Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Huruma za kuuzisha

  Kanisa la Roma lilifanya Biashara ya Neema ya Mungu. Chini ya maombi ya kuongeza mali kwa ajili ya kujenga jengo la Petro mtakatifu kule Roma, huruma kwa ajili ya zambi zilizotolewa kwa kuuzishwa kwa ruhusa ya Papa. Kwa bei ya uovu hekalu lilipaswa kujengwa kwa ajili ya ibada ya Mungu. Ilikuwa ni jambo hili ambalo liliamusha adui mkubwa sana wa kanisa la Roma na kufikia kwa vita ambayo ilitetemesha kiti cha Papa na mataji matatu juu ya kichwa cha askofu huyu.TSHM 55.4

  Tetzel, mjumbe aliyechaguliwa kuongoza uujishaji wa huruma katika Ujeremani, alikuwa amehakikishwa makosa mabaya juu ya watu na sheria ya Mungu, lakini alitumiwa kwa kuendesha mipango ya faida ya Papa katika Ujeremani. Akasema bila haya mambo ya uongo na hadizi za ajabu kwa kudanganya watu wajinga wanaoamini yasiyo na msingi. Kama wangekuwa na neno la Mungu hawangedanganywa, lakini Biblia ilikatazwa kwao.TSHM 55.5

  Wakati Tetzel alipoingia mjini, mjumbe alimutangulia mbele, kutangaza: “Neema ya Mungu na ya baba mtakatifu inakuwa milangoni mwenu”. Watu wakamkaribisha mtu wa uwongo anayetukana Mungu kama kwamba angekuwa Mungu mwenyewe. Tetzel, kupanda mimbarani ndani ya kanisa, akatukuza uujisaji wa huruma kama zawadi za damani sana za Mungu. Akatangaza kwamba kwa uwezo wa sheti cha msamaha, zambi zote ambazo mnunuzi angetamani kuzitenda baadaye zitasamehewa na “hata toba si ya lazima.” Akahakikishia wasikilizi wake kwamba vyeti vyake vya huruma vilikuwa na uwezo wa kuokoa wafu; kwa wakati ule kabisa pesa inapogonga kwa sehemu ya chini ya sanduku lake, roho inayolipiwa pesa ile itatoroka kutoka toharani (purgatoire) na kufanya safari yake kwenda mbinguni.TSHM 55.6

  Zahabu na feza zikajaa katika nyumba ya hazina ya Tetzel. Wokovu ulionunuliwa na mali ulipatikana kwa upesi kuliko ule unaohitaji toba, imani, na kufanya bidii kwa kushindana na kushinda zambi. (Tazama Nyongezo)TSHM 56.1

  Luther akajazwa na hofu kuu. Wengi katika shirika lake wakanunua vyeti vya msamaha. Kwa upesi wakaanza kuja kwa mchungaji (pasteur) wao, kwa kutubu zambi na kutumainia maondoleo ya zambi, si kwa sababu walitubu na walitamani matengenezo, bali kwa msingi wa sheti cha huruma. Luther akakataa, na akawaonya kwamba isipokuwa walipaswa kutubu na kugeuka, walipaswa kuangamia katika zambi zao. Wakaenda kwa Tetzel na malalamiko kwamba muunganishaji wao alikataa vyeti vyake, na wengine wakauliza kwa ujasiri kwamba mali yao irudishwe. Alipojazwa na hasira, mtawa (religieux) akatoa laana za kutisha, akataka mioto iwake mbele ya watu wote, na akatangaza kwamba “alipata agizo kwa Papa kuunguza wapinga dini wote wanaosubutu kupinga, vyeti vyake vya huruma takatifu zaidi.”TSHM 56.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents