Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kutiwa giza kwa jua na Mwezi

  Miaka makumi mbili na tano baadaye ishara ingine iliotajwa katika unabii ikaonekana -Kutiwa giza kwa jua na mwezi. Wakati wa kutimilika kwake kulionyeshwa kabisa katika mazungumzo ya Mwokozi na wanafunzi wake juu ya mlima wa Mizeituni. “Katika siku zile nbaada ya mateso yale, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa nuru yake.” Marko 13:24. Siku 1260, ao miaka, zilimalizika katika mwaka 1798, robo ya karne mbele, mateso yalikuwa karibu kuisha kabisa. Kufuata mateso haya, jua likatiwa giza. Kwa tarehe 19 mai 1780, unabii huu ukatimilika.TSHM 143.5

  Shahidi aliyejionea kwa macho katika Massachusetts akaeleza jambo hili kama ifuatavyo: “Wingu nzito sana likatawanyika juu ya mbingu nzima isipokuwa ukingo mwembamba juu ya upeo wa macho, na ilikuwa giza kama inavyokuwa kwa kawaida saa tisa kwa majira ya baridi jioni...TSHM 144.1

  “Woga, mashaka, na hofu polepole vikajaa mioyoni mwa watu. Wanawake wakasimama mlangoni, kutazama juu ya kipande cha inchi ya giza; watu wakarudi kutoka kazini mwao katika mashamba; sermala akaacha vyombo vyake, mhunzi kuacha kiwanda chake, mchuuzi kuacha meza yake. Vyuo vikafungwa, na kwa kutetemeka watoto wakakimbilia kwao. Wasafiri wakaenda kutafuta kimbilio karibu sana ya nyumba ya mashamba. “Ni kitu gani kita kuja?” Swali hili lilikuwa katika midomo yote na ndani ya moyo. Ilionekana kwamba zoruba kali ilitaka kupita inchini, ao siku ya maangamizi ya vitu vyote.TSHM 144.2

  “Mishumaa ikatumiwa, mioto ya nyumbani ikaangaza kwa mwangaza mwingi kama usiku wa wakati wa baridi, bila mwezi... Kuku wakatoka na kwenda kwa vituo vyao na kwenda kulala, mifugo ikakusanyika kwa fito za malisho na kulala, vyura vikalia, ndege wakaimba nyimbo zao za jioni, na popo wakaruka. Lakini watu walijua kwamba usiku ulikuwa haujafika bado...TSHM 144.3

  “Makutano yakaja pamoja kwa mahali ... pengi. Maneno kwa hotuba zisizo za kawaida kwanza zilikuwa zile zisizogeuka za kuonyesha kwamba giza ililingana na unabii wa Maandiko... Giza ilikuwa nyingi zaidi kwa upesi baada ya saa tano.”TSHM 144.4

  “Kwa sehemu nyingi za inchi ilikuwa kubwa sana katika nyakati za mchana, ambaye watu hawakuweza kutaja saa wala kwa saa ndogo ao kubwa, wala kula chakula, ao kufanya kazi zao za nyumbani, bila nuru ya mishumaa.”TSHM 144.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents