akapelekwa kwa jumba la mfalme. Akafanywa pia mwalimu (fundi) wa chuo kikuu na baadaye mkuu wa chuo kikuu (recteur). Mwanafunzi mwema munyenyekevu akawa kiburi cha inchi yake, jina lake likajulikana po pote katika Ulaya.TSHM 39.4

  Jerome, ambaye baadaye alishirikiana na Huss, akaleta toka Uingereza maandiko ya Wycliffe. Malkia wa Uingereza, aliyegeuzwa na mafundisho ya maisha ya Wycliffe, alikuwa binti wa mfalme wa Bohemia. Kwa njia ya mvuto wake kazi za Mtengenezaji zikatangazwa sana katika inchi yake ya kuzaliwa. Huss akainama na kukubali kwa heshima matengenezo yaliyoletwa. Tayari, ingawa hakuijua, akaingi kwa njia ambayo iliweza kumwongoza mbali sana ya Roma.TSHM 40.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents