Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    23 / SIRI YA WAZI YA PAHALI PATAKATIFU

    Maandiko ambayo ni ya juu ya mengine yalikuwa vyote viwili, msingi na nguzo ya katikati ya imani ya kuja kwa Yesu ilikuwa tangazo, “Hata mangaribi na asubui ya siku elfu mbili mia tatu; halafu Pahali patakatifu patatakaswa.” Danieli 8:14. Haya yalikuwa maneno ya mazoezi kwa waamini wote juu ya kuja upesi kwa Bwana. Lakini Bwana hakutokea. Waamini walijua kwamba Neno la Mungu halitaweza kushindwa; maelezo yao ya unabii yalikuwa na kosa. Lakini kosa lilikuwa wapi?TSHM 196.1

    Mungu aliongoza watu wake katika mwendo mkubwa wa kuja kwa Yesu. Hangeuruhusu mwisho wake uwe wa giza na uchungu, kulaumiwa kama wa uwongo na wa ushupavu. Ijapo wengi wakaacha kuhesabia nyakati zao za unabii na wakakana msingi ulioimarishwa mwendo, wengine hawakutaka kukataa mambo ya imani na maisha yaliyokubaliwa na Maandiko na Roho wa Mungu. Ilikuwa wajibu wao kushikilia kwa nguvu ukweli waliyokwisha kupata. Kwa maombi ya juhudi wakajifunza Maandiko kwa kuvumbua kosa lao. Kwa namna hawakuweza kuona kosa kwa hesabu zao za nyakati za unabii, wakachunguza zaidi sana fundisho la Pahali patakatifu.TSHM 196.2

    Wakajifunza kwamba hakuna ushahidi wa Maandiko unaokubali maoni ya watu wengi kwamba dunia ni Pahali patakatifu; lakini wakapata maelezo kamili ya Pahali patakatifu; asili yake, pahali, na matumizi:TSHM 196.3

    “Basi hata agano la kwanza lilikuwa na amri ya kuabudu Mungu, na Pahali patakatifu pake pa dunia. Maana hema ilitengenezwa ile ya kwanza iliyokuwa na taa, na meza na mikate ya onyesho kwa Mungu, palipoitwa Pahali patakatifu. Na nyuma ya pazia la pili, ilikuwa hema iliyoitwa Pahali patakatifu pa patakatifu, yenye kifukizo cha zahabu na sanduku ya agano iliyofunikwa na zahabu pande zote, na ndani yake kulikuwa kopo la zabahu yenye mana, na fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vibao vya agano; na juu yake makerubi ya zahabu, yakitia kivuli juu ya kiti cha rehema:” Waebrania 9:1-5.TSHM 196.4

    “Pahali patakatifu” ilikuwa ni hema iliyojengwa na Musa kwa agizo la Mungu kama pahali pa kukaa pa kidunia pa Mwenyezi Mungu. “Na wanifanyie Pahali patakatifu; nipate kukaa katikati yao” (Kutoka 25:8), ilikuwa ni agizo lililotolewa kwa Musa. Hema wala maskani ilikuwa ni umbo kubwa la fahari. Zaidi ya uwanja wa inje, hema yenyewe ilikuwa na vyumba viwili vilivyoitwa Pahali patakatifu na Pahali patakatifu pa patakatifu, vilivyogawanywa na pazia nzuri sana, Kifuniko cha namna moja kilifunga mlango kwa chumba cha kwanza.TSHM 196.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents